ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Sawa, sikatai. ila na mimi nauliza, nisiulize sasa?!

Kipindi cha Kuanzia Miaka 2500 kabla ya kutolewa unabii hadi siku ya kutolewa unabii, maarifa yaliongezeka au yalipungua?
 
Sawa, sikatai. ila na mimi nauliza, nisiulize sasa?!

Kipindi cha Kuanzia Miaka 2500 kabla ya kutolewa unabii hadi siku ya kutolewa unabii, maarifa yaliongezeka au yalipungua?
Yaliongezeka lakini watu hawakuenda mbio. Hivyo hoja yako haikanushi unabii huo
 
Vip kuhusu waliogundua umeme? Vipi kuhusu waliogundua engine? ChatGpt naona kama hata sio uvumbuzi mpya bali mwendelezo tu wa tekonolia ya computer
 
Yaliongezeka lakini watu hawakuenda mbio. Hivyo hoja yako haikanushi unabii huo
Sasa kama yalikuwa yanaongezeka kipindi hicho maana yake nusu ya utabiri huo tayari sio utabiri. Haya tuendeleee..

Kipindi utabiri unatolewa, watu walikuwa wanakimbia mbio kwa speed ipi, na hivi leo watu wanaenda mbio kwa speed ipi? (In km/hr)..?
 
Vip kuhusu waliogundua umeme? Vipi kuhusu waliogundua engine? ChatGpt naona kama hata sio uvumbuzi mpya bali mwendelezo tu wa tekonolia ya computer
Nimeishasema, nimeitaja chatGPT kwa kuwa ni habari ya mjini kwa sasa. Lakini chatGPT ni sehemu tu ya ongezeko kubwa la maarifa katika nyanja mbalimbali. Hivyo kugunduliwa kwa umeme na engine, yote hayo bado yanatimiza huo unabii maana hayakuwepo hayo wakati unabii unatolewa.
 
Sasa kama yalikuwa yanaongezeka kipindi hicho maana yake nusu ya utabiri huo tayari sio utabiri. Haya tuendeleee..

Kipindi utabiri unatolewa, watu walikuwa wanakimbia mbio kwa speed ipi, na hivi leo watu wanaenda mbio kwa speed ipi? (In km/hr)..?
Usiwe mvivu. Muulize chatGPT atakuambia Speed ya farasi(usafiri wa mbio wa wakati ule na ndege/airplane usafiri wa mbio wa sasa)
 
Sasa kama yalikuwa yanaongezeka kipindi hicho maana yake nusu ya utabiri huo tayari sio utabiri.
Ngoja nikupe elimu zaidi. Kuongezeka kwa maarifa ni sehemu tu ya ishara na dalili nyingi zilizotabiriwa kuwa zitatokea kabla ya kurudi kwa Yesu na mwisho wa dunia. Soma dalili nyingine zilizotimia katika Mathayo 24.

Sasa Maandiko yanasema: Mt 24:33 SUV "nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni."
 
Kijana kwako chatgpt ndio umeona ndio kiwango cha juu sana cha maendeleo?
 
Haya yalianza jadiliwa kabla kristo, kila jambo jipya duniani binadamu hutahayari na kuona sasa maandiko yatatimia, siku yatakapo timia ndipo mtakumbuka maandiko, ila sio mkumbuke maandiko ndio itimie
 
Yani umri huu bado unaamini kwenye hekaya za watu WA jangwani😂😂😂
 
Nipe habari ww unayeijua mbinguni
Soma Biblia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Kwa ufupi, mbinguni hakuna kuugua, hakuna kulia, hakuna njaa, siku 1000 ni sawa na siku moja, hakuna giza, hakuna vita, hakuna kifo nk nk nk nk nk nk
 
Hakuna lolote Ka maana kikawaida ni kwamba kila technology mpya inapo gundulika huwa ni kama Miujiza lakini yote watu tulikuwa hatufahamu Hicho kitu
 
Hakuna lolote
Sawa. Hata wakati wa Nuhu watu waliambiwa gharika itakuja wakapuuza. Mimi nimeishatoa onyo huu ni wakati wa mwisho
Mit 29:1-14 SUV
Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.
 
Haya mambo ya siku za mwisho ni hadithi za kutungwa na wahuni fulani
 
Sio lazima iwe hivyo. Tangu ulipoanza kula chumvi imepita miaka mingapi. Kuna chumvi mpya umeiona
Hili swali ni sawa na kuniuliza kama nimeona aina mpya ya maji tofauti na yaliyopo.

Ila kwa umro nilionao nmeyaona mabadiliko mengi ya kiteknolojia na hata hapa tulipo sio mwisho wa ujio wa teknolojia mpya.

Sawa na watu walioishi kipindi ambacho hapakuwa na radio, ujio wa radio ilionekana kama jambo la kistaajabisha sana, iweje mtu aongee kwenye vipande vya nyaya na vibatii?, ndio sawa na sisi tunavyoiwaza AI na utendaji kazi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…