Chato: Kijiji kilichokaribia kuwa makao makuu ya mkoa-2

Chato: Kijiji kilichokaribia kuwa makao makuu ya mkoa-2

kumbe nchi ilishafilisika? Tumshukuru Mungu kutupatia mama maana mwendazake asiweza kukamilisha miradi aliyoianzisha kwa pupa. Yule ana akili ya panzi. Alifakamia pesa alizoacha JK na kuchuka mikopo yeney riba ya kibiashara, akaharibu uhusiano na nchi jirani pamoja na nchi za nje. Kweli Mungu fundi bado anatupenda sijui mpaka leo tungekuwa ktk hali gani.

Mama ameshakaribia kukamilisha miradi yote pamoja na ile mipya aliyoanzisha, amepandisha wafanyakazi madaraja yote, ameongeza mishahara, ametoa ajira sekta zote. Wakulima wanafaidika na mazao yao tunataka nini, tumshukuru Mungu.
Tulishaingizwa Chato wote lakini Mungu wa Watanzania ni mkubwa!
 
Wamegawanyika katika makundi matatu
1. Kuna ambao hawajui (hawakua na access na mitandao, ndio wamepata bundle na smartphones recently)

2. Kuna ambao Wana uwezo mdogo plus Ukabili na ulimbukeni, hawajui chochote ila hawajui kama hawajui. Hawa ni wengi na huna cha kuwaanbia, wamebatizwa jina la Wanyonge, unyonge wao ni upi wakati Wana miguu na mikono na akili, na wenyewe pia hawajui! .

3. La tatu ni lile kama la akina Musiba, Sabaya, Gambo, na wengine akina Charamila ambao hawakuwahi kumiliki kitu halafu ghafla wakapewa madaraka, wakayatumia kama source ya income.

Watu kama Hawa ndio kama yule Mbunge aliyesema kuwa kwa jinsi UBUNGE ulivyo mtamu yuko tayari hata kuua ilimradi TU abaki na ubunge wake.
Hope nimeeleweka
Umeeleweka vizuri sana.
 
Hapana. Nachukia kwamba Magufuli alitumia mabilioni ya watanzania kujenga miradi mikubwa ambayo sasa inakufa kwa sababu haikustahi kujengwa Chato.
Ilistahili ijengwe kwenu? Hakuna miradi mfu maeneo mengine? Machinga complex? Tanganyika Packers? Gineries all over the country? Reli ya kaskazini-nayo mmushukuru huyu mnayemtukana leo kwa kuifufua, majumba ya sinema ya mikoa, skimu za umwagiliaji nk
 
Ilistahili ijengwe kwenu? Hakuna miradi mfu maeneo mengine? Machinga complex? Tanganyika Packers? Gineries all over the country? Reli ya kaskazini-nayo mmushukuru huyu mnayemtukana leo kwa kuifufua, majumba ya sinema ya mikoa, skimu za umwagiliaji nk
Vyote ulivyotaja havikufanyika kwa weledi ilikuwa ni danganya toto yote hayo yamekufa na Magufuli. Alikuwa hasara kwa nchi.
 
Ilistahili ijengwe kwenu? Hakuna miradi mfu maeneo mengine? Machinga complex? Tanganyika Packers? Gineries all over the country? Reli ya kaskazini-nayo mmushukuru huyu mnayemtukana leo kwa kuifufua, majumba ya sinema ya mikoa, skimu za umwagiliaji nk
Tulia basi mzee tulia
Hawakusema isijengwe hapana .walisema ilijengwa bila kufuata utaratibu wa bunge! Hajatukanwa na mtu watu wameandika kitabu baada ya utafiti
I AM THE STATE
 
Vyote ulivyotaja havikufanyika kwa weledi ilikuwa ni danganya toto yote hayo yamekufa na Magufuli. Alikuwa hasara kwa nchi.
Mtatumia miaka yenu iliyosalia kumuandika magufuli na namna hiyo jina lake litazidi kudumu. Leta hasara zaidi alizoleta tujadili
 
Mtatumia miaka yenu iliyosalia kumuandika magufuli na namna hiyo jina lake litazidi kudumu. Leta hasara zaidi alizoleta tujadili
Akina Idd Amin na Mobutu nao watakumbukwa daima lakini kwa mabaya sio mema. Wewe nitajie mradi mmoja wa Magufuli unaoliingizia taifa letu hela.
 
Mkwere unamsingizua tu. Zaidi ya kujijengea makazi yake binafsi alifanya nini tena ndani ya Msoga?
We umepita lini msoga bwashee .kuna bonge ya round about utadhani uko toronto. Katikati ya round about kasimika bonge la nanasi nahsi limetengenezwa kwa tanzanite
 
Mambo mengi ndio alifanya kuendeleza kwao kwa faida yake ila hii chuki isifanye miradi mingine ikatelekezwa ambayo ingeleta manufaa kwa taifa. Mfano mbuga ya burigi ikiendelezwa inaweza kuleta manufaa makubwa. Mfano kuna watalii wanaoenda Rwanda wengi tu wanaishia kuona nyani na rwanda imevutia sana watalii kama hii mbuga isingejumuishwa kwenye chuki kwa mwenda zake binafsi naamini ingeleta manufaa kwa Taifa. Hasa kwa watalii ambao wangeweza kuconnect kutoka Rwanda.
 
Akina Idd Amin na Mobutu nao watakumbukwa daima lakini kwa mabaya sio mema. Wewe nitajie mradi mmoja wa Magufuli unaoliingizia taifa letu hela.
Sawa, Huna hasara zingine? Zimeisha?nakupa hasara zaidi, Ya ndege za cash umeisahau? Reli ya SGR? Meli ziwa Victoria? Hospital za Kanda za Rufaa? Majengo ya mahakama? Tuendelee?
 
Haya yote ni sehemu ndogo tu ya maovu, ukatili, ufisadi, ubadhirifu, hasara, wendawazimu na ubovu wake.

Nawashukuru na kuwapongeza waandishi na wachapishaji kwa uzalendo wao.
Niwaombe na kuwatia moyo wengine kujitokeza na kuueleza umma yaliyokuwa yakijiri gizani. Lazima ukweli ujulikane na haki itendeke, ili tusijerudi tena huko asilan!

Kwa wale watetezi wa "legacy ya Kishetani " na mashabiki wa Mwendazake, ambao hujietetea kusema "...mbona tuhuma hizi/zinaletwa sasa.....kwa nini zisingetolewa alipokuwa hai ili "
'azijibu au kujitetea'....". Utetezi huo ni wa kipumbavu na wa kinafiki - hivi kuna mtu yeyote aliyepingana na dikteta hadharani, iwe kimawazo au kimatendo akabaki halafu salama? Mwendazake majibu na utetezi wake si ulijulikana waziwazi na kushagiliwa na "wanyonge" - kuua, kufilisi, kutesa, kufunga???

Je damu, maumivu, ulemavu na ukatili, hasara nk waliofanyiwa "wapinzani" wake hamkuviona wala kusikia?? Ukweli mnaujua na siku moja mtakiri mbele za Mola wetu.

Pamoja na hayo, budi sasa mjiandae kusikia na kuona bila chenga authentic 'replay' ya aliyoyatenda "shujaa" wenu dhalim Magufuli kwa HDV.
Tena haya ni mwanzo tu. Kuna mengi mno, tena ya kutisha tutaendelea kuhabirishwa siku na miaka ijayo.
Ukitaka kujua kiwango cha upumbavu pamoja na tatizo la afya ya akili kwa watanzania, basi angalia wafuasi wake
 
Sawa, Huna hasara zingine? Zimeisha?nakupa hasara zaidi, Ya ndege za cash umeisahau? Reli ya SGR? Meli ziwa Victoria? Hospital za Kanda za Rufaa? Majengo ya mahakama? Tuendelee?
Hakuna mahali tumetupa fedha kama mradi wa ndege. Tunanunua ndege na kuzipaki uwanjani. SGR, hospitali ya rufaa Chato ni kichekesho kikubwa! Yapo mengi.
 
