Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Hiyo ni cream yake hapo KIKWETE hahusiki hata chembe, wateule wake wengi wamepigwa na chini kwa nini asingewatetea hao waliopigwa mwereka??? tafuteni blanketi lakunfunika Magu sio KWIKWETE haingii hapo. Hushangai watu wanakwambia kuwa huyo KITWANGA ni rafiki wa kufa na kupona wa Magu??? tafuta lingine sasa.

Hivi Magu kuwa na urafiki na Kitwanga ni kosa? Na nyie tafuteni marafiki wa kufa na kupona basi.
 
M
Magufuli akitumia style ya China na South Korea Serikali yote itafungwa Jela maana hakuna Msafi wote wana madoa na madhambi Yao , ni vigumu kufuata sheria za China kwani tayari ameonyesha mfano Kwa kumlinda Mwakyembe juu ya Ununuzi wa mabehewa chakavu.

Wale wakurugenzi ndio waliomuingiza chaka pamoja na procurement manager! Nakumbuka tenda ilibidi wapewe wachina ila katikati apo jamaa wakachakachua sijui kwa maelekezo ya nn wakawapa wahindi kwa double price!Magu anajua mchezo mzima na anajua Mwaki hahusiki labda.Ila mpk mwakani mawaziri kadhaa naamini watapumzishwa na watatakiwa kujibu tuhuma zao
 
Magufuli akitumia style ya China na South Korea Serikali yote itafungwa Jela maana hakuna Msafi wote wana madoa na madhambi Yao , ni vigumu kufuata sheria za China kwani tayari ameonyesha mfano Kwa kumlinda Mwakyembe juu ya Ununuzi wa mabehewa chakavu.
sio mwakyembe tu mkuu alituma meseji ya flow meters alibainika na prof muhongo,,kwani kafanywa nini mpaka leo??
 
unajua tukisema ukweli wakati mwingine watu wanaona kama tunapendelea vyama lakini ki msingi nadhani si vyema hoja hizi kuzileta kwa hoja za vyama bali kwa mikakati.

to be honest i was very much disapointed by ooposition last minute move kuacha ajenda zao wakachukua ajenda nyingine ili wapate madaraka.

lakini hilo linatufundisha kuwa uongozi si nyimbo ambazo watu wanaimba kwenye majukwaa bali ni mikakati ya kile wanachotaka kufanya.

hizi ajenda za chama fulani kimeleta hiki na kile kimeleta kile mimi nadhani wapinzani mlizianzisha na kuziua wenyewe wakati wa uchaguzi wa 2015 lakini ni vizuri imewapa wananchi uwanja mpana wa kuchambua siasa.

mbali na kuwa serikali iliyoko madarakani ina mambo kama haya kwangu mimi naona inajitahidi kuliko ambavyo tungepata kiongozi mwingine yeyote iwe kutoka chama chenyewe au upinzani.

sera za raisi alizozianzisha tangu huko nyuma za kutokumuangalia mtu usoni bali anafanya maamuzi kama una haki unapata haki kama umekosea unakosolewa ndio inatusaidia kwa sasa na hakuna mtanzania mwingine aliyeonyesha uthubutu huo.

matatizo yatakuwepo na ndio hayo badala ya kuingiza uchama tuseme hili ni kosa na hili ni sahihi tupate mambo mazuri kutoka serikali hii.

huwezi kunishawishi kuwa kuna watu wengine walitaka kubadilisha mfumo wakati walikuja wamekumbatia "friends[ of president" ambao hawa ndio hufilisi nchi kwa kumdhamini raisi wakati wa kampeni na anapochukua madaraka basi hutaka kulipwa fadhila kama ni kupewa nyadhifa aya, kama ni kulindwa katika biashara ya kutokulipa kodi aya, kama ni kuwatafutia marafiki zao nyadhifa aya. kimsingi serikali inakuwa imetekwa.

hapa tunaweza kuwa na matatizo kwa maana raisi hawezi kuwajua watu wote anaowateua labda ateue marafiki zake tu ambao nao hawezi kuwajua vizuri.

hivyo tumkosoe raisi na serikali yake kwa mantiki ya kutaka wafanye vizuri kwa faida yetu lakini kudhani we had a best option before hiyo ni kuwa kijionyesha kuwa kipofu.

