Chato: Kijiji kilichokaribia kuwa makao makuu ya mkoa-2

Katika mfululizo wa mapitio ya kitabu, 'I am the State: A President's Whisper from Chato' (Mimi ni Dola: Mnong'ono wa Rais kutoka Chato) leo tunaangazia sura yake ya pili inayozungumzia Chato kama kijiji ambacho kilikaribia kuwa makao makuu ya mkoa.

Kitabu kinaanza kwa kuelezea kulivyokuwa na mdororo wa uchumi nchini kote, uliosababishwa na mazingira mabaya ya biashara kati ya 2015 na 2020. Kwa miaka mitatu mfululizo (2016-2018), karibu biashara 4,640 zilifungwa kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya biashara yanayotokana na sera mbaya, uwezo mdogo wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wadogo na wa kati na ukosefu wa motisha.

Kelele za kupungua na hatimaye kufungwa kwa biashara kote nchini zilitolewa mara kadhaa na wabunge, ingawa Serikali haikuwahi kukiri jambo hilo.

Waandishi wa kitabu hicho miongoni mwa vyanzo walivyotumia, kimojawapo kimesema fedha kwenye mzunguko zilipungua kutoka asilimia 22 mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka 2018 na kwamba kati ya 2011 na 2017 ukuaji wa Pato la Taifa (GNP) ulikuwa wa asilimia 7.8 lakini kufikia 2018 ulikuwa chini hadi asilimia 6.8.

Kutokana na hali kuwa mbaya, kati ya mwaka 2015 na 2020, Benki Kuu (BoT) ilichukua hatua kadhaa ama kusimamisha, kuunganisha au kufunga baadhi ya benki, zikiwamo Benki ya Wanawake Tanzania, Twiga BanCorp, Ecobank, Efatha Bank, Covenant Bank, Kagera Farmers' Cooperative Bank, Meru Community Bank na Njombe Community Bank.

Waandishi wa kitabu hicho wanasema ingawa ni sahihi kwa BoT kuchukua hatua kali dhidi ya mabenki katika hali ya ufilisi, ni kweli vilevile kwamba hali ya uchumi wa Taifa ina athari kubwa kwa hali ya taasisi hizo za kifedha.
Waandishi hao waligundua kuwa karibu benki zote zilizoathirika zilikuwa za binafsi, isipokuwa Twiga Bancorp, ambayo hatimaye iliunganishwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) pamoja na Benki ya Wanawake na kuunda Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Kwa hiyo, kadiri biashara zilivyokuwa zikipungua siku baada ya siku tangu 2016, hatima ya sekta kibinafsi ilikuwa katika hali mbaya zaidi. Serikali iliamua kuunda "Kikosi Kazi" kukusanya kodi kwa niaba ya taasisi yenye mamlaka hayo kisheria, TRA.
Katika mchakato huo, biashara nyingi zilikumbana na hali ngumu zaidi. Akaunti nyingi za biashara zilizuiwa na mabilioni ya pesa kuchukuliwa. Katika baadhi ya matukio, kwa sababu zinazojulikana zaidi na Serikali, wamiliki wa biashara walishtakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi.

Kuhusu Chato
Baada ya kueleza kinaganaga hali ya biashara ilivyokuwa na masaibu yaliyowakumba wafanyabiashara wengi, waandishi wa ‘I am the State’ wakaigeukia Chato.
Wanasema wakati biashara zikiporomoka katika maeneo mengi ya nchi kati ya 2016 na 2020 kutokana na mazingira yaliyotajwa hapo juu, kipindi hicho kilikuwa cha neema kwa Chato.
Ulianzishwa uwekezaji wa kimkakati katika wilaya ambayo haikujulikana kwa jumuiya yoyote kubwa ya wafanyabiashara, kinaandika kitabu hicho.
Biashara za Chato hazikuendeshwa na soko, wanasema, lakini zilisukumwa kisiasa na Rais ambaye alikuwa amejitokeza kukaidi sayansi ya biashara katika azma yake ya kubadili na kuendeleza mji wake wa Chato.
Na hivyo ndivyo Benki ya CRDB ilivyojikuta kwenye mtanziko ilipoamriwa kufungua tawi Chato lililofunguliwa Machi 9, 2018.
Kitabu kinamnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akisema benki hiyo ilikuwa imekataa kufungua tawi hilo Chato kwa sababu upembuzi yakinifu umeonyesha hakuna uwezekano wa kufanya biashara, lakini kuanzishwa kwa tawi hilo kulitokana na “utafiti uliofanywa na Rais mwenyewe.”

Ilionekana wazi kuwa pamoja na kwamba CRDB inaongoza kwenye orodha ya benki kubwa nchini kama NMB, NBC, Stanbic, Standard Chartered, Absa, DTB, Exim, Azania na Citi Bank, haikuwa na nia ya kunyakua fursa hii ya kuwepo Chato hadi ilipolazimishwa na mkuu wa nchi.

Watafiti wa kitabu hicho walizunguka Chato kuangalia huduma mbalimbali katika hoteli, baa, migahawa na nyumba za wageni. Uchunguzi wao ukabaini kuwa nyumba nyingi za kulala wageni zimeamua kushusha gharama za huduma kutokana na kupungua kwa wateja.

Wakati wa utafiti wao walitembelea hoteli kubwa Chato kwa kulinganisha. Katika matokeo ya utafiti wanabainisha kuwa biashara zilikuwa zimedorora.
Mathalan, wanazungumzia pia maeneo ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Chato ilipima na kuuza takriban viwanja 2,000.
Kati ya hivyo, viwanja 1,500 vilipata wateja ingawa wengi kwa mkopo. Mradi huo ulivutia wanunuzi kutoka Chato na kwingineko, hasa watumishi wa umma. Lakini tangu mwaka 2021, kitabu kinabainisha, mradi unaonekana kutelekezwa, huku watu wengi waliokuwa wameanza ujenzi wakionekana kubadili mawazo.

Waandishi wa kitabu hicho wamebaini kuwa kati ya viwanja vyote vilivyopatikana katika mradi huu, ni asilimia 30 tu ndio vinaendelezwa. Wamebaini pia kuwa kuna hali ya kuzorota kwa biashara huko Chato na kwamba furaha kubwa iliyoshuhudiwa kati ya 2015 na 2021, imefifia.
Biashara nyingi ambazo zilikuwa zimeanza kuota mizizi, hususan za ujenzi, zimesimama na kuwa tangu Machi 2021 biashara nyingi zimefungwa. Wawekezaji wamepunguza kasi au wamebadili mawazo yao.

Timu ya utafiti ya kitabu ilibaini kuwa watumishi wengi wa Serikali, hasa wale wa ofisi binafsi ya rais, walinunua viwanja hivyo ili kumvutia. Baadhi yao walikuwa wameanza ujenzi, lakini hawajafanya maendeleo zaidi tangu Machi 2021 Magufuli alipoaga dunia.
Waandishi wa kitabu wamebaini kuwa wengi wao walikuwa wakiendeleza viwanja vyao wakati wa safari za kikazi kwenda Chato kwa sababu wangekaa Chato kwa miezi kadhaa kulingana na muda wa kukaa kwa bosi wao, lakini kwa kuwa safari rasmi zimekoma, nao wameacha kwenda.

Kitabu kinataja ujenzi wa Hoteli ya Burigi-Chato Park. Jiwe la msingi liliwekwa na Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo, Dk Hamis Kigwangalla Oktoba 10, 2019. Lakini shughuli za ujenzi wake nazo zimesimama na eneo lipo katika hali mbaya.
Watu walitabili, lakini utabili ukatimia kabla hata mizizi haijaota
 
Nipo Chato yaliyoandikwa hapa nikweli tupu kuna watu walikuwa na viwanja vyao wakazingua wanataka mamilioni sahivi wanalia bora wangeuza wakati huo kwa sasa wanakubembeleza hata laki 5 uchukuwe kiwanja. Maisha haya balaa sana
 
Haya yote ni sehemu ndogo tu ya maovu, ukatili, ufisadi, ubadhirifu, hasara, wendawazimu na ubovu wake.

Nawashukuru na kuwapongeza waandishi na wachapishaji kwa uzalendo wao.
Niwaombe na kuwatia moyo wengine kujitokeza na kuueleza umma yaliyokuwa yakijiri gizani. Lazima ukweli ujulikane na haki itendeke, ili tusijerudi tena huko asilan!

