Charles Magari tokea kuondoka Tanzania, sanaa basi

Nimekumbuka kwny movie ya Kanumba ile ya young billionaire"kwa sauti ya mkwaruzo akimnanga ,aunt Ezekiel "hii takataka ya kutupa dampo" anavoitamka hiyo takataka , tulikua tunacheka sana home,na kutaniana
 
Jamaa kwakweli alituburudisha sana. Tunamshukuru aliutendea haki muda wake.
 
Kati ya vitu vilinishinda kutazama ni hizo kitu zinaaitwa bongo movie...

Mara ya mwisho kuwa mfuatiliaji wa hizo vitu (wakati huo tukiita tu maigizo) ni wakati wa Mambo Hayo na Kaole (enzi zile za Nyamayao, Muhogo...), Kaole walinifurahisha kwa kuwa scripts zao zilizingatia mno ufasaha wa lugha ya Kiswahili...kina Mwita Maranya na Onyango...
 

Halafu ukute unakomaa na sci fi za wambele.

Jamani tuwasaidie hawa wasanii wetu kwa kusaport vya kwao ili wazidi kutuletea vulivyo bora.

Kanumba aliwahi kusema,hata ray tatizo la yote haya ni bajeti,huwezi tengewa na mfadhili 5mln utoe kitu kinachoeleweka,lazima upruni kuendana na hela iliyopo.mfadhili pia haelewi maana hana uhakika kama mauzo yatavuka 15ml,achukue taje 7 faida na 8 awaache mgawane[emoji16][emoji16]

Bajeti ya animation kama rango tu ni pesa za kibongo bilion 400 na zaidi,imagine kutoka milion 5 mpaka bilioni 400 utakuwa umenuna mara ngapi mpaka uje ufurahi[emoji1787][emoji1787]
 

Mkuu bajeti ina sehemu yake lakini si kitu pekee kinachoifanya filamu iwe bora...

Binafsi kitu ninachotazama sana ni uhalisia wa kile kitu watu wanaigiza, mpangilio wa script, mbinu za uigizaji n.k...

Mathalani, ukitazama filamu zetu namna watu wanavyoongea, huwa wanakuwa na pozi fulani hivi la kuongea kama robots ambapo katika maisha ya kawaida huwa hatuongei taratibu vile na kwa minyato...

Filamu huwa zinajaa makelele ya background music, urefushwaji wa frame (mfano mtu anaweza akatoka Kiluvya hadi Posta, akaoneshwa anapanda daladala, anadaiwa nauli hadi anafika Posta, anashuka, anaanza kutafuta jengo analoenda....hapo kati ni ala ya muziki tu inapigwa)...

Mtu ambaye nimeona anaweza akaleta mapinduzi kwenye filamu Tanzania ni Idris, kuna wakati kupitia Youtube alikuwa anaweka short films kwenye channel ya Lokomotion kama Danga na Ndomu, naamini bajeti yake si kubwa lakini matokeo yake yana uelekeo wa kuwa bora...
 
Wewe ni muongo. Pauni 5000 kwa mwezi haiwezekani labda paundi za Sudan.
 
Nimekumbuka kwny movie ya Kanumba ile ya young billionaire"kwa sauti ya mkwaruzo akimnanga ,aunt Ezekiel "hii takataka ya kutupa dampo" anavoitamka hiyo takataka , tulikua tunacheka sana home,na kutaniana
Mkiwa na beki tatu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…