Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Yaani naona Hilo eneo watapewa hati yao na DP WORLD wakija, watalitaka ili iwe Bandari kavu, na serikali itabidi ilikodi kutoka Zanzibar kwa bei ambayo itatajwa na SMZ ...wanaupiga mwingi sana...pasi ndefu sana na zote zinamfikia mlengwa .
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hekari 17,000 walikuwa wananenepesha ng'ombe wangapi at a time?

Lifutiwe umiliki kwa kutoendelezwa halafu lipangwe wauziwe wenye uhitaji.
Vipi kuhusu Ambayo wameshajenga tayar umewafikiria?
 
Angalizo tu; wachangiaji baadhi wajue hilo eneo limetolewa tangu enzi za Mwalimu. Wasije kufikiria ni awamu ya sita. Maana kuna wavivu wa kusoma history ya nchi ila wepesi kujadili history ya nchi wasiyoijua

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary amefafanua suala la eneo lililopo Makurunge Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesema “Eneo linaitwa Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA), marehemu Rais Julius Nyerere alilikabidhi kwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe, lilikuwa likitumika kuwanenepesha ng’ombe kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.

“Kulikuwa na Meli inaitwa Jitihada iliyotumika kuwasafirisha ng’ombe, baadaye mradi huo ulififia na hakukuwa na ng’ombe wanaosafirishwa, eneo likabaki tu kwa muda mrefu.

“Watu wengi wameona liko tupu wakanza kuvamia, kuna watu walianza kuuziwa na wengine wakawa wanaambiwa jenga haraka.”

Alipoulizwa kuusu Hati
“Kuhusu nyaraka zikiwemo Hati zinafanyiwa kazi kwa sasa.”

"Tulipoona uvamizi unaendelea ndipo tukatoa taarifa, eneo hilo lina ukubwa wa Hekari 6,000, kabla ilikuwa zaidi ya 17,000, likapunguzwa kwa makubaliano ya Zanzibar na hao waliogaiwa.

“Sehemu ya eneo hilo pia linaingia shamba la miwa la Bakhresa, kwa sasa Serikali inaangalia na muda mfupi ujao tutajua kitakachofanyika pale.”
Chanzo: PowerBreakfast (Clouds FM)
imeenda hiyo, mama kashagawa kama bandari kwa DPW, uliona wapi eneo upewe miaka ya 1960 hati utafute awamu ya sita, 2023 ahsante samia kwa unayowafanyia watangayika, kuna siku wataamka kwa mshindo mkuu, chuki unayoijenga itaongea na vizazi vijavyo
 
Ila kuna haja Sheria ya ardhi ikafanyiwa maboresho.

Haiwezekani Ardhi yote ya Tanzania kuwa ni mali ya Rais kama msimamizi.

Ndiyo maana maRais wetu wamekuwa wakiiuza kadri wapendavyo kwa wageni.

Refer ardhi ya Loliondo na hiyo ya Bagamoyo waliyopewa Wazanzibar kwa utashi wa Rais peke yake 🙌
wagawaji wote ni wanzibari, hakuna rais mtanganyika anayegawa ardhi
 
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary amefafanua suala la eneo lililopo Makurunge Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesema “Eneo linaitwa Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA), marehemu Rais Julius Nyerere alilikabidhi kwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe, lilikuwa likitumika kuwanenepesha ng’ombe kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.

“Kulikuwa na Meli inaitwa Jitihada iliyotumika kuwasafirisha ng’ombe, baadaye mradi huo ulififia na hakukuwa na ng’ombe wanaosafirishwa, eneo likabaki tu kwa muda mrefu.

“Watu wengi wameona liko tupu wakanza kuvamia, kuna watu walianza kuuziwa na wengine wakawa wanaambiwa jenga haraka.”

Alipoulizwa kuusu Hati
“Kuhusu nyaraka zikiwemo Hati zinafanyiwa kazi kwa sasa.”

"Tulipoona uvamizi unaendelea ndipo tukatoa taarifa, eneo hilo lina ukubwa wa Hekari 6,000, kabla ilikuwa zaidi ya 17,000, likapunguzwa kwa makubaliano ya Zanzibar na hao waliogaiwa.

