Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Charles Kimei: One of the most exposed and reputable banking top executives in East & Central Africa. Hakupaswa kujiingiza katika siasa hizi za vyama

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Mambo vp JamiiForums.

Ninapoandika hoja hii, ninaomba ifahamike kuwa i have nothing personal with mzee Kimei na ninatambua kuwa yeye ni moja katika ya hazina kubwa ambazo taifa hili linazo katika masuala mazima ya uchumi na banking.

Watu walikuwa wanapenda sana kumshambulia kaka yangu Pascal Mayalla kuwa amejiingiza katika siasa kwa sababu ya njaa. Sasa huyu CEO mstaafu yeye ana njaa gani? Charles Kimei alipaswa kubaki kama mzee mshauri wa masuala ya uchumi/banking hapa Tanzania/Africa Mashariki na sio kujiingia katika siasa hizi za vyama.

He is one of the most exposed and reputable top executives in banking and finance industry kwa hapa Tanzania na East Africa. Hakupaswa kuonesha mlengo wa wazi wazi wa chama chochote cha kisiasa kiwe upinzani au tawala.

Siasa hizi za vyama angewaachia mzee Dr. Bashiru Ally na Mheshimiwa Mbowe. Kimei angebaki kuwa kama William B. Harrison Jr. CEO mstaafu wa bank kubwa kuliko zote ya Marekani ya JPMorgan Chase ambaye sasa ni mshauri mwandamizi katika umoja wa banks za nchini humo - The American Bankers Association - (ABA)

William B. Harrison Jr.
=====

aaaaaaaaasdfgggggggggg.jpg


Hata kama asingekuwa mbunge wa CCM akaamua kujiunga na CHADEMA, CUF au ACT, kitendo cha kujiingiza katika siasa za vyama kunampotezea intergrity yake aliyotumia nguvu kubwa na miaka mingi sana katika kuijenga kwenye tasnia ya masuala ya uchumi/banking.

Watumishi wa CRDB wenye mlengo tofauti wa kisiasa (upinzani) waliokuwa wanamuona kama role model wao sasa wataanza kuzozana naye hata kama sio face to face hata kupitia mitandao. Alistaafu kwa heshima nzuuuuri mzee wa watu, sasa anajiharibia heshima alipojiingiza kwenye siasa.

Achilia mbali CRDB, wale watumishi wa banks zingine waliokuwa wanamuona kama kioo bora kwa maana aliitoa CRDB kutoka kuwa bank ya kitanzania mpaka kufungua matawi yake nchi jirani, sasa nao atakuwa anajibizana nao kwa sababu za kisiasa. Yeye CCM wao wapinzani. Ipo wapi tena heshima ya mzee Kimei katika industry ya banking?

Kimei kwa levels zake angepaswa awe anaendesha kampuni kubwa sana ya masuala ya ushauri wa kiuchumi/kibank Africa Mashariki na sio kwenda bungeni kurushiana vijembe na wanasiasa ambao wengi ni umri wa watoto wake wa kuzaa, tena anawazidi mpaka exposure.

Kuna mada ilianzishwa humu kuhusiana na kauli yake moja ya kisiasa ( Dkt. Kimei na Spika Ndugai, watoto wenu mliwasomesha ufundi simu? ) ambayo inaonekana imewakera wengi na watu wanamshambulia kweli kweli.

images (2).jpg


Mzee Kimei kwa sasa ni mwanasiasa wa mlengo wa chama tawala (CCM), ina maana watu waliokuwa wanamuheshimu kama CEO bora kwenye banking/uchumi ambao wapo mlengo wa siasa za upinzani sasa wataanza kumtukana na kumrushia maneno ya kejeli jambo ambalo mzee hakuwa na ulazima wa kulifanya.

Wapo watu watahoji mbona kuna professors na PhD holders wapo katika siasa miaka nenda rudi, lakini ni nani kama Kimei katika taaluma ya banking? Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

Wadau woooooote wa tasnia ya banking waliokuwa wanakupenda "unconditionally" sasa umewagawa. Nusu wapo na wewe na nusu nyingine wapo upande ule wa upinzani. Mzee toka kwenye siasa rudi kuwa mshauri katika taaluma yako.
 
