Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Kama Bunge lisipokubali kupiga vigelegele na likafuatilia, hakuna mtu atapona.
Kazi ya Bunge ni kuishauri na KUISIMAMIA serikali. Likitimiza wajibu hizo mbili nchi itarudi kwenye mstari
Siyo kwa bunge la Job Ndugai angalia hata kwenye uchaguzi wa kamati za PAC na LAART, ambazo kimsingi ni za kuisimamia serikali alivyozichakachua,
 
Kwanini walipwe pesa yote wakati hata nusu ya kazi haijafanyika.Sasa naona ngoma imefikia patamu. Tusisahau tembo wawili wanapopigana .....
 
Wengine tuhuma tu mtu wanatumbuliwa... ila waziri akiwa na tuhuma haguswi.....kina january makamba na mu italiano wake nayo ishapotea.... #ndosiasazabongo
 
Hoja dhaifu, dini yao inaingiaje hapa? Na nani ameachwa au kutumbuliwa kwa sababu ya dini yake?
Hao hawawezi kuhuswa
1 kwa dini yao
2 kwa uwezo wao
3 kiburi chao
4 mvinyo ndio ule ule
 
Unafiki sio tusi ni sifa ya mtu mwny kupenda kujifanya anazungum ziada upande mmoja. Kwa hiyo ukiwa unazungumzia jambo kinafiki nafki hatutaepuka kukukanya. Kukumbusha kuwa Mbowe kasema Rushwa ndani ya Chadema na ukosefu wa nidhamu viliwakosesha ushindi iweje uwe mkali?
Kutokufikishwa Mahakamani sio kigezo kuwa ni wasafi.

Unafiki ni kuamini Misikitini,Makanisani,Saccos na Vyama vya Upinzani hakuna Rushwa kwa kuwa tu hawajafikishwa Mahakamani
Kwa hiyo wale tuliowapa mamlaka ya kukusanya kodi na kuzitumia ili kutuletea maendeleo wanapoacha jukumu hilo na wanaishia kuziiba na kufisidi, wewe na upofu wako wa akili na mapenzi yako ya kijuha ya CCM unataka tusijadili, tusishutumu, kwa kufananisha hawa wenye dhamana wanaotuibia mabilioni kama siyo matrilioni ya shilingi na kufananisha na petty thieves wa misikitini, makanisani na Saccos na vyama vya upinzani? You are nut, keep it in your mind you are nut
 
Kweli wingi wa division 0 n 4 si kwasababu walimu kwasababu mmeamua kuzipata kwa kupindisha mafundisho ya walimu wenu.

Tuhuma zimevumisha hata mwezi bado, ushahidi hata haujapatikana, mmejaa mapovu kumlaumu Magufuli na kuanza kutoa mahitumisho,

Jamani, kuweni na hata kumbukumbu ya yale mliyo elekezwa. ' no evidence no right to speak'.
Ushahidi wa January Makamba na dada yake Mwamvita kwenye utapeli wa yule mtaliano nao haukupatikana au haujapatikana? Usiwafanye watu wote wajinga kama umeamua kuwa mjinga wewe, niambie kuna mwanasiasa gani katumbuliwa? Kungekuwa kuna wenye akili na nidhamu mtu mwenye tuhuma kama Chenge angepewa uenyekiti wa bunge?
 
Sidhani kama hii ni cream yake halisi aliyokuwa anaitaka ndiyo maana kabla ya kuitangaza nakumbuka Mwenyekiti alimuita wakampa mikakati ya chama kama kisingizio kuwa chama kinataka hivi otherwise kama nae ni mmojawapo basi ajitumbue tu

Hiyo ni cream yake hapo KIKWETE hahusiki hata chembe, wateule wake wengi wamepigwa na chini kwa nini asingewatetea hao waliopigwa mwereka??? tafuteni blanketi lakunfunika Magu sio KWIKWETE haingii hapo. Hushangai watu wanakwambia kuwa huyo KITWANGA ni rafiki wa kufa na kupona wa Magu??? tafuta lingine sasa.
 
Magufuli huwa ni mbishi linapokuja suala la kuwafanyia vetting watu anaowateua. Huwa hakubali kabisa wateule wake wafanyiwe vetting.
 
Anaitwa Charles,tunachambua bila kujali ni wa imani yetu.mguse Dau sasa weeee(in Joti's voice)

Dau hakumpa tenda rafiki yake au kushrikiana na kampuni yake (kama anayo) na kupiga dili za mabilion, hakuna ushahidi wa waziwazi kama huu na kama upo kama huu au kuzidi huu basi ulete. Madude mengi yanatumia rafiki zao na ndugu zao kusimamia kampuni zao na wao kuwa viungo wakuu wa kuwapa tenda na mapesa mengine yaserikali, mfano mdogo tu ni huo wa huyo jamaa KITWANGA. ni tofauti na Dau, zinaletwa shutma hazina uthibitisho wa mabest friend kushirikiana nae kupiga pesa au kampuni zake kuhusika.
 
Hapa Ni shida maana akuna political will to do so, David Kameroni sasa yuko ktk shida kama wa Iceland amejiuzuru naye pia atajuzuru kwa sababu amebenefit kutoka kwa baba yake na fedha alizoyumia kifanyia kampein.
 
[QUOTE="OKW BOBAN SUNZU, post: 15834322, member: 52569naitwa Charles,tunachambua bila kujali ni wa imani yetu.mguse Dau sasa weeee(in Joti's voice)[/QUOTE]
Wale majuha wasingeweza kuchangia kama zile tuhuma za Dau, wanaingiza udini inaonyesha dhahiri upofu wa akili zao
 
[QUOTE="valour, post: 15835843, member: 25013"nimesoma comments za watu wengi humu ndani nimegundua wana conclude na kuhukumu kabla hata ya kupata upande wa pili wa habari. Watanzania sasa hivi tumekuwa watu wa ajabu tunapenda na kufurahia watu wakipata shida, wakifukuzwa kazi, wakipelekwa mahakamani na kupata mateso. Sijui hata tunaelekea wapi. Sina uhakika na ukweli wa habari hii ila ninachojua Mkurugenzi wa Nida sio owner wa Infosys. Nimeshangaa kama mwandishi wa habari ameshindwa kufanya research kidogo tu na kujua nani owner wa Infosys, kwanini niendelee kuamini habari yote. Ukweli utajulikana tu. Lakini watanzania tuache ushabiki hasa kama hatujapata taarifa kutoka pande zote mbili.[/QUOTE]
Si kweli kuwa kamati ya bunge ndiyo iliyoibua haya?
 
Hiyo ni cream yake hapo KIKWETE hahusiki hata chembe, wateule wake wengi wamepigwa na chini kwa nini asingewatetea hao waliopigwa mwereka??? tafuteni blanketi lakunfunika Magu sio KWIKWETE haingii hapo. Hushangai watu wanakwambia kuwa huyo KITWANGA ni rafiki wa kufa na kupona wa Magu??? tafuta lingine sasa.
Simtetei magu wala JK, tena nataka wapasuane haswa. Hawa ndiyo waliotufikisha hapa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom