- Thread starter
- #41
Kumtetea Magufuli ni jambo gumu na linahitaji propaganda sana. Hatuhitaji kuwa mtaalamu wa uchumi kujua kuwa Magufuli alifanya ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma alifanya miradi mikubwa bila utafiti wa kutosha au ridhaa ya bunge. Miradi ya Chato ilikuwa ya kwake binafsi ipo mingi; uwanja wa ndege, mahoteli, mbuga ya wanyama, etc. Uthibitisho wa miradi hii kuwa ililazimishwa bila kufuata market demand, ni kwamba miradi hii yote imekufa! Hili sio tatizo la covid.Upotoshaji upotoshaji, Watanzania wana haki ya kupewa maelezo sahihi. Sehemu ya kwanza ya kuchumi kudorora kuna mambo 3 hayasemwi. La kwanza ni Covid-19 ya 2019/2020 hii inajibu kila kitu. Marehemu "Dikteta" alikataa kuifunga Nchi, hatukuumia kama walivyoumia almost dunia nzima. He was a Visionary, more so than Trump, or the EU, or WHO, dunia nzima. Na kuna sala tulifunga kwa kuongozwa na Mufti na Askofu Malasusa na Askofu Ruwaichi kwa pamoja, umoja huo haujawahi kuonekana hapa duniani.
Imetajwa benki ya CRDB sababu za kipuuzi tu. Maendeleo huletwa na uwepo wa benki, hasa kama ni za umma, siyo benki kupelekwa kwenye maendeleo tayari. Hili Dr Kimei analijua, na ndivyo alivyosema, Wahariri kwa wametumbukiza maneno yao mdomoni mwake kwa sababu zao.
Jiulize NBC: hii 1997 ilipobinafsishwa, matawi mazuri yaliyokuwa mijini yalinyofolewa wakapewa makaburu almost for free. NBC wakaitafuna, sasa angalia NBC iko wapi? Yale matawi ya hasara yemekaa kama Chatochato yalimegwa ikapewa NMB mpya, benki ya makabwela. Leo NMB ndiyo benki kubwa inayoongoza Tanzania, how do you explain that?
NBC ilikuwa iende DSE kama mashirika mengine TBL, TCC, TOL, nk, wanunue Watanzania, lakini hadi leo makaburu wamekataa kuipeleka DSE kwa makusudi kabisa, inatumiwa kama conduit ya hela zao tu.
Pia imetajwa benki moja eti "mbovu" - ya Twiga Bancorp. Hii si mbovu hata kidogo, it was the best bank in the NBC system kwa sababu ndiyo pekee iliyokuwa na forex wakati mgumu tulipokuwa Nchi haina hela za kigeni. Ilikuwa ichukukiwe na makaburu pamoja na NBC lakini ni Wazalendo hawa hawa kina Dr Kimei wakaona ukweli huu ikanyofolewa NBC haraka haraka kabla haijauzwa. Hilo nalo halisemwi, Magufuli wala hahusiki.
Benki zingine ikiwamo ya Wanawake ni za tangu zamani, na hizo zingine zililemewa na Covid, si za Magufuli.
Umetajwa pia mradi wa hoteli ya Burigi Chato, hii tatizo lake pekee lilikuwa Covid mapato ya Utalii kupungua, si ya Magufuli. Mbuga za wanyama magharibi ya Ziwa toka Kyerwa Ibanda hadi Rubondo na Chato ni nzuri mno, uamuzi wa kuzikwamua haukuwa wa Magufuli ni bahati mbaya tu ukakunbwa na Covid.
Huo "utafiti" wa Wahariri ni sawa na zero, sijui ni nani aliyewalipa kutunga hadithi hizo za kitoto.
Naomba wasomaji haya wayatafakari kabla hatujaja "utafiti" wa Chato kama Chato.
Magufuli alikuwa the wrong president aliharibu uhuru wa kujieleza, watu waliporwa mali zao kibabe, uchaguzi mkuu ulivurugwa vibaya kuwahi kutokea barani Afrika. watu wameumizwa na kuuwawa. Utamdanganya nani kwamba haya yote ni kwasababu ya covid? Magufuli was a catastrophe for our country!