Kwa wale watetezi wa "legacy ya Kishetani " na mashabiki wa Mwendazake, ambao hujietetea kusema "...mbona tuhuma hizi/zinaletwa sasa.....kwa nini zisingetolewa alipokuwa hai ili "
'azijibu au kujitetea'....". Utetezi huo ni wa kipumbavu na wa kinafiki - hivi kuna mtu yeyote aliyepingana na dikteta hadharani, iwe kimawazo au kimatendo akabaki halafu salama? Mwendazake majibu na utetezi wake si ulijulikana waziwazi na kushagiliwa na "wanyonge" - kuua, kufilisi, kutesa, kufunga???

Je damu, maumivu, ulemavu na ukatili, hasara nk waliofanyiwa "wapinzani" wake hamkuviona wala kusikia?? Ukweli mnaujua na siku moja mtakiri mbele za Mola wetu.

Pamoja na hayo, budi sasa mjiandae kusikia na kuona bila chenga authentic 'replay' ya aliyoyatenda "shujaa" wenu dhalim Magufuli kwa HDV.
Tena haya ni mwanzo tu. Kuna mengi mno, tena ya kutisha tutaendelea kuhabirishwa siku na miaka ijayo.
 
Chato=Gbadolite.Ni kweli alitaka aendeleze kwao kama Mkwere alivyotaka kuendeleza kwao lkn angalia na mazingira kwanza kabla ya kutupa shilingi ikiwa mradi husika utadumu au ukiondoka nao umekufa.By the way Mzilankende alijua ana muda mrefu ila bahat mbaya muda wake ulikuwa ukingoni.Nilichokuwa naogopa ni kukaa siku moja nikijua mtu atatawala daima milele baada ya kutengua katiba hii kitu ilikuwa inaniumiza sana kichwa
 
Wapi kinapatikana kitabu hiki?

Kumbukeni na mm nakaribia kutoa kitabu changu kiitwacho "MAGUFULI, The Master of Chaos".
Kila la heri.

Pamoja na utangulizi msisahau kutujulishs vitabu venu vitakapokuwa vinapatikana, home and abroad.
 
Nipo Chato yaliyoandikwa hapa nikweli tupu kuna watu walikuwa na viwanja vyao wakazingua wanataka mamilioni sahivi wanalia bora wangeuza wakati huo kwa sasa wanakubembeleza hata laki 5 uchukuwe kiwanja. Maisha haya balaa sana
Asante kwa kutupa ushahidi.
 
Kama Nyerere angekuwa na ubinafsi kama wa huyu mwamba wa chato basi musoma ingekuwa Jiji la pili kwa ukubwa baada ya dar.Tena Kuna mbuga ya wanyama ya Serengeti sio ile ya kutengeneza burigi chato.ila mzee wa watu hakuwa na makuu kabisa
Tukiuliza kwani kilifanyika nini chato kikubwa? Utasikia watu wazima wanalalamikia taa za barabarani! Ujenzi wa CRDB, uwanja wa mpira! Mambo ya kijinga kabisa as if kama sehemu nyingine hamna!
 
Chato=Gbadolite.Ni kweli alitaka aendeleze kwao kama Mkwere lkn angalia na mazingira kwanza kabla ya kutupa shilingi ikiwa mradi husika utadumu au ukiondoka nao umekufa.By the way Mzilankende alijua ana muda mrefu ila bahat mbaya muda wake ulikuwa ukingoni.Nilichokuwa naogopa ni kukaa siku moja nikijua mtu atatawala daima milele baada ya kutengua katiba hii kitu ilikuwa inaniumiza sana kichwa
Pole kwa hilo; yaani hata mimi lilinisumbua hasa kati ya 2017/2018, nilifuatilia kauli na matendo yake wakati wa kampeni 2020 na alionyesha kiburi na jeuri hatari sana; baada tu ya uchaguzi wa 2020, nilipata majibu yaliyonipa amani sana. Nakumbuka nilitamka "Magufuli kafanya yake, lakini si lazima kwamba atamaliza huu mhula" - Maana niliona jinsi alivyovuka mstari mwekundu wa uovu, na hakujali kabisa. Nilihisi na kuamini 100% kwamba sasa Magufuli alijiweka rasmi ulingoni dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kiburi na tamaa zake vilimfikisha kwenye 'point of no return'. Kuanzia pale ilikuwa ni kuhesabu tu siku na saa - Litimie.

