Chato: Kijiji kilichokaribia kuwa makao makuu ya mkoa-2

Haya yote ni sehemu ndogo tu ya maovu, ukatili, ufisadi, ubadhirifu, hasara, wendawazimu na ubovu wake.

Nawashukuru na kuwapongeza waandishi na wachapishaji kwa uzalendo wao.
Niwaombe na kuwatia moyo wengine kujitokeza na kuueleza umma yaliyokuwa yakijiri gizani. Lazima ukweli ujulikane na haki itendeke, ili tusijerudi tena huko asilan!

Kwa wale watetezi wa "legacy ya Kishetani " na mashabiki wa Mwendazake, ambao hujietetea kusema "...mbona tuhuma hizi/zinaletwa sasa.....kwa nini zisingetolewa alipokuwa hai ili "
'azijibu au kujitetea'....". Utetezi huo ni wa kipumbavu na wa kinafiki - hivi kuna mtu yeyote aliyepingana na dikteta hadharani, iwe kimawazo au kimatendo akabaki halafu salama? Mwendazake majibu na utetezi wake si ulijulikana waziwazi na kushagiliwa na "wanyonge" - kuua, kufilisi, kutesa, kufunga???

Je damu, maumivu, ulemavu na ukatili, hasara nk waliofanyiwa "wapinzani" wake hamkuviona wala kusikia?? Ukweli mnaujua na siku moja mtakiri mbele za Mola wetu.

Pamoja na hayo, budi sasa mjiandae kusikia na kuona bila chenga authentic 'replay' ya aliyoyatenda "shujaa" wenu dhalim Magufuli kwa HDV.
Tena haya ni mwanzo tu. Kuna mengi mno, tena ya kutisha tutaendelea kuhabirishwa siku na miaka ijayo.

Ukweli ulio wazi yapo mambo mema ambayo Magufuli aliwatendea waTz lakini ukiyaweka kwenye mzani mambo mabaya ya kishetani yalizidi kupita kiasi halafu kwa ujinga wa Hali ya juu alikuwa hachagui Chama Wala siasa, hachagui kabila Wala dini, hakujali unyeti wa yule anayemfanyia ubaya...yaani pamoja na mabaya yake yote eti Kuna wakati alikuwa anakula mahindi barabarani bila kunawa mikono , msukuma yule Bora Mungu alivyomwambia "Pita huku" ama sivyo vijana wangetumia manati ya kizungu maana ilikuwa Hanna namna
 
Unakumbuka story yake ya kujenga kanisa kijijini kwake na kuamuru Sadaka apewe Mama yake?? Watoto wa juzi hawajui haya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na yule ndugu aliyemmaliza je? Ndugu wakachachama?
 
Na kumchafua Magufuli kunahitaji propaganda sana na upotoshaji mkubwa maana ana mazuri mengi mno na mara nyingi ukimuona mtu anaandika habari mbaya kuhusu Magufuli ni wale vyeti feki, wakwepa kodi, wadhulumaji, mafisadi, wezi, walamba asali, majizi, wauza ngada mimi sioni faida ya huu uharo mnaoufanya mitandaoni kumchafua Magufuli ili hali huo uhuru wa vyombo vya habari haujaondoa ufisadi mkubwa unaofanyika leo maisha magumu kwa watanzania
Rais yeyeote duniani huchaguliwa kwa lengo la kufanya mazuri kwa wananchi wake, kwa mantiki hii Rais kufanya mazuri ni wajibu wake usio hitaji kusifiwasifiwa maana ni sawa na kumsifia baba kumnunulia mwanae mdogo kaptula na wala baba huyo hawezi kujitangazatangaza mitaani kwamba kanunua kaptula.

Wanao andika mabaya ya Magufuli siyo vyeti feki maana majina yao yapo kwenye kitabu walichokiandika na hatukuwaona ktk orodha ya vyeti feki bali wewe sasa inaonekana kama ndiye mwenye cheti feki maana hata kusoma umeshindwa.

Mazuri ya Rais haiwezi kuwa stori maana Ndiyo wajibu wake ila akifanya mabaya tena yake yanayohatarisha uhai wa watu na taifa ndipo kumbukumbu ya maandishi hulazika kuwekwa ili kuepuka makosa hayo kujirudia tena kwa vizazi vijavyo.

