Charles Odero, afungua kesi Katika Mahakama Kuu kupinga tozo za Miamala ya Simu

Charles Odero, afungua kesi Katika Mahakama Kuu kupinga tozo za Miamala ya Simu

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
51,303
Reaction score
40,190
Wanaukumbi.

Mwanaharakati wa Masuala ya Haki za Binadamu, Charles Odero, amefungua kesi Katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam dhidi ya Waziri wa Fedha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga tozo za Miamala ya Simu iliyoanza Julai Mosi. Kesi hiyo itaanza Alhamisi,Agosti 12.

Hawa ndiyo wanaharakati wanaotakiwa wapo kwa ajilii ya maslahi ya taifa.

Alaa Salah, shangazi mwenye umri ya miaka 22 aliongoza wananchi Sudan kusimamia Haki;
Alaa Salah, alikuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa kidikteta wa Omar Al-Bashir hadi ulipoanguka. Tanzania tunanogeshana kwa Space huku wamekaa kwenye sofa majumbani wanakunywa wisk tu karanga.


IMG_20210808_215345.jpg
 
Ritz kwa mara ya kwanza umeongea jambo la mbolea! Nakubaliana na wewe uharakati ni vitendo na sio uharakati wa mitandaoni,nampongeza sana charles kwa hatua aliyochukua, ajaishia tu kulalamika tozo toz mitandaoni bali ameenda next step ya kisheria ,wapo baadhi ya wanaharakati wamepinga vitu kwa vitendo kuhusu mambo mabli mbali.

Tozo inaumiza sana hasa kwa sisi tunaotuma na kupokea miamala,kazi zetu zinafanyika maporini hivyo transactions nyingi tunatumia simu,tunakatwa sana tozo zinaumiza ,ukituma 50k basi andaa 4100 ya serikali ya nyongeza ukiachana na za awali za makato.
 
Hata mimi naweza kuwa shahidi wake kwenye hili kesi na haya ndiyo mambo ya msingi kuipigia kelele.
Hahahaah CCM mnatengeneza tatizo then mnataka kupata fursa kwenye hilo tatizo! Wabunge wote 300+ wa CCM walipitisha huu upotolo, then mnataka watu watumie mitandao kukataa tozo! Basi tuvunje bunge tuwe na mijadala tu kwenye mitandao.
 
Safi sana, akomae asikate tamaa

Pia awe makini wasije kumpoteza

Move on Odero.
 
Back
Top Bottom