Hakuna mahali tumetupa fedha kama mradi wa ndege. Tunanunua ndege na kuzipaki uwanjani. SGR, hospitali ya rufaa Chato ni kichekesho kikubwa! Yapo mengi.
Sawa Tuendelee kuaainisha hasara, daraja la Kijazi-Ubungo, stand ya Magufuli mbezi, upanuzi wa barabara hadi kibaha, ujenzi na uhamiaji makao makuu dodoma
 
Katika mfululizo wa mapitio ya kitabu, 'I am the State: A President's Whisper from Chato' (Mimi ni Dola: Mnong'ono wa Rais kutoka Chato) leo tunaangazia sura yake ya pili inayozungumzia Chato kama kijiji ambacho kilikaribia kuwa makao makuu ya mkoa.

Kitabu kinaanza kwa kuelezea kulivyokuwa na mdororo wa uchumi nchini kote, uliosababishwa na mazingira mabaya ya biashara kati ya 2015 na 2020. Kwa miaka mitatu mfululizo (2016-2018), karibu biashara 4,640 zilifungwa kutokana na mazingira yasiyo rafiki ya biashara yanayotokana na sera mbaya, uwezo mdogo wa kibiashara kati ya wafanyabiashara wadogo na wa kati na ukosefu wa motisha.

Kelele za kupungua na hatimaye kufungwa kwa biashara kote nchini zilitolewa mara kadhaa na wabunge, ingawa Serikali haikuwahi kukiri jambo hilo.

Waandishi wa kitabu hicho miongoni mwa vyanzo walivyotumia, kimojawapo kimesema fedha kwenye mzunguko zilipungua kutoka asilimia 22 mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka 2018 na kwamba kati ya 2011 na 2017 ukuaji wa Pato la Taifa (GNP) ulikuwa wa asilimia 7.8 lakini kufikia 2018 ulikuwa chini hadi asilimia 6.8.

Kutokana na hali kuwa mbaya, kati ya mwaka 2015 na 2020, Benki Kuu (BoT) ilichukua hatua kadhaa ama kusimamisha, kuunganisha au kufunga baadhi ya benki, zikiwamo Benki ya Wanawake Tanzania, Twiga BanCorp, Ecobank, Efatha Bank, Covenant Bank, Kagera Farmers' Cooperative Bank, Meru Community Bank na Njombe Community Bank.

Waandishi wa kitabu hicho wanasema ingawa ni sahihi kwa BoT kuchukua hatua kali dhidi ya mabenki katika hali ya ufilisi, ni kweli vilevile kwamba hali ya uchumi wa Taifa ina athari kubwa kwa hali ya taasisi hizo za kifedha.
Waandishi hao waligundua kuwa karibu benki zote zilizoathirika zilikuwa za binafsi, isipokuwa Twiga Bancorp, ambayo hatimaye iliunganishwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) pamoja na Benki ya Wanawake na kuunda Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

Kwa hiyo, kadiri biashara zilivyokuwa zikipungua siku baada ya siku tangu 2016, hatima ya sekta kibinafsi ilikuwa katika hali mbaya zaidi. Serikali iliamua kuunda "Kikosi Kazi" kukusanya kodi kwa niaba ya taasisi yenye mamlaka hayo kisheria, TRA.
Katika mchakato huo, biashara nyingi zilikumbana na hali ngumu zaidi. Akaunti nyingi za biashara zilizuiwa na mabilioni ya pesa kuchukuliwa. Katika baadhi ya matukio, kwa sababu zinazojulikana zaidi na Serikali, wamiliki wa biashara walishtakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi.

