Mkuu uko sahihi, lakini implementations za hizi skills lazima ziendane na uhalisia. Kwa mfano, mtu anaamua kujiajiri katika sekta isiyo rasmi, kitendo cha kujiajiri ni kigumu sana, na changamoto zake si mchezo (waliojiajiri wanajua). Ninaposema ziendane na uhalisia, namaanisha taasisi zinazohusika (TRA, SIDO, Halmashauri nk) inabidi zilegeze kamba hasa kwa vijana wanaoanza, ziwalee (incubation) na kuwawezesha kwa namna flani ili waweze kusimama. Vijana wakisimama inaongeza wigo wa ajira si kwao to, hata kwa wale ambao wataajiriwa nao.