1. Charles Kimei kama Mtanzania yeyote ana haki ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote cha siasa, au kutojiunga,ana haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, au kuomba kuchaguliwa.

2. Charles Kimei kwangu mimi hakuwa na integrity yoyote ya maana. Alisema anamuogopa Magufuli sana na atafanya chochote Magufuli atakachosema.

Kauli hii kutoka kwa mtu mume inawekea shaka utu wake na uanaume wake. Kutoka kwa CEO wa Benki, inatilia shaka integrity ya benki hiyo.

Maana ni kama alisema kwamba Magufuli angetaka kuiba hela za CRDB aende kuzitumia kwenye uchaguzi, Kimei angekubali tu.

Hivyo sioni Kimei atapoteza integrity gani, wakati alikuwa hana integrity tangu mwanzo.
 
Kimei amesema watoto wafundishwe zaidi u fundi. Ninakumbuka katika historia ya elimu, kutoa elimu kwa jamii ilikua gharama kubwa, hakukua wana vitabu vya kuchapishwa, elimu watu walikopi kutoka kwa wajuzi kwa kutumia maandishi ya mikono.

Ujuzi ulipasiwa kwa watoto wa matajiri tu. watoto masikini walikua ni tabaka la watawaliwa.

Kadiri siku zilivyokwenda, watawala waligundua kuwa, kuwapa elimu watawaliwa kunaleta faida katika biashara na kupunguza gharama za uendeshaji wa utawala. Watawaliwa wakijua kusoma na kuandika, watarudisha chenji sahihi katika biashara na kuhesabu mali iliyopo ghalani.

Kimei anataka kuwaandaa watoto wa watawaliwa kwa faida ya watawala. Si kuwaendeleza ili nao wawe watawala siku moja.
 
Kimei amesema watoto wafundishwe zaidi u fundi. Ninakumbuka katika historia ya elimu, kutoa elimu kwa jamii ilikua gharama kubwa, hakukua wana vitabu vya kuchapishwa, elimu watu walikopi kutoka kwa wajuzi kwa kutumia maandishi ya mikono.

Ujuzi ulipasiwa kwa watoto wa matajiri tu. watoto masikini walikua ni tabaka la watawaliwa...

 
Mzee Kimei bado unaweza kuwa mzalendo kama mimi pasipo kuwa mwanasiasa.

Wadau woooooote wa tasnia ya banking waliokuwa wanakupenda "unconditionally" sasa umewagawa. Nusu wapo na wewe na nusu nyingine wapo upande ule wa upinzani. Mzee toka kwenye siasa rudi kuwa mshauri katika taaluma yako.
Ktk hierarchy of needs ile ya juuu KBS,ndio anaitafuta.
 
Ni swali tu, na suo vurugu zisizo umiza.

Ni mchaga wa wapi hivi?

Mleta uzi amempamba sana Kimei kuwa ni mbobezi wa mambo ya kibenki Tanzania na Afrika Mashariki nzima; cha kushangaza ni kwamba huyo Kimei hajajitambua na ndio maana akakubali kwenda kudhalilishwa wakati wa kuusaka ubunge na kwenda kwa Sangoma!!!! Unajua kiasi gani cha mikopo chefuchefu Kimei aliiacha alipostaafu CRDB? Unajua kuwa hiyo mikopo chefu chefu aliitoa kwa hao wanaoitwa mafisadi wakina Manji? Je hakufaidika na hiyo mikopo chefu chefu kwa wakina Manji?

Huyo Kimei wenu hakuingia ccm kwa bahati mbaya bali aliingia huko kama njia ya kujikinga na uchafu alioufanya akiwa huko CRDB!!! CCM ni kichaka cha wahalifu.
 
Acheni mawazo ya kidikteta. Kila mtu haki ya kuamua maisha yake. Nyie makamanda uchwara mnajiona mnaweza kuamua Kimei aishi vipi?
 
Back
Top Bottom