::By the way; huwa iko hivyo hata kwenye maisha ya kawaida tu ya watu. Ukichunguza (observe) utaona, huwa kuna downward patterns ambazo baadaye huwa trends....halafu - The End.

"Ushujaa" na ujasiri wake ulikuwa wa Kishetani kabisa. Wengine tutaendelea kumshukuru Mwenyezi MUNGU kila tunapokumbuka haya.
 
Na hivyo ndivyo Benki ya CRDB ilivyojikuta kwenye mtanziko ilipoamriwa kufungua tawi Chato lililofunguliwa Machi 9, 2018.
Kitabu kinamnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akisema benki hiyo ilikuwa imekataa kufungua tawi hilo Chato kwa sababu upembuzi yakinifu umeonyesha hakuna uwezekano wa kufanya biashara, lakini kuanzishwa kwa tawi hilo kulitokana na “utafiti uliofanywa na Rais mwenyewe
Hii kauli aliongea Dr Kimei mwenyewe siku ya ufunguzi nakumbuka
 
Naomba kuuliza Tangu lini kijiji kikawa na watu zaidi ya laki 5?
 
Katika mfululizo wa mapitio ya kitabu, 'I am the State: A President's Whisper from Chato' (Mimi ni Dola: Mnong'ono wa Rais kutoka Chato) leo tunaangazia sura yake ya pili inayozungumzia Chato kama kijiji ambacho kilikaribia kuwa makao makuu ya mkoa.

Kitabu kinaanza kwa kuelezea kulivyokuwa na mdororo wa uchumi nchini kote, uliosababishwa na mazingira mabaya ya biashara kati ya 2015 na 2020. Kwa miaka mitatu mfululizo (2016-2018), karibu biashara 4,640 zilifungwa kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya biashara yanayotokana na sera mbaya, uwezo mdogo wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wadogo na wa kati na ukosefu wa motisha.

Kelele za kupungua na hatimaye kufungwa kwa biashara kote nchini zilitolewa mara kadhaa na wabunge, ingawa Serikali haikuwahi kukiri jambo hilo.

Waandishi wa kitabu hicho miongoni mwa vyanzo walivyotumia, kimojawapo kimesema fedha kwenye mzunguko zilipungua kutoka asilimia 22 mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka 2018 na kwamba kati ya 2011 na 2017 ukuaji wa Pato la Taifa (GNP) ulikuwa wa asilimia 7.8 lakini kufikia 2018 ulikuwa chini hadi asilimia 6.8.

Kutokana na hali kuwa mbaya, kati ya mwaka 2015 na 2020, Benki Kuu (BoT) ilichukua hatua kadhaa ama kusimamisha, kuunganisha au kufunga baadhi ya benki, zikiwamo Benki ya Wanawake Tanzania, Twiga BanCorp, Ecobank, Efatha Bank, Covenant Bank, Kagera Farmers' Cooperative Bank, Meru Community Bank na Njombe Community Bank.

Waandishi wa kitabu hicho wanasema ingawa ni sahihi kwa BoT kuchukua hatua kali dhidi ya mabenki katika hali ya ufilisi, ni kweli vilevile kwamba hali ya uchumi wa Taifa ina athari kubwa kwa hali ya taasisi hizo za kifedha.
Waandishi hao waligundua kuwa karibu benki zote zilizoathirika zilikuwa za binafsi, isipokuwa Twiga Bancorp, ambayo hatimaye iliunganishwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) pamoja na Benki ya Wanawake na kuunda Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Kwa hiyo, kadiri biashara zilivyokuwa zikipungua siku baada ya siku tangu 2016, hatima ya sekta kibinafsi ilikuwa katika hali mbaya zaidi. Serikali iliamua kuunda "Kikosi Kazi" kukusanya kodi kwa niaba ya taasisi yenye mamlaka hayo kisheria, TRA.
Katika mchakato huo, biashara nyingi zilikumbana na hali ngumu zaidi. Akaunti nyingi za biashara zilizuiwa na mabilioni ya pesa kuchukuliwa. Katika baadhi ya matukio, kwa sababu zinazojulikana zaidi na Serikali, wamiliki wa biashara walishtakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi.