QUOTE="ChescoMatunda, post: 15838934, member: 13157"]Mkuu ni mfumo ambayo ccm wametujengea wengine walipenda tuuondoe mfumo huo lakini wenye mfumo walizidi mbinu najua watanzania wengi hawataki mfumo huo tushirikiane tuondoe ccm na mfumo wake[/QUOTE]
 
Samaki wote wameoza. Kitwanga na Kipilimbi wanaiwakilisha jamii inayonuka rushwa, jamii iliyojaa wazembe, waongo wasiowajibika na kila aina ya uovu. Hakuna msafi; MCC ni ile ile.

JPM ameonesha nia ya kuibadilisha jamii but inahitajika mbinu mpya siyo zile zile za zamani.
 
Kumekuwa na wimbi kubwa ya wazabuni wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakiidai Serikali ya mabilioni hasa wakati wa utawala wa awamu ya nne.

Wengi walikuwa wakiidai Idara ya Polisi, Magereza n.k. Leo hii tunasoma kwenye magazeti kuwa LUGUMI amelipwa billioni37 (mtu mmoja) huku wazabuni wengine wakisotea madai yao miaka nenda rudi hata kufikia hatua ya kufilisiwa.

Mimi najiuliza hivi Serikali ya awamu tuliyoiweka sisi wananchi ilikuwa kwa manufaa ya wananchi?

Haki iko wapi wakati wazabuni wengi wanaidai Wizara ya Mambo ya Ndani lakini mtu mmoja analipwa billioni 37?
 
Sijawahi kuona watu wapole duniani kama Tanzania. Lakini serikali yao ipo katili hatari.
 
Tatizo ni kwenu nyie viherehere, walioona tatizo hilo ni Kamati ya Bunge. Kamati imetoa siku saba kupata maelezo toka kwa wahusika ili watoe maamuzi, viherehere kelele kila siku
 
Naona upo busy kutoa Rushwa ili kupoteza ushahidi wote kisha kesho uje ukanushe kuwa hakuna kilichofannyika kabsa, Watanzania wa Sasa wameamka wanajua mbinu zote mnazotumia kukwepa Majipu yasitumbuliwe .

Hilo ndio tatizo ukishaamua unachojiaminisha ndio hicho hata ukiambiwa ukweli. Mlichoamka nini zaidi mnaendelea kulala tu. Mimi hata siku moja siwezi kushabikia habari ninayoipata bila kuifanyia utafiti. Kosa la kwanza la mwandishi, mkurugenzi wa NIDA sio owner wa Infosyis. Sasa kama watu wanalipwa kudanganya makusudi, hilo hatuwezi kuzuia. Kwa sababu kitu kama hicho kiko wazo BRELLA, sasa kama hakutaka kwenda huko ana lake jambo. Sasa angalia watu wanavyofurahia Ana Kilango kutenguliwa, hiyo ni akili kweli.
 
Mkuu kama unajua vzr funguka usiishie kulaumu tu

Watu hawataki ukweli ndio maana wana hukumu na wameshasema ukweli ndio huu kwahio hata ukweli ukisemwa watasema wamehonga. Siku zote ukweli utajulikana tu sooner or later. Kwa kweli watanzania wengi ni wa kuhurumia, kushabikia vitu wasivyovijua na shida za watu ni furaha yao. Hivi kwa hali ya kawaida utafurahia Ana Kilango kutenguliwa nafasi yake. Mungu awasemehe.
 
Wazabuni wengi nchi nzima wamekuwa wakiidai Wizara ya Mambo ya Ndani mamilioni ya fedha kutokana na huduma waliyoitoa kwa Wizara hiyo. Wengi wa wazabuni wamefuatilia sana malipo yao bila mafanikio na wengi wamefilisiwa. Leo hii tunasoma kuwa LUGUMI alilipwa shillingi billioni thelathini na saba (mtu mmoja) wakati wazabuni wengi wanahangaika kufuatilia malipo yao.Tena tunasoma fedha amelipwa kwa asilimia 99 bila kukamilisha kazi aliyopewa. Mimi najiuliza kweli ni haki mtu mmoja kama LUGUMI kulipwa kiasi hicho cha fedha ilihali wazabuni wengine tena wengi wanakosa malipo yao. Hivi Serikali ya awamu ya nne tuiyoiweka madarakani ilikuwa kwa manufaa ya wananchi?.
 
