Charles Hilary afafanua sehemu ya ardhi ya Bagamoyo kumilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Yaani naona Hilo eneo watapewa hati yao na DP WORLD wakija, watalitaka ili iwe Bandari kavu, na serikali itabidi ilikodi kutoka Zanzibar kwa bei ambayo itatajwa na SMZ ...wanaupiga mwingi sana...pasi ndefu sana na zote zinamfikia mlengwa .
 
Reactions: Cyb
Hekari 17,000 walikuwa wananenepesha ng'ombe wangapi at a time?

Lifutiwe umiliki kwa kutoendelezwa halafu lipangwe wauziwe wenye uhitaji.
Vipi kuhusu Ambayo wameshajenga tayar umewafikiria?
 
Huko Zanzibar .....Tanganyika linamiliki nini
 
Angalizo tu; wachangiaji baadhi wajue hilo eneo limetolewa tangu enzi za Mwalimu. Wasije kufikiria ni awamu ya sita. Maana kuna wavivu wa kusoma history ya nchi ila wepesi kujadili history ya nchi wasiyoijua

imeenda hiyo, mama kashagawa kama bandari kwa DPW, uliona wapi eneo upewe miaka ya 1960 hati utafute awamu ya sita, 2023 ahsante samia kwa unayowafanyia watangayika, kuna siku wataamka kwa mshindo mkuu, chuki unayoijenga itaongea na vizazi vijavyo
 
wagawaji wote ni wanzibari, hakuna rais mtanganyika anayegawa ardhi
 
Waje wakichukue o.w wafunge domo
 
"Mimi sio Chalesi.... Mimi ni CHAZ"
 
Anawaambia hataki kuongelea hati, anataka story.
Hati ndio zinashughulikiwa saiv, maanake ndio wanakabidhiwa rasmi.
Kila kitu wala urojo wanaendesha na kutuamulia maaana ndio washika Hatamu kwa ssa
Samia
Mwinyi
Makame
Masauni
Hatari sana masikin TANGANYIKA YANGU HAINA MTETEZI WA KWELI
Maaana Watanganyika wenyewe wanataka Madaraka tu na si kuwatetea wenzao hatari sana
 
Hakuna documents za umiliki kwa upande wa Zanzibar zaidi ya maneno kama hayo, kesi ipo mahakamani Watanganyika wameifungua
Unajua sijaelewa nyerere aliwaza nni na muungano huuu mbona kma kuna mambo ya kimchongo sana
 
Asante mkuuu kwa darasa huru kidgo
 
Nimeelewa wanachojaribu kufanya hapo ni kuhalalisha Hilo shamba la baresa liwe lake milele, kwamba alipewa ardhi ya Zanzibar nae baresa ni mzanzibar

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Na hapo wanataka hizo hekari za baresa za miwa zihesabike ni za mzanzibar akiwa kwenye eneo la serikali yake

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini nyaraka na hati zifanyiwe kazi leo? Mimi nadhani nyaraka zilipaswa kuwekwa hadharani.
 
Na hapo wanataka hizo hekari za baresa za miwa zihesabike ni za mzanzibar akiwa kwenye eneo la serikali yake

Ngoja waendelee kutupiga tu akili si hatuna bwana. Serikali yetu ni takataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…