Kuhusu Chato
Baada ya kueleza kinaganaga hali ya biashara ilivyokuwa na masaibu yaliyowakumba wafanyabiashara wengi, waandishi wa ‘I am the State’ wakaigeukia Chato.
Wanasema wakati biashara zikiporomoka katika maeneo mengi ya nchi kati ya 2016 na 2020 kutokana na mazingira yaliyotajwa hapo juu, kipindi hicho kilikuwa cha neema kwa Chato.
Ulianzishwa uwekezaji wa kimkakati katika wilaya ambayo haikujulikana kwa jumuiya yoyote kubwa ya wafanyabiashara, kinaandika kitabu hicho.
Biashara za Chato hazikuendeshwa na soko, wanasema, lakini zilisukumwa kisiasa na Rais ambaye alikuwa amejitokeza kukaidi sayansi ya biashara katika azma yake ya kubadili na kuendeleza mji wake wa Chato.
Na hivyo ndivyo Benki ya CRDB ilivyojikuta kwenye mtanziko ilipoamriwa kufungua tawi Chato lililofunguliwa Machi 9, 2018.
Kitabu kinamnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akisema benki hiyo ilikuwa imekataa kufungua tawi hilo Chato kwa sababu upembuzi yakinifu umeonyesha hakuna uwezekano wa kufanya biashara, lakini kuanzishwa kwa tawi hilo kulitokana na “utafiti uliofanywa na Rais mwenyewe.”

Ilionekana wazi kuwa pamoja na kwamba CRDB inaongoza kwenye orodha ya benki kubwa nchini kama NMB, NBC, Stanbic, Standard Chartered, Absa, DTB, Exim, Azania na Citi Bank, haikuwa na nia ya kunyakua fursa hii ya kuwepo Chato hadi ilipolazimishwa na mkuu wa nchi.

Watafiti wa kitabu hicho walizunguka Chato kuangalia huduma mbalimbali katika hoteli, baa, migahawa na nyumba za wageni. Uchunguzi wao ukabaini kuwa nyumba nyingi za kulala wageni zimeamua kushusha gharama za huduma kutokana na kupungua kwa wateja.

Wakati wa utafiti wao walitembelea hoteli kubwa Chato kwa kulinganisha. Katika matokeo ya utafiti wanabainisha kuwa biashara zilikuwa zimedorora.
Mathalan, wanazungumzia pia maeneo ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Chato ilipima na kuuza takriban viwanja 2,000.
Kati ya hivyo, viwanja 1,500 vilipata wateja ingawa wengi kwa mkopo. Mradi huo ulivutia wanunuzi kutoka Chato na kwingineko, hasa watumishi wa umma. Lakini tangu mwaka 2021, kitabu kinabainisha, mradi unaonekana kutelekezwa, huku watu wengi waliokuwa wameanza ujenzi wakionekana kubadili mawazo.

Waandishi wa kitabu hicho wamebaini kuwa kati ya viwanja vyote vilivyopatikana katika mradi huu, ni asilimia 30 tu ndio vinaendelezwa. Wamebaini pia kuwa kuna hali ya kuzorota kwa biashara huko Chato na kwamba furaha kubwa iliyoshuhudiwa kati ya 2015 na 2021, imefifia.
Biashara nyingi ambazo zilikuwa zimeanza kuota mizizi, hususan za ujenzi, zimesimama na kuwa tangu Machi 2021 biashara nyingi zimefungwa. Wawekezaji wamepunguza kasi au wamebadili mawazo yao.

Timu ya utafiti ya kitabu ilibaini kuwa watumishi wengi wa Serikali, hasa wale wa ofisi binafsi ya rais, walinunua viwanja hivyo ili kumvutia. Baadhi yao walikuwa wameanza ujenzi, lakini hawajafanya maendeleo zaidi tangu Machi 2021 Magufuli alipoaga dunia.
Waandishi wa kitabu wamebaini kuwa wengi wao walikuwa wakiendeleza viwanja vyao wakati wa safari za kikazi kwenda Chato kwa sababu wangekaa Chato kwa miezi kadhaa kulingana na muda wa kukaa kwa bosi wao, lakini kwa kuwa safari rasmi zimekoma, nao wameacha kwenda.

