CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Umesema USA wamelickdown lakini vifo vinaongezeka. Huoni kama umejibu swali lako mwenyewe kuwa lockdown aisaidii?
 
Utakwenda kwa NANI wakati Kila nchi imefunga mipaka yake
 

Attachments

  • IMG_20200409_001808.jpg
    99.2 KB · Views: 1
Unajua ni rahisi sana kutoa matamko kama haya ukiwa unadhani huu ugonjwa hauwezi kuchukua uhai wako na ukiwa bado hujaona matokeo hasi ya huu ugonjwa. Huko nje watu wanakufa 400 hadi 1000 kwa siku halafu tunachukulia mzaha. Je hatupendi uhai wetu? au akili zitarudi tukianza kufa? Na msidhani watakufa watu wengine hata nyie mpo kwenye hiyo hatihati ya kufa na huu ugonjwa.
 
Akilitime,
Mbona CHADEMA wamekuharibu akili kiasi hiki. Unadhani Corona ni kwa ajili ya CHADEMA TU. Pendekeza Suluhisho kwa ajili ya Tanzania na si eti kuwakomoa CHADEMA. Hii corona ni ya kwetu wote tuunganishe nguvu sio Swala la kutafutia Sifa.
 
Akilitime, Fuatilia S.A watu wanapinga kwa kuwa serikali haitoi chakula.
Usipozuia watu kutoka kisa wajitafutie ugali utapata maafa makubwa.
Maghala ya taifa hayana chakula?

Na ninyi mnaotoa misaada kwenda serikali hamjifunzi?
 
Chadema wameingiaje hapo? Ndio wanaosababisha uchumi wa nchi kuharibika vibaya ndani ya miaka mitano ya Magufuli? Ndio waliosababisha wakulima wa korosho wasilipwe? Wamesababisha biashara kufungwa? Wamesababisha kusiwe na ajira mpya miaka 5 wala kusiwe na nyongeza ya mishahara? Hizi ndio tabia za nyie na kutumia makalio kufikiri
 
Metaphor
 
Yan kagonjwa ka corona ninkadogo ? aisee hizi dhihaka za viongozi na uwongo kwa raia utawakost sana waunga juhudi na watatucost sisi pia daaah aisee, YAN ITALY WAMESHINDWA KWA DINI TUTAWEZA SISI ? sio kweli na TUSIDANGANYANE KABISA WAKUU


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna vichaa humu!!
Shule na vyuo vilifungwa tukiwa tuna kesi za ugonjwa kwa watu wanaoingia nchini. Leo Waziri wa Afya anatangaza kuanza kuwa na maambukizi ya ndani (wenyewe kwa wenyewe), bwege mmoja anataka shule na vyuo vifungue!!!
 
Mask siyo kama khanga mkuu. Zina utaalam wake. Ingekuwa ni kitambaa hata leso ingefaa.

Muhimu hapa ni kuwa tuna nchi zinatutegemea. Sisi tuchape kazi tu ili nao wenzetu wasije wakapata madhara.

..mask ya kitambaa au leso ni afadhali kuliko kuji-expose.

..tuchukue tahadhari zote ambazo tunaweza kuzichukua kulingana na mazingira yetu.

..essential transit goods ziruhusiwe mipakani kama huduma kwa majirani zetu, na safari zisizo za lazima zisiruhusiwe.
 
Natumai kiongozi katoa mwongozo inabidi tuufuate, hajakurupa yupo makini na majukumu yake kwetu.
 
Tazama picha kwa makini sana,huyu ni kiongozi mkuu wa nchi,kazi picha macho.
 
Umesema USA wamelickdown lakini vifo vinaongezeka. Huoni kama umejibu swali lako mwenyewe kuwa lockdown aisaidii?
Nlitaka nikuchunie ila ngoja nikujibu.
Trump haku take action mapema alikua akisema we will b fine. We are doing good. It's Chinese virus. ....na kila aina ya BS.
Wakati anayasema haya watu wakaendelea kuambukizwa mmoja baada ya mwingine. Kuja kushtukia the shit has has hit fan already. Lockdown. Too late. Very late. Na lockdown ilikua ya kishkaji. Beaches zilikua zinafurika balaa. Kirusi hakikuwaacha. Sasa ikaja total lockdown. Extremely late. Hivyo hawa wanaokufa ndio walee waliokua locked down wakati it was already late. Ndio hao wanakufa sasa. Kwa nini wanaongezeka kila siku? Sababu watu wako locked down na maambukizi tayar hivyo wanazidi kuambukizana tu. Health system imekua overwhelmed. Total chaos.
Tanzania kwa sasa tuko pazuri. Kama tungefumba macho tukapiga lockdown hata ya mwezi mmoja tu tutakua tumecheza safi sana. Tukisubir maambukizi shazi ndio hayo ya wamarekani yatatukuta.
 
Anakumbuka shuka kumekucha!

Hivi siku zote alikuwa wapi? Au leo alitaka tu auze sura kwenye TV? Kauli yake aliyoitoa leo inatusaidia nini?

Bora tu angejinyamazia kimya huko alikokimbilia.
 
Mzeebaba yupo sawa kabisa, tuna matatizo mengine yanahitaji more attention kuliko hayo mafua ya mizungu. Kufunga mipaka sio suluhisho.
 
Kwanini aligoma kufunga tangu mwanzoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakukua na haja hiyo, huwezi funga mipaka ya nchi hujaanalyze tatizo vizuri kujua effect yake itakuaje, ni obvious mipaka ikifungwa nchi itakua kwenye wakati mgumu sana kiuchumi na ugonjwa wenyewe hata bado ilikua haijulikani kama utasurvive kwenye mazingira kama ya Tanzania ambayo climate ni tofauti.
 
Kumbe upo pazuri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi hua nasifia panapo sifiwa na napondea panapopondewa sina upendeleo. Kwa hili Magu kafanya la maana sana. Nchi kama Italy zilikua za kwanza kufunga mipaka leo hii wanaongoza kwa vifo. Kufunga mipaka sio solution maana watanzania watarudi tu huwezi fungia wananchi wako wasirudi sanasana utafukuza wageni peke yake ila watanzania watakaorudi nyumbani watauleta
 
Mkuu kwani majirani wakifunga mipaka na sisi Tanzania hatujafunga mipaka ni faida gani tutapata?
Angalau sio sisi tuliofunga ni wao, hapo tayari tuna kadi moja ya kucheza wakitusumbua au tukitaka kitu toka kwao huko mbeleni tunaitumia tunawapiga mkwara na sisi wa kuwafungia mipaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…