Magufuli alifanya mazuri mengi lakini pia alifanya "mabaya Sana"machache yaliyofunika hata uzuri wa mengi. Na hili iltakuwa somo zuri kwa kila kiongozi.

Mfano mbaya Sana ni mauaji ya wakosoaji wake hata akaweza kumuua aliyehoji elimu yake feki ya udaktari (PhD) Ben Saanane. Kumbe inaonekana hata yeye Magufuli mwenyewe alikuwa na cheti feki duu! Ama kweli waswahili tunasema "Mchawi humjua Mchawi mwenzie".
 
Sio kwamba havipo sehemu zingine ila sehemu vipojengwa ndio shida,hivi unaonaje tukijenga shule katikati ya mbuga ya wanyama.will it be useful? Yani uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini chato ambapo hakuna kivutio chochote Wala shughuli za kiuchumi,really?

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
😅😅😅
 
Hivi hayo matrilioni yanayopigwa na mafisadi hamyaoni mkayaandikia kitabu mmebaki kumsema sema marehemu Magufuli kwa chato palikuwa ni Burundi mnajua mnafanya unafiki na chuki nyie vyeti feki, wakwepa kodi, mafisadi,wahujumu uchumi
Hapa hatumsemi marehemu ila tunawasema wafuasi wake kupitia yeye ili mjifunze kuwa na adabu na utii.maana tukiwaacha mtaendelea kuwadanganya hao mliowaita wanyonge huku mkijua mnawahadaa kwakuwa hawakuwa na elimu ya kutambua uovu wenu

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Hapana. Nachukia kwamba Magufuli alitumia mabilioni ya watanzania kujenga miradi mikubwa ambayo sasa inakufa kwa sababu haikustahi kujengwa Chato.
Weka takwimu za miradi ya maendeleo kwa kila mkoa tuone ni mkoa gani unaongoza
 
Nipo Chato yaliyoandikwa hapa nikweli tupu kuna watu walikuwa na viwanja vyao wakazingua wanataka mamilioni sahivi wanalia bora wangeuza wakati huo kwa sasa wanakubembeleza hata laki 5 uchukuwe kiwanja. Maisha haya balaa sana
Hata Dodoma hali ilikuwa zaidi ya hapo
 
Rais yeyeote duniani huchaguliwa kwa lengo la kufanya mazuri kwa wananchi wake, kwa mantiki hii Rais kufanya mazuri ni wajibu wake usio hitaji kusifiwasifiwa maana ni sawa na kumsifia baba kumnunulia mwanae mdogo kaptula na wala baba huyo hawezi kujitangazatangaza mitaani kwamba kanunua kaptula.

Wanao andika mabaya ya Magufuli siyo vyeti feki maana majina yao yapo kwenye kitabu walichokiandika na hatukuwaona ktk orodha ya vyeti feki bali wewe sasa inaonekana kama ndiye mwenye cheti feki maana hata kusoma umeshindwa.

Mazuri ya Rais haiwezi kuwa stori maana Ndiyo wajibu wake ila akifanya mabaya tena yake yanayohatarisha uhai wa watu na taifa ndipo kumbukumbu ya maandishi hulazika kuwekwa ili kuepuka makosa hayo kujirudia tena kwa vizazi vijavyo.

Magufuli alifanya mazuri mengi lakini pia alifanya "mabaya Sana"machache yaliyofunika hata uzuri wa mengi. Na hili iltakuwa somo zuri kwa kila kiongozi.

Mfano mbaya Sana ni mauaji ya wakosoaji wake hata akaweza kumuua aliyehoji elimu yake feki ya udaktari (PhD) Ben Saanane. Kumbe inaonekana hata yeye Magufuli mwenyewe alikuwa na cheti feki duu! Ama kweli waswahili tunasema "Mchawi humjua Mchawi mwenzie".
Mkuu nimependa Paragraph ya Tatu
 
Wewe ulitaka akajenge kwenu!
Zao la shule za kata.
Fedha alizochezea huko Chato ni kodi za waTanganyika ambazo zilistahili kutumia vizuri na utaratibu tuliojiwekea.

