ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Mkuu wapi watu wameanza kukimbia huku na huko
Hahaa, mkuu, kwanza umejijibu - watu wanakimbia vita. Ni sawa. Vita vipo sehemu nyingi duniani wakati huu. Na hilo la vita lilitabiriwa pia. Pili, kwa kuwa maarifa yameongezeka, watu siku hizi "wanakimbia" huku na huko kwa pikipiki, magari na ndege 🙂
 
Hahaa, mkuu, kwanza umejijibu - watu wanakimbia vita. Ni sawa. Vita vipo sehemu nyingi duniani wakati huu. Pili, kwa kuwa maarifa yameongezeka, watu siku hizi "wanakimbia" huku na huko kwa pikipiki, magari na ndege 🙂
Hivi wewe unavijua vita au hizo biblia mnazisoma Mmezigeuza juu chini?

Kafatilie vita vya wa Amaleki, Wafilist, Wamoabu, vita ya Jeshi la Nebdkadineza dhidi ya Waisraeli, Washami na wasamaria, watu walikufa kwa idadi kubwa kwa siku haijawahi kutokea ktk modern world.

Nitakupa mfano.

Vita walivyopigana Waisrael dhidi ya wabenjamini walikuwa wanachinja na kuua wapiganaji, watoto na wanawake kwa siku elfu 70 hadi elfu 80.

Soma: Waamuzi, utaona baada ya Wabenjamini wa Yerusalem kumbaka yule Mwanamke wa Msafiri walichofanywa.

Kama ni mwisho wa dunia ungeanzia hapo

Vita ya Gaza israel inayoendelea hadi leo vifo hata elfu 50 havifiki kwa miaka miwili.
 
Chatgpt asipo dhibitiwa ataleta shida Jana nimechati nae.kama mwana kabisa ...haifai kabisa...Ina Mambo mengi ambayo akili ilitakiwa kuchakata Ila yeyewe inalipa majibu fasta na kwa usahihi mzuri
 
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."

Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.

Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!

Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).

Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI
View attachment 3235549 View attachment 3235550View attachment 3235551View attachment 3235552View attachment 3235553
Kutabiri kwamba maarifa yataongezeka siku zijazo ni sawa na kutabiri kuwa jua litaonekana kuchomoza kesho.

Very banal and unimpressive.
 
Kama ni mwisho wa dunia ungeanzia hapo
Kuongezeka kwa maarifa ni moja tu kati ya dalili nyingi za kuja kwa Yesu na mwisho wa dunia. Soma Marko 13, kisha soma 2 Timotheo 3:1-9 utaona dalili nyingine.
 
Kutabiri kwamba maarifa yataongezeka siku zijazo ni sawa na kutabiri kuwa jua litaonekana kuchomoza kesho.

Very banal and unimpressive.
Mkuu, try to imagine, ungekuwa uko hai miaka 2500 iliyopita, kisha ukafa, halafu ukafufuka leo na kuona maarifa yalivyoongezeka, usingesema ni unimpressive.

What makes Daniel 12:4 compelling is the scale and velocity of today’s transformation. For centuries, knowledge crept forward—it took 1,900 years, for example, to go from oil lamps to electric light. But in mere decades, we’ve seen the internet, computing, and AI like ChatGPT radically democratize access to information for billions at near-light speed. This isn’t just 'increase'—it’s a global deluge made possible only by once-unimaginable technology. Thus, it could mirror the 'time of the end' prophecy: not mere change, but a historical inflection point.
 
Huyo ChatGPT mwenyewe hajazoeleka bado na tayari ameshapata wapinzani wake kina Deepsek na wengine wengi. Je, huoni baada ya miaka 5 hadi 10 ijayo patakuwa na maarifa tofauti na bora zaidi ya hizi akili mnemba? Huu ni mwanzo tu, maarifa kamili ni kwa karne zijazo mtumishi wa Mungu.
Kabisa aisee...bado kuna mengi yatakuja ya kushangaza..
 
Unateseka Ukiwa Wapi Ndugu?
Ila masuala ya kuamini vitabu vilivyo kuja na mitumbwi ni kazi Sana.

.hapo muislamu hajaja na maandiko yake.
.Muhindu nae
. Watu wa Buddha nao.

ila sisi afrika Ina tutesa Sana, tume ikomalia mnooo.
wakati roho mbaya, chuki, mauaji, wizi, ndio sera zetu.
Ekaeka
 
ChatGpt Inahusikaje Hapo Hapo Ungeweza pia Kusema Ujio Wa Gari Umetimiza utabiri uliotabiriwa miaka 2500 ilopita
 
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."

Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.

Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!

Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).

Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI
View attachment 3235549 View attachment 3235550View attachment 3235551View attachment 3235552View attachment 3235553
Nikuulize huo wimbo umeimba wewe na vyombo umepigiwa kupitia simu au....
 
Mkuu, try to imagine, ungekuwa uko hai miaka 2500 iliyopita, kisha ukafa, halafu ukafufuka leo na kuona maarifa yalivyoongezeka, usingesema ni unimpressive.

What makes Daniel 12:4 compelling is the scale and velocity of today’s transformation. For centuries, knowledge crept forward—it took 1,900 years, for example, to go from oil lamps to electric light. But in mere decades, we’ve seen the internet, computing, and AI like ChatGPT radically democratize access to information for billions at near-light speed. This isn’t just 'increase'—it’s a global deluge made possible only by once-unimaginable technology. Thus, it could mirror the 'time of the end' prophecy: not mere change, but a historical inflection point.
Nakwambia hivii, hata leo naweza kutabiri kirahisi tu kwamba dunia ikiendelea kuwepo kwa miaka 2500 ijayo, maarifa yataongezeka sana.

Kama ninavyoweza kutabiri kuwa jua litaonekana kuchomoza kesho.

That is banal and unimpressive.
 
Katika kipindi chote cha tangu kuanza binadamu kujifshamu, ni lini maarifa yaliwahi kupungua? Kwamba sasa tuone kuongezeka ni unabii
 
Hakuna lolote. We waishangaa chatgpt kwa sababu mengine umeyakuta. Wewe wadhan watu wa zama za miaka ya 60 walioanaje uvumbuzi wa computer?

Mara ya kwanza kujua uwepo wa Google, nilikuwa nashangaa nasearch kitu inaniletea majibu niliona ni kitu kimoja amazing sana.

So chagpt ni uvumbuzi tu wa kawaida sema ni exciting kwa sababu ni uvumbuzi mpya.
Hashangai ndege iligunduliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, anashangas AI
 
Nakwambia hivii, hata leo naweza kutabiri kirahisi tu kwamba dunia ikiendelea kuwepo kwa miaka 2500 ijayo, maarifa yataongezeka sana.

Kama ninavyoweza kutabiri kuwa jua litaonekana kuchomoza kesho.

That is banal and unimpressive.
If something seems unimpressive to one person, that doesn't mean everyone sees it the same way. Personally, I find the increase in knowledge, especially AI, to be very impressive. And regardless of whether Daniel’s prophecy is seen as banal or unimpressive, it has been fulfilled. Period
 
Back
Top Bottom