“Sehemu ya eneo hilo pia linaingia shamba la miwa la Bakhresa, kwa sasa Serikali inaangalia na muda mfupi ujao tutajua kitakachofanyika pale.”
Chanzo: PowerBreakfast (Clouds FM)
Waje wakichukue o.w wafunge domo
 
Anawaambia hataki kuongelea hati, anataka story.
Hati ndio zinashughulikiwa saiv, maanake ndio wanakabidhiwa rasmi.
Kila kitu wala urojo wanaendesha na kutuamulia maaana ndio washika Hatamu kwa ssa
Samia
Mwinyi
Makame
Masauni
Hatari sana masikin TANGANYIKA YANGU HAINA MTETEZI WA KWELI
Maaana Watanganyika wenyewe wanataka Madaraka tu na si kuwatetea wenzao hatari sana
 
Hakuna documents za umiliki kwa upande wa Zanzibar zaidi ya maneno kama hayo, kesi ipo mahakamani Watanganyika wameifungua
Unajua sijaelewa nyerere aliwaza nni na muungano huuu mbona kma kuna mambo ya kimchongo sana
 
Huyu ni mzazibar lazima atetee Zanzibar.
Hilary, ambaye pia aliasisi kipindi cha Charanga Time kilichomzidishia umaarufu akiwa Radio One Stereo, alizaliwa Zanzibar miaka 56 iliyopita eneo la Jang’ombe. Aliwahi kunusurika kuuawa kwa risasi mwaka 1964, siku moja baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoundoa utawala wa Sultan na kuiweka Serikali ya Watu wa Zanzibar.
Asante mkuuu kwa darasa huru kidgo
 
Nimeelewa wanachojaribu kufanya hapo ni kuhalalisha Hilo shamba la baresa liwe lake milele, kwamba alipewa ardhi ya Zanzibar nae baresa ni mzanzibar

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Hajafafanua na wala hajatoa maelezo ya kutosha. Kalikimbia swali kwa kusema "kwa sasa tusiongelee hilo". Kuna red flags nyingi sana kwenye hili suala.

Kwa mujibu wa maelezo yake, eneo la RAZABA huko Makurunge lilikua na ukubwa wa hekari 17,000. Mpaka leo hii kasema lina hekari 6,000 tu. Nani anaweza kuachia zaidi ya nusu ya mali yake kirahisi hivyo?

Masoud alipouliza kuhusu vielelezo vya umiliki na kama huenda hayati Mwl. Nyerere alimkabidhi mzee Jumbe eneo hilo walitumie kwa muda tu na sio kulimiliki moja kwa moja, akalikwepa swali.

Dada yangu ni mmoja kati ya wahanga wa eneo hili la Makurunge, inauma sana.
Na hapo wanataka hizo hekari za baresa za miwa zihesabike ni za mzanzibar akiwa kwenye eneo la serikali yake

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary amefafanua suala la eneo lililopo Makurunge Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesema “Eneo linaitwa Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA), marehemu Rais Julius Nyerere alilikabidhi kwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe, lilikuwa likitumika kuwanenepesha ng’ombe kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.

“Kulikuwa na Meli inaitwa Jitihada iliyotumika kuwasafirisha ng’ombe, baadaye mradi huo ulififia na hakukuwa na ng’ombe wanaosafirishwa, eneo likabaki tu kwa muda mrefu.

“Watu wengi wameona liko tupu wakanza kuvamia, kuna watu walianza kuuziwa na wengine wakawa wanaambiwa jenga haraka.”

Alipoulizwa kuusu Hati
“Kuhusu nyaraka zikiwemo Hati zinafanyiwa kazi kwa sasa.”

"Tulipoona uvamizi unaendelea ndipo tukatoa taarifa, eneo hilo lina ukubwa wa Hekari 6,000, kabla ilikuwa zaidi ya 17,000, likapunguzwa kwa makubaliano ya Zanzibar na hao waliogaiwa.

“Sehemu ya eneo hilo pia linaingia shamba la miwa la Bakhresa, kwa sasa Serikali inaangalia na muda mfupi ujao tutajua kitakachofanyika pale.”
Chanzo: PowerBreakfast (Clouds FM)
Kwa nini nyaraka na hati zifanyiwe kazi leo? Mimi nadhani nyaraka zilipaswa kuwekwa hadharani.
 
Na hapo wanataka hizo hekari za baresa za miwa zihesabike ni za mzanzibar akiwa kwenye eneo la serikali yake

Ngoja waendelee kutupiga tu akili si hatuna bwana. Serikali yetu ni takataka.
 
Back
Top Bottom