Laiti fedha zilizichezewa zingekuwa zake au familia yake hakuna ambaye angelalamika.

Najaribu kufikiria kama angeanza kuongoza taifa letu,Tanganyika ingekuwa na ukabila mbaya kuliko taifa la Kenya.Mungu mbariki Mwl Nyerere aliijenga misingi mizuri ya umoja na upendo Tanganyika.
 
Mgangaji na yeye analia biashara mbaya.

Tanzania ilikuwa inaongozwa na mtu wa hovyo kabisa kuwahi kutokea
Katika mfululizo wa mapitio ya kitabu, 'I am the State: A President's Whisper from Chato' (Mimi ni Dola: Mnong'ono wa Rais kutoka Chato) leo tunaangazia sura yake ya pili inayozungumzia Chato kama kijiji ambacho kilikaribia kuwa makao makuu ya mkoa.

Kitabu kinaanza kwa kuelezea kulivyokuwa na mdororo wa uchumi nchini kote, uliosababishwa na mazingira mabaya ya biashara kati ya 2015 na 2020. Kwa miaka mitatu mfululizo (2016-2018), karibu biashara 4,640 zilifungwa kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya biashara yanayotokana na sera mbaya, uwezo mdogo wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wadogo na wa kati na ukosefu wa motisha.

Kelele za kupungua na hatimaye kufungwa kwa biashara kote nchini zilitolewa mara kadhaa na wabunge, ingawa Serikali haikuwahi kukiri jambo hilo.

Waandishi wa kitabu hicho miongoni mwa vyanzo walivyotumia, kimojawapo kimesema fedha kwenye mzunguko zilipungua kutoka asilimia 22 mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka 2018 na kwamba kati ya 2011 na 2017 ukuaji wa Pato la Taifa (GNP) ulikuwa wa asilimia 7.8 lakini kufikia 2018 ulikuwa chini hadi asilimia 6.8.

Kutokana na hali kuwa mbaya, kati ya mwaka 2015 na 2020, Benki Kuu (BoT) ilichukua hatua kadhaa ama kusimamisha, kuunganisha au kufunga baadhi ya benki, zikiwamo Benki ya Wanawake Tanzania, Twiga BanCorp, Ecobank, Efatha Bank, Covenant Bank, Kagera Farmers' Cooperative Bank, Meru Community Bank na Njombe Community Bank.

Waandishi wa kitabu hicho wanasema ingawa ni sahihi kwa BoT kuchukua hatua kali dhidi ya mabenki katika hali ya ufilisi, ni kweli vilevile kwamba hali ya uchumi wa Taifa ina athari kubwa kwa hali ya taasisi hizo za kifedha.
Waandishi hao waligundua kuwa karibu benki zote zilizoathirika zilikuwa za binafsi, isipokuwa Twiga Bancorp, ambayo hatimaye iliunganishwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) pamoja na Benki ya Wanawake na kuunda Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Kwa hiyo, kadiri biashara zilivyokuwa zikipungua siku baada ya siku tangu 2016, hatima ya sekta kibinafsi ilikuwa katika hali mbaya zaidi. Serikali iliamua kuunda "Kikosi Kazi" kukusanya kodi kwa niaba ya taasisi yenye mamlaka hayo kisheria, TRA.
Katika mchakato huo, biashara nyingi zilikumbana na hali ngumu zaidi. Akaunti nyingi za biashara zilizuiwa na mabilioni ya pesa kuchukuliwa. Katika baadhi ya matukio, kwa sababu zinazojulikana zaidi na Serikali, wamiliki wa biashara walishtakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi.