Niliwahi kuona hapa jamaa anakula bata ndefu sana!! kumbe hera yenyewe hajaifanyia kazi!!
 
Wazabuni wengi nchi nzima wamekuwa wakiidai Wizara ya Mambo ya Ndani mamilioni ya fedha kutokana na huduma waliyoitoa kwa Wizara hiyo. Wengi wa wazabuni wamefuatilia sana malipo yao bila mafanikio na wengi wamefilisiwa. Leo hii tunasoma kuwa LUGUMI alilipwa shillingi billioni thelathini na saba (mtu mmoja) wakati wazabuni wengi wanahangaika kufuatilia malipo yao.Tena tunasoma fedha amelipwa kwa asilimia 99 bila kukamilisha kazi aliyopewa. Mimi najiuliza kweli ni haki mtu mmoja kama LUGUMI kulipwa kiasi hicho cha fedha ilihali wazabuni wengine tena wengi wanakosa malipo yao. Hivi Serikali ya awamu ya nne tuiyoiweka madarakani ilikuwa kwa manufaa ya wananchi?.
Nani alikwambia kuna haki nchi/nji hii mkui
 
Watu hawataki ukweli ndio maana wana hukumu na wameshasema ukweli ndio huu kwahio hata ukweli ukisemwa watasema wamehonga. Siku zote ukweli utajulikana tu sooner or later. Kwa kweli watanzania wengi ni wa kuhurumia, kushabikia vitu wasivyovijua na shida za watu ni furaha yao. Hivi kwa hali ya kawaida utafurahia Ana Kilango kutenguliwa nafasi yake. Mungu awasemehe.
Ukikuta watu wanashangilia Uongo ..manake hajatokea mkweli. ..akauweka Hadharani....cha muhimu...unaejua ukweli ukisema unakuwa umetimiza Wajibu wako kazi kwao
 
Wazabuni wengi nchi nzima wamekuwa wakiidai Wizara ya Mambo ya Ndani mamilioni ya fedha kutokana na huduma waliyoitoa kwa Wizara hiyo. Wengi wa wazabuni wamefuatilia sana malipo yao bila mafanikio na wengi wamefilisiwa. Leo hii tunasoma kuwa LUGUMI alilipwa shillingi billioni thelathini na saba (mtu mmoja) wakati wazabuni wengi wanahangaika kufuatilia malipo yao.Tena tunasoma fedha amelipwa kwa asilimia 99 bila kukamilisha kazi aliyopewa. Mimi najiuliza kweli ni haki mtu mmoja kama LUGUMI kulipwa kiasi hicho cha fedha ilihali wazabuni wengine tena wengi wanakosa malipo yao. Hivi Serikali ya awamu ya nne tuiyoiweka madarakani ilikuwa kwa manufaa ya wananchi?.
Nani alisema amelipwa asilimia 99 acheni uongo subirini report ya CAG.
 
10% ya nguvu hapo watu wamekula. Wenye tenda za milioni 5 hawana chao.
 
Wazabuni wengi nchi nzima wamekuwa wakiidai Wizara ya Mambo ya Ndani mamilioni ya fedha kutokana na huduma waliyoitoa kwa Wizara hiyo. Wengi wa wazabuni wamefuatilia sana malipo yao bila mafanikio na wengi wamefilisiwa. Leo hii tunasoma kuwa LUGUMI alilipwa shillingi billioni thelathini na saba (mtu mmoja) wakati wazabuni wengi wanahangaika kufuatilia malipo yao.Tena tunasoma fedha amelipwa kwa asilimia 99 bila kukamilisha kazi aliyopewa. Mimi najiuliza kweli ni haki mtu mmoja kama LUGUMI kulipwa kiasi hicho cha fedha ilihali wazabuni wengine tena wengi wanakosa malipo yao. Hivi Serikali ya awamu ya nne tuiyoiweka madarakani ilikuwa kwa manufaa ya wananchi?.
Hapo waliokula hizo ni punda? Si ni wanachi?
 
Yetu macho na masikio. Kumpata mtu safi kwenye system ya Ccm ni sawa na kutaka mwanamume abebe ujauzito.
Kuna mtu mmoja alisema kupata mtu msafi ndani ya ccm ni sawa na kumtafuta mwanamke bikra wodi ya wazazi, du hii hii balaa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom