Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary ametolea ufafanuzi suala eneo ambalo lipo Bagamoyo Tanzania Bara lakini eneo hilo linamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chanzo: PowerBreakfast (Clouds FM)
Charlse Hillary kawa lini mwanasheria?

Suala kama hili inatakiwa amuite Mwanasheria Mkuu wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ndo wanaweza kuliongelea.

Na wao neno lao bado litakuwa sio la mwisho katika sheria, bali ni Mahakama ya Rufaa ndo inaweza kutoa neno la mwisho kuhusu sheria.
 
Huyu ni mzazibar lazima atetee zanzibar.
Hilary, ambaye pia aliasisi kipindi cha Charanga Time kilichomzidishia umaarufu akiwa Radio One Stereo, alizaliwa Zanzibar miaka 56 iliyopita eneo la Jang’ombe. Aliwahi kunusurika kuuawa kwa risasi mwaka 1964, siku moja baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoundoa utawala wa Sultan na kuiweka Serikali ya Watu wa Zanzibar.
Acheze kwa step na Kauli zake, lile tamko la Mwanzo alibugi.
Au alifanya kwa makusudi akijua kitakachotokea.
 
Huyu ni mzazibar lazima atetee zanzibar.
Hilary, ambaye pia aliasisi kipindi cha Charanga Time kilichomzidishia umaarufu akiwa Radio One Stereo, alizaliwa Zanzibar miaka 56 iliyopita eneo la Jang’ombe. Aliwahi kunusurika kuuawa kwa risasi mwaka 1964, siku moja baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoundoa utawala wa Sultan na kuiweka Serikali ya Watu wa Zanzibar.

Alizaliwa miaka 56 iliyopita halafu akanusurika kifo kwa risasi mwaka 1964!😂 get your facts straight
 
Nyerere alikabidhi kwa makubaliano yapi ( onesheni nyaraka za makabidhiano) hatuwezi kujua labda alimpa kwa muda tu ila siyo kisheria.
 
Angalizo tu; wachangiaji baadhi wajue hilo eneo limetolewa tangu enzi za Mwalimu. Wasije kufikiria ni awamu ya sita. Maana kuna wavivu wa kusoma history ya nchi ila wepesi kujadili history ya nchi wasiyoijua.[emoji120][emoji120][emoji120]
Kuna uthibitisho wa haya unayosema??
 
Back
Top Bottom