Kuhusu Chato
Baada ya kueleza kinaganaga hali ya biashara ilivyokuwa na masaibu yaliyowakumba wafanyabiashara wengi, waandishi wa ‘I am the State’ wakaigeukia Chato.
Wanasema wakati biashara zikiporomoka katika maeneo mengi ya nchi kati ya 2016 na 2020 kutokana na mazingira yaliyotajwa hapo juu, kipindi hicho kilikuwa cha neema kwa Chato.
Ulianzishwa uwekezaji wa kimkakati katika wilaya ambayo haikujulikana kwa jumuiya yoyote kubwa ya wafanyabiashara, kinaandika kitabu hicho.
Biashara za Chato hazikuendeshwa na soko, wanasema, lakini zilisukumwa kisiasa na Rais ambaye alikuwa amejitokeza kukaidi sayansi ya biashara katika azma yake ya kubadili na kuendeleza mji wake wa Chato.
Na hivyo ndivyo Benki ya CRDB ilivyojikuta kwenye mtanziko ilipoamriwa kufungua tawi Chato lililofunguliwa Machi 9, 2018.
Kitabu kinamnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akisema benki hiyo ilikuwa imekataa kufungua tawi hilo Chato kwa sababu upembuzi yakinifu umeonyesha hakuna uwezekano wa kufanya biashara, lakini kuanzishwa kwa tawi hilo kulitokana na “utafiti uliofanywa na Rais mwenyewe.”

Ilionekana wazi kuwa pamoja na kwamba CRDB inaongoza kwenye orodha ya benki kubwa nchini kama NMB, NBC, Stanbic, Standard Chartered, Absa, DTB, Exim, Azania na Citi Bank, haikuwa na nia ya kunyakua fursa hii ya kuwepo Chato hadi ilipolazimishwa na mkuu wa nchi.

Watafiti wa kitabu hicho walizunguka Chato kuangalia huduma mbalimbali katika hoteli, baa, migahawa na nyumba za wageni. Uchunguzi wao ukabaini kuwa nyumba nyingi za kulala wageni zimeamua kushusha gharama za huduma kutokana na kupungua kwa wateja.

Wakati wa utafiti wao walitembelea hoteli kubwa Chato kwa kulinganisha. Katika matokeo ya utafiti wanabainisha kuwa biashara zilikuwa zimedorora.
Mathalan, wanazungumzia pia maeneo ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Chato ilipima na kuuza takriban viwanja 2,000.
Kati ya hivyo, viwanja 1,500 vilipata wateja ingawa wengi kwa mkopo. Mradi huo ulivutia wanunuzi kutoka Chato na kwingineko, hasa watumishi wa umma. Lakini tangu mwaka 2021, kitabu kinabainisha, mradi unaonekana kutelekezwa, huku watu wengi waliokuwa wameanza ujenzi wakionekana kubadili mawazo.

Waandishi wa kitabu hicho wamebaini kuwa kati ya viwanja vyote vilivyopatikana katika mradi huu, ni asilimia 30 tu ndio vinaendelezwa. Wamebaini pia kuwa kuna hali ya kuzorota kwa biashara huko Chato na kwamba furaha kubwa iliyoshuhudiwa kati ya 2015 na 2021, imefifia.
Biashara nyingi ambazo zilikuwa zimeanza kuota mizizi, hususan za ujenzi, zimesimama na kuwa tangu Machi 2021 biashara nyingi zimefungwa. Wawekezaji wamepunguza kasi au wamebadili mawazo yao.

Timu ya utafiti ya kitabu ilibaini kuwa watumishi wengi wa Serikali, hasa wale wa ofisi binafsi ya rais, walinunua viwanja hivyo ili kumvutia. Baadhi yao walikuwa wameanza ujenzi, lakini hawajafanya maendeleo zaidi tangu Machi 2021 Magufuli alipoaga dunia.
Waandishi wa kitabu wamebaini kuwa wengi wao walikuwa wakiendeleza viwanja vyao wakati wa safari za kikazi kwenda Chato kwa sababu wangekaa Chato kwa miezi kadhaa kulingana na muda wa kukaa kwa bosi wao, lakini kwa kuwa safari rasmi zimekoma, nao wameacha kwenda.

Kitabu kinataja ujenzi wa Hoteli ya Burigi-Chato Park. Jiwe la msingi liliwekwa na Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo, Dk Hamis Kigwangalla Oktoba 10, 2019. Lakini shughuli za ujenzi wake nazo zimesimama na eneo lipo katika hali mbaya.
 
Na kitabu cha mazuri ya Magufuli kiandikwe pia ili kubalance stori maana aliijenga Dodoma,alinunua ndege,hapakuwa na mifumuko ya bei kwenye utawala wake,nchi iliingia uchumi wa kati,alidhibiti,wala rushwa na mafisadi,alijenga hospital ya mwalimu Nyerere iliyoshindikana miaka 40 , alinunua rada 3,alifungua balozi 6, alijenga barabara sehemu mbalimbali,aliweka mradi mkubwa wa maji Arusha,alianza ujenzi wa bwawa la umeme la stigler gauge,
Mradi wa maji Arusha si juhudi za mwendazake.

Mradi ulikuwepo tangu enzi za Mkwere.
 
Tukiuliza kwani kilifanyika nini chato kikubwa? Utasikia watu wazima wanalalamikia taa za barabarani! Ujenzi wa CRDB, uwanja wa mpira! Mambo ya kijinga kabisa as if kama sehemu nyingine hamna!
Taa za barabarani kwa ajili ya kuongoza ng'ombe wasigongane
 
Atakama kwani kuweka Taa za. Kuongezea magari ni serikali kuu ndo inafanya hivo? Hiyo ni alama moja wapo ya usalama barabaran haijalishi inatumika wapi!
 
Sio kwamba havipo sehemu zingine ila sehemu vipojengwa ndio shida,hivi unaonaje tukijenga shule katikati ya mbuga ya wanyama.will it be useful? Yani uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini chato ambapo hakuna kivutio chochote Wala shughuli za kiuchumi,really?

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
Songwe kuna kivutio gan cha utalii? Si bora hapo Chato kwa week kuna ruti 2 za air Tanzania kuliko Songwe umejengwa uwanja na hakuna ndege zinaenda
 
Ukweli ulio wazi yapo mambo mema ambayo Magufuli aliwatendea waTz lakini ukiyaweka kwenye mzani mambo mabaya ya kishetani yalizidi kupita kiasi halafu kwa ujinga wa Hali ya juu alikuwa hachagui Chama Wala siasa, hachagui kabila Wala dini, hakujali unyeti wa yule anayemfanyia ubaya...yaani pamoja na mabaya yake yote eti Kuna wakati alikuwa anakula mahindi barabarani bila kunawa mikono , msukuma yule Bora Mungu alivyomwambia "Pita huku" ama sivyo vijana wangetumia manati ya kizungu maana ilikuwa Hanna namna
Na hayo "mema" aliyotenda pia hayakuwa kwa 'good faith'. Yalikuwa ni sawa na chambo ili kumhadaa samaki.
Sawa tu na tapeli au baradhuli kumnunulia chips na soda binti wa shule ili ampate.

Yanayoitwa "Mazuri" ya Magufuli, mengi yake, ukiyachunguza kidogo tu, utagundua yalilenga kitu fulani kiovu nyuma yake. Yalikuwa na double-purposes. Hayakuwa mema kwa wema.

Yaani alikuwa mwovu tangu kwenye nia na mawazo hadi kwenye yale maigizo yake ya "achievements".
 
Pumbavu zenu nendeni mkautoe uwanja wa ndege ,mbuga na hospital ya kanda
Hahaha umeletewa kitabu hapahapa ili upate kisoma na kujua upumbavu wa mpumbavu unayemlilia kila dskika. Kwakuwa wewe ni mpumbavu hutaelewa utaishia kuwakashifu na kuwatukana kina lisu tu.
Soma hiyo
 
Katika mfululizo wa mapitio ya kitabu, 'I am the State: A President's Whisper from Chato' (Mimi ni Dola: Mnong'ono wa Rais kutoka Chato) leo tunaangazia sura yake ya pili inayozungumzia Chato kama kijiji ambacho kilikaribia kuwa makao makuu ya mkoa.

Kitabu kinaanza kwa kuelezea kulivyokuwa na mdororo wa uchumi nchini kote, uliosababishwa na mazingira mabaya ya biashara kati ya 2015 na 2020. Kwa miaka mitatu mfululizo (2016-2018), karibu biashara 4,640 zilifungwa kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya biashara yanayotokana na sera mbaya, uwezo mdogo wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wadogo na wa kati na ukosefu wa motisha.

Kelele za kupungua na hatimaye kufungwa kwa biashara kote nchini zilitolewa mara kadhaa na wabunge, ingawa Serikali haikuwahi kukiri jambo hilo.