Kuhusu Chato
Baada ya kueleza kinaganaga hali ya biashara ilivyokuwa na masaibu yaliyowakumba wafanyabiashara wengi, waandishi wa ‘I am the State’ wakaigeukia Chato.
Wanasema wakati biashara zikiporomoka katika maeneo mengi ya nchi kati ya 2016 na 2020 kutokana na mazingira yaliyotajwa hapo juu, kipindi hicho kilikuwa cha neema kwa Chato.
Ulianzishwa uwekezaji wa kimkakati katika wilaya ambayo haikujulikana kwa jumuiya yoyote kubwa ya wafanyabiashara, kinaandika kitabu hicho.
Biashara za Chato hazikuendeshwa na soko, wanasema, lakini zilisukumwa kisiasa na Rais ambaye alikuwa amejitokeza kukaidi sayansi ya biashara katika azma yake ya kubadili na kuendeleza mji wake wa Chato.
Na hivyo ndivyo Benki ya CRDB ilivyojikuta kwenye mtanziko ilipoamriwa kufungua tawi Chato lililofunguliwa Machi 9, 2018.
Kitabu kinamnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akisema benki hiyo ilikuwa imekataa kufungua tawi hilo Chato kwa sababu upembuzi yakinifu umeonyesha hakuna uwezekano wa kufanya biashara, lakini kuanzishwa kwa tawi hilo kulitokana na “utafiti uliofanywa na Rais mwenyewe.”

Ilionekana wazi kuwa pamoja na kwamba CRDB inaongoza kwenye orodha ya benki kubwa nchini kama NMB, NBC, Stanbic, Standard Chartered, Absa, DTB, Exim, Azania na Citi Bank, haikuwa na nia ya kunyakua fursa hii ya kuwepo Chato hadi ilipolazimishwa na mkuu wa nchi.

Watafiti wa kitabu hicho walizunguka Chato kuangalia huduma mbalimbali katika hoteli, baa, migahawa na nyumba za wageni. Uchunguzi wao ukabaini kuwa nyumba nyingi za kulala wageni zimeamua kushusha gharama za huduma kutokana na kupungua kwa wateja.

Wakati wa utafiti wao walitembelea hoteli kubwa Chato kwa kulinganisha. Katika matokeo ya utafiti wanabainisha kuwa biashara zilikuwa zimedorora.
Mathalan, wanazungumzia pia maeneo ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Chato ilipima na kuuza takriban viwanja 2,000.
Kati ya hivyo, viwanja 1,500 vilipata wateja ingawa wengi kwa mkopo. Mradi huo ulivutia wanunuzi kutoka Chato na kwingineko, hasa watumishi wa umma. Lakini tangu mwaka 2021, kitabu kinabainisha, mradi unaonekana kutelekezwa, huku watu wengi waliokuwa wameanza ujenzi wakionekana kubadili mawazo.

Waandishi wa kitabu hicho wamebaini kuwa kati ya viwanja vyote vilivyopatikana katika mradi huu, ni asilimia 30 tu ndio vinaendelezwa. Wamebaini pia kuwa kuna hali ya kuzorota kwa biashara huko Chato na kwamba furaha kubwa iliyoshuhudiwa kati ya 2015 na 2021, imefifia.
Biashara nyingi ambazo zilikuwa zimeanza kuota mizizi, hususan za ujenzi, zimesimama na kuwa tangu Machi 2021 biashara nyingi zimefungwa. Wawekezaji wamepunguza kasi au wamebadili mawazo yao.

Timu ya utafiti ya kitabu ilibaini kuwa watumishi wengi wa Serikali, hasa wale wa ofisi binafsi ya rais, walinunua viwanja hivyo ili kumvutia. Baadhi yao walikuwa wameanza ujenzi, lakini hawajafanya maendeleo zaidi tangu Machi 2021 Magufuli alipoaga dunia.
Waandishi wa kitabu wamebaini kuwa wengi wao walikuwa wakiendeleza viwanja vyao wakati wa safari za kikazi kwenda Chato kwa sababu wangekaa Chato kwa miezi kadhaa kulingana na muda wa kukaa kwa bosi wao, lakini kwa kuwa safari rasmi zimekoma, nao wameacha kwenda.

Kitabu kinataja ujenzi wa Hoteli ya Burigi-Chato Park. Jiwe la msingi liliwekwa na Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo, Dk Hamis Kigwangalla Oktoba 10, 2019. Lakini shughuli za ujenzi wake nazo zimesimama na eneo lipo katika hali mbaya.
I am the state. Kitabu kizuri cha kujifunza madhara halisi ya ukosefu wa utawala bora.
U4= 1. Uthubutu 2. Ushupavu 3. Ubinafsi 4. Ukabila
 
Back
Top Bottom