Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo Bungeni, Mbunge wa Vunjo ameuliza swali lililoanzia kwenye misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini ambapo Waziri Mwigulu alisema Taasisi za dini zinazofanya shughuli za kiuchumi kwa lengo la kujipatia faida zinatakiwa kusajiliwa na TRA kama wafanyabiashara wengine na kulipa kodi ya mapato kulingana na faida inavyopatikana.
Pia waziri Mwigulu amesema Serikali imekuwa ikipokea maombi ya kusamehe kodi za miaka ya nyuma na ianaendelea kutathmini maombi hayo kuona hatua zinazoweza kuchukuliwa bila kuathiri sheria zilizopo.
Baada ya hapo Kimei aliuliza swali la Nyongeza
Dkt. Charles Kimei: Nampongeza waziri kwa kutoa majibu mazuri yanayotoa faraja sana kwa wanaoendesha shughuli hizo. Serikali itakuwa tayari kurejesha kodi iliyokusanywa kutoka kwenye taasisi hizo kwa shinikizo na hatimaye kuzidhoofisha sana? Pili Serikali iko tayari kuchukua hatua za kinidhamu kwa maofisa wa TRA wanaokiuka sheria?
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba: Serikali ina utaratibu wa kerejesha fedha ambazo zilichukuliwa kwa mujibu wa sheria zinatakiwa kurejeshwa kwa utaratibu ulio wa kawaida wa kufanya refund.
Kwa maeneo ambayo kuna ukiukwaji wa kisheria, taratibu za kisheria huwa zinafuatwa na hatua stahiki za kinidhau kuchukuliwa kwa wale wanaokiuka sheria.