Waandishi wa kitabu hicho miongoni mwa vyanzo walivyotumia, kimojawapo kimesema fedha kwenye mzunguko zilipungua kutoka asilimia 22 mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka 2018 na kwamba kati ya 2011 na 2017 ukuaji wa Pato la Taifa (GNP) ulikuwa wa asilimia 7.8 lakini kufikia 2018 ulikuwa chini hadi asilimia 6.8.

Kutokana na hali kuwa mbaya, kati ya mwaka 2015 na 2020, Benki Kuu (BoT) ilichukua hatua kadhaa ama kusimamisha, kuunganisha au kufunga baadhi ya benki, zikiwamo Benki ya Wanawake Tanzania, Twiga BanCorp, Ecobank, Efatha Bank, Covenant Bank, Kagera Farmers' Cooperative Bank, Meru Community Bank na Njombe Community Bank.

Waandishi wa kitabu hicho wanasema ingawa ni sahihi kwa BoT kuchukua hatua kali dhidi ya mabenki katika hali ya ufilisi, ni kweli vilevile kwamba hali ya uchumi wa Taifa ina athari kubwa kwa hali ya taasisi hizo za kifedha.
Waandishi hao waligundua kuwa karibu benki zote zilizoathirika zilikuwa za binafsi, isipokuwa Twiga Bancorp, ambayo hatimaye iliunganishwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) pamoja na Benki ya Wanawake na kuunda Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Kwa hiyo, kadiri biashara zilivyokuwa zikipungua siku baada ya siku tangu 2016, hatima ya sekta kibinafsi ilikuwa katika hali mbaya zaidi. Serikali iliamua kuunda "Kikosi Kazi" kukusanya kodi kwa niaba ya taasisi yenye mamlaka hayo kisheria, TRA.
Katika mchakato huo, biashara nyingi zilikumbana na hali ngumu zaidi. Akaunti nyingi za biashara zilizuiwa na mabilioni ya pesa kuchukuliwa. Katika baadhi ya matukio, kwa sababu zinazojulikana zaidi na Serikali, wamiliki wa biashara walishtakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi.

Kuhusu Chato
Baada ya kueleza kinaganaga hali ya biashara ilivyokuwa na masaibu yaliyowakumba wafanyabiashara wengi, waandishi wa ‘I am the State’ wakaigeukia Chato.
Wanasema wakati biashara zikiporomoka katika maeneo mengi ya nchi kati ya 2016 na 2020 kutokana na mazingira yaliyotajwa hapo juu, kipindi hicho kilikuwa cha neema kwa Chato.
Ulianzishwa uwekezaji wa kimkakati katika wilaya ambayo haikujulikana kwa jumuiya yoyote kubwa ya wafanyabiashara, kinaandika kitabu hicho.
Biashara za Chato hazikuendeshwa na soko, wanasema, lakini zilisukumwa kisiasa na Rais ambaye alikuwa amejitokeza kukaidi sayansi ya biashara katika azma yake ya kubadili na kuendeleza mji wake wa Chato.
Na hivyo ndivyo Benki ya CRDB ilivyojikuta kwenye mtanziko ilipoamriwa kufungua tawi Chato lililofunguliwa Machi 9, 2018.
Kitabu kinamnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akisema benki hiyo ilikuwa imekataa kufungua tawi hilo Chato kwa sababu upembuzi yakinifu umeonyesha hakuna uwezekano wa kufanya biashara, lakini kuanzishwa kwa tawi hilo kulitokana na “utafiti uliofanywa na Rais mwenyewe.”

Ilionekana wazi kuwa pamoja na kwamba CRDB inaongoza kwenye orodha ya benki kubwa nchini kama NMB, NBC, Stanbic, Standard Chartered, Absa, DTB, Exim, Azania na Citi Bank, haikuwa na nia ya kunyakua fursa hii ya kuwepo Chato hadi ilipolazimishwa na mkuu wa nchi.

Watafiti wa kitabu hicho walizunguka Chato kuangalia huduma mbalimbali katika hoteli, baa, migahawa na nyumba za wageni. Uchunguzi wao ukabaini kuwa nyumba nyingi za kulala wageni zimeamua kushusha gharama za huduma kutokana na kupungua kwa wateja.

Wakati wa utafiti wao walitembelea hoteli kubwa Chato kwa kulinganisha. Katika matokeo ya utafiti wanabainisha kuwa biashara zilikuwa zimedorora.
Mathalan, wanazungumzia pia maeneo ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Chato ilipima na kuuza takriban viwanja 2,000.
Kati ya hivyo, viwanja 1,500 vilipata wateja ingawa wengi kwa mkopo. Mradi huo ulivutia wanunuzi kutoka Chato na kwingineko, hasa watumishi wa umma. Lakini tangu mwaka 2021, kitabu kinabainisha, mradi unaonekana kutelekezwa, huku watu wengi waliokuwa wameanza ujenzi wakionekana kubadili mawazo.

Waandishi wa kitabu hicho wamebaini kuwa kati ya viwanja vyote vilivyopatikana katika mradi huu, ni asilimia 30 tu ndio vinaendelezwa. Wamebaini pia kuwa kuna hali ya kuzorota kwa biashara huko Chato na kwamba furaha kubwa iliyoshuhudiwa kati ya 2015 na 2021, imefifia.
Biashara nyingi ambazo zilikuwa zimeanza kuota mizizi, hususan za ujenzi, zimesimama na kuwa tangu Machi 2021 biashara nyingi zimefungwa. Wawekezaji wamepunguza kasi au wamebadili mawazo yao.

Timu ya utafiti ya kitabu ilibaini kuwa watumishi wengi wa Serikali, hasa wale wa ofisi binafsi ya rais, walinunua viwanja hivyo ili kumvutia. Baadhi yao walikuwa wameanza ujenzi, lakini hawajafanya maendeleo zaidi tangu Machi 2021 Magufuli alipoaga dunia.
Waandishi wa kitabu wamebaini kuwa wengi wao walikuwa wakiendeleza viwanja vyao wakati wa safari za kikazi kwenda Chato kwa sababu wangekaa Chato kwa miezi kadhaa kulingana na muda wa kukaa kwa bosi wao, lakini kwa kuwa safari rasmi zimekoma, nao wameacha kwenda.

Kitabu kinataja ujenzi wa Hoteli ya Burigi-Chato Park. Jiwe la msingi liliwekwa na Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo, Dk Hamis Kigwangalla Oktoba 10, 2019. Lakini shughuli za ujenzi wake nazo zimesimama na eneo lipo katika hali mbaya.
Mungu ni FUNDI sana. Huyu mjinga alisimamisha miradi ya Gesi Mtwara ma ujenzi wa Bagamoyo Port kwa kuiita ile miradi ya kiuwendawazimu. Halafu na yeye anakwenda kuwekeza miundombinu mikubwa kijijini kwake Chato?

Mungu akamuonyesha ukweli kwamba yeye ndiye MWENDAWAZIMU na siyo yule aliyetaka kujenga Bagamoyo Port. Magufuli aendelee kuungua na moto mkali wa jehanam!! Shenzi taipu
 
Nipo Chato yaliyoandikwa hapa nikweli tupu kuna watu walikuwa na viwanja vyao wakazingua wanataka mamilioni sahivi wanalia bora wangeuza wakati huo kwa sasa wanakubembeleza hata laki 5 uchukuwe kiwanja. Maisha haya balaa sana
Hahahahaha . Oh hahahaha.
 
Songwe kuna kivutio gan cha utalii? Si bora hapo Chato kwa week kuna ruti 2 za air Tanzania kuliko Songwe umejengwa uwanja na hakuna ndege zinaenda
Na huyo aliyejenga Songwe pia alikosea vivyo hivyo.

Fedha za umma zinataka zitumike kwa tija na maslahi mapana ya Taifa - kwa utashi na wapendavyo watawala.
Na ndio maana kama nchi zimetumika trillion shs kwenye miradi na uwekezaji nchini lakini value na impact ni very low. Poor leadership, horrible vision, no integrity...... vimetugharimu sana kwa muda mrefu.

Hebu angalia sasa hivi wabunge na hilo Bunge letu. Yaani wabunge wame prioritized kurudi bungeni 2025 kuliko kushughulikia ufisadi ulikothiri ref. CAG reports!
 
Back
Top Bottom