JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Your browser is not able to display this video.
Amesema βEneo linaitwa Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA), marehemu Rais Julius Nyerere alilikabidhi kwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe, lilikuwa likitumika kuwanenepesha ngβombe kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.
βKulikuwa na Meli inaitwa Jitihada iliyotumika kuwasafirisha ngβombe, baadaye mradi huo ulififia na hakukuwa na ngβombe wanaosafirishwa, eneo likabaki tu kwa muda mrefu.
βWatu wengi wameona liko tupu wakanza kuvamia, kuna watu walianza kuuziwa na wengine wakawa wanaambiwa jenga haraka.β
Alipoulizwa kuusu Hati
βKuhusu nyaraka zikiwemo Hati zinafanyiwa kazi kwa sasa.β
"Tulipoona uvamizi unaendelea ndipo tukatoa taarifa, eneo hilo lina ukubwa wa Hekari 6,000, kabla ilikuwa zaidi ya 17,000, likapunguzwa kwa makubaliano ya Zanzibar na hao waliogaiwa.
βSehemu ya eneo hilo pia linaingia shamba la miwa la Bakhresa, kwa sasa Serikali inaangalia na muda mfupi ujao tutajua kitakachofanyika pale.β