Huyu kibaraka katili toka kwa Mwendazake amepewa madaraka yanayomzidi kimo.
Wala si kibaraka. Mkuu nikwambie jambo. Sheria ya kodi ipo wazi. Wabunge wengi nao hawajui sheria za kodi. Ukionewa unafuata hatua na zipo wazi. Pale TRAB kuna kesi toka za mwaka 2007 mpaka leo hazijaamliwa. Na serikali kupitia serikali haina chochote inaweza kukifanya kesi zikienda Huko. Sheria pia ipo wazi kuhusu Taasisi za Dini na NGO. Zinatakiwa kupewa Kibali na Commissioner, lakini pia hazipewi Msamaha kama watu wanavyozani. Zinapewa punguzo la 25% ya mapato yao yasipigwe kodi.
Mara nyingi ukipewa msamaha wa 25% kwenye mapato unaishia kuwa na Hasara na hivyo haulipi kodi. Ndio maana taasisi za dini hazilipi kodi mara nyingi.
Usipotii Sheria unapigwa kodi kama kawaida.
Pia wana JF niwakumbushe jambo moja muhimu, Sheria ya kodi hata Rais si Rahisi kuiingilia. Anaweza kufanya hivyo halafu anasubiri Bunge lipitishe ndiyo inakuwa sheria.
Nakumbuka Hayati Magufuli alishawahi lalamikia Mahakama za Rufani za kodi kuwa haziamui Kesi Mapema. Na kesi nyingine zimebaki hapo hakuwa na cha Kuwafanya. Na Serikali haiwezi hata shika mali ya mtu kama issue ipo Mahakama za kodi.
Mimi kwasababu nimekuwa Tax Consultant wa miaka mingi, natamani Nchi yangu iwekeze kwenye elimu ya mlipa kodi. Watu hawaelewi sheria ndio maana wanalalamika mno kwa kila jambo hasa Masuala ya Kodi.
Niwaulize, lini umesikia CRDB, NMB, Vodacom, Airtel, Cocacola, Pepsi Co, AZAM, Viwanda vya vingi wanalalamika kuhusu kodi? Hawalalamiki kwasababu wana watu Wazuri/ Wataalamu wa Kodi wanao simamia Makampuni hayo hapo tajwa. Wanakutana na Ukaguzi, lakini baada ya huo ukaguzi wana watu safi wa kusimamia mambo yao ya kodi.
Wana JF mwambieni Mama Kitengo cha Elimu kwa mlipa kodi kimekufa au kipo dhaifu sana ama tuanze fundisha elimu ya Mlipa Kodi Primary Schools au Secondary angalau kwa level ya Utangulizi tu.
Kwa hiyo wamekubali kwa kauli moja kwamba marehemu alikwapua fedha za watu bila kufuata sheria eee!! hii nchi ilikuwa inaelekea kubaya aisee