Kitabu kinataja ujenzi wa Hoteli ya Burigi-Chato Park. Jiwe la msingi liliwekwa na Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo, Dk Hamis Kigwangalla Oktoba 10, 2019. Lakini shughuli za ujenzi wake nazo zimesimama na eneo lipo katika hali mbaya.
Upotoshaji upotoshaji, Watanzania wana haki ya kupewa maelezo sahihi. Sehemu ya kwanza ya kuchumi kudorora kuna mambo 3 hayasemwi. La kwanza ni Covid-19 ya 2019/2020 hii inajibu kila kitu. Marehemu "Dikteta" alikataa kuifunga Nchi, hatukuumia kama walivyoumia almost dunia nzima. He was a Visionary, more so than Trump, or the EU, or WHO, dunia nzima. Na kuna sala tulifunga kwa kuongozwa na Mufti na Askofu Malasusa na Askofu Ruwaichi kwa pamoja, umoja huo haujawahi kuonekana hapa duniani.

Imetajwa benki ya CRDB sababu za kipuuzi tu. Maendeleo huletwa na uwepo wa benki, hasa kama ni za umma, siyo benki kupelekwa kwenye maendeleo tayari. Hili Dr Kimei analijua, na ndivyo alivyosema, Wahariri kwa wametumbukiza maneno yao mdomoni mwake kwa sababu zao.

Jiulize NBC: hii 1997 ilipobinafsishwa, matawi mazuri yaliyokuwa mijini yalinyofolewa wakapewa makaburu almost for free. NBC wakaitafuna, sasa angalia NBC iko wapi? Yale matawi ya hasara yemekaa kama Chatochato yalimegwa ikapewa NMB mpya, benki ya makabwela. Leo NMB ndiyo benki kubwa inayoongoza Tanzania, how do you explain that?

NBC ilikuwa iende DSE kama mashirika mengine TBL, TCC, TOL, nk, wanunue Watanzania, lakini hadi leo makaburu wamekataa kuipeleka DSE kwa makusudi kabisa, inatumiwa kama conduit ya hela zao tu.

Pia imetajwa benki moja eti "mbovu" - ya Twiga Bancorp. Hii si mbovu hata kidogo, it was the best bank in the NBC system kwa sababu ndiyo pekee iliyokuwa na forex wakati mgumu tulipokuwa Nchi haina hela za kigeni. Ilikuwa ichukukiwe na makaburu pamoja na NBC lakini ni Wazalendo hawa hawa kina Dr Kimei wakaona ukweli huu ikanyofolewa NBC haraka haraka kabla haijauzwa. Hilo nalo halisemwi, Magufuli wala hahusiki.

Benki zingine ikiwamo ya Wanawake ni za tangu zamani, na hizo zingine zililemewa na Covid, si za Magufuli.

Umetajwa pia mradi wa hoteli ya Burigi Chato, hii tatizo lake pekee lilikuwa Covid mapato ya Utalii kupungua, si ya Magufuli. Mbuga za wanyama magharibi ya Ziwa toka Kyerwa Ibanda hadi Rubondo na Chato ni nzuri mno, uamuzi wa kuzikwamua haukuwa wa Magufuli ni bahati mbaya tu ukakunbwa na Covid.

Huo "utafiti" wa Wahariri ni sawa na zero, sijui ni nani aliyewalipa kutunga hadithi hizo za kitoto.

Naomba wasomaji haya wayatafakari kabla hatujaja "utafiti" wa Chato kama Chato.
 
Mmeshauza nakala ngapi za hicho kigazeti chenu? Jaribuni kugawa bure kina mama wapate karatasi za kufungia maandazi
 
Tukiuliza kwani kilifanyika nini chato kikubwa? Utasikia watu wazima wanalalamikia taa za barabarani! Ujenzi wa CRDB, uwanja wa mpira! Mambo ya kijinga kabisa as if kama sehemu nyingine hamna!
Sio kwamba havipo sehemu zingine ila sehemu vipojengwa ndio shida,hivi unaonaje tukijenga shule katikati ya mbuga ya wanyama.will it be useful? Yani uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini chato ambapo hakuna kivutio chochote Wala shughuli za kiuchumi,really?

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom