Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Wakuu nina imani wote mko salaama, poleni mlio na changamoto za kibinadamu nazo pia ni sehemu ya Maisha ya mwanadamu zina mwanzo wake na zina mwisho wake pia.

Nina swali wakuu, nini faida ya kombucha kiafya, nini madhara yake kiafya?

Pia kombucha kiimani imekaaje naomba kujua kwa wajuzi wa hapa JF

Kombucha yenyewe ndio hiyo kwenye picha nimeambatanisha.

20230924_123342.jpg
 
Wakuu nina imani wote mko salaama, poleni mlio na changamoto za kibinadamu nazo pia ni sehemu ya Maisha ya mwanadamu zina mwanzo wake na zina mwisho wake pia .

Nina swali wakuu, nini Faida ya kombucha kiafya ,nini madhara yake kiafya

Pia kombucha kiimani imekaaje naomba kujua kwa wajuzi wa hapa jf
Kombucha yenyewe ndio hiyo kwenye picha nimeambatanisha View attachment 2760761
Kwanini usingeanza kutoa kwanza maana ya KOMBUCHA ??, nafikiri itakuwa faida ya mchangiaji kujua achangiacho.
 
Swaadaktaaa!!

Juice yake nilikuwa chachu tamuuu kama alozera!

Nalilikuwa linazaa chapati nyenzake kisha unaibandua na kuiweka kwenye chombo kingine chenye maji nayo inaendelea kuzaa na kutoa juice yake!

Juice yake nilikuwa nzuriii ajabu, mpaka leo nahisi ule utamu wake wenye ladha ya ajabu, lilivyokufa kwa kunyauka baada ya kusafiri na kulisahahu bila kuliwekea maji, nilisikitika sana tena sana, mapaka leo nahangaika kulitafuta bila mafanikio mkuu!

Mwenye nalo au taarifa ya mahali lilipo tafadhali tusaidiane maana nahisi kunyong'onyea kwa urahibu wa kulikosa!
Tangu miaka hii hukuona umuhimu wa kushare hiyo mmea na mtu yoyote ili na wengine pia wafaidike na hata kuendeleza zaidi. Leo usingeleta hii stori hapa.
 
Umenikumbusha mbali sana, huo mmea ulikuwepo nyumbani. Ila tulitahadharishwa tutumie kimiminika chake tu kilichochujwa vizuri na tusijahidi tusile hata kipande kidogo cha nyama ya mkate huo maana tuliambiwa ukivimeza vinaweza kukua katika tumbo la Binadamu.
Ila kwa ushauri tu, jaribu kutembelea hizi Chinese restaurants naamini watakupa pa kuanzia.
Ukifanikiwa usisahau kutupatia mrejesho, maana naamini wahitaji ni wengi ila hawajui pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom