Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili wazo lako la kukaa mbalimbali litasababisha madhara. Kumbuka kuna nchi 8 zinatutegemea. 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂Mpelelezi J. Hata Usa ni law enforcement agencies ndio wanasimamia haya. Nimeona wanaweka hadi cones kama alama ili mtu asimame hapo ili awe mbali na mwingine kama anakata ticket au la. Na sisi tuige hao waliofanikiwa. Na kama ikiwezekana ifanyike mapema.
Sasa utapata wapi pesa za kununua hizo mask. Kaendelee kuchapa kazi achana na mambo ya kuvaa maski. Chapa kazi kuna nchi zinatutegemea...pia watu wote walazimishwe kavaa face mask, vitambaa, kukinga pua na mdomo.
..hatua yoyote ya tahadhari ambayo iko ndani ya UWEZO wetu tusiache kuichukua.
Kuna mstari mwembamba unaotenganisha ushujaa na ujinga, huwezi kumwona simba mwenye njaa amelala ukaenda kuminya kengele zakeHii nchi hatupo seriaz saiv tunapeana kauli za kishujaa
Yakifika kama ya Italy na Spain tutaanza kuuza kesi kwa Mabeberu na wapinzani
View attachment 1415673
Amesisitiza kuwa Serikali imeamua kutowazuia Watu ndani ya nyumba zao wala kufunga mipaka kwa kutambua madhara mkubwa yanayoweza kutokeza kwa kufanya hivyo.
Aidha, amesema madhara hayo yanaweza pia kuziathiri nchi 8 ambazo zinatengemea kupata huduma na bidhaa kupitia Tanzania hususan bandari ya Dar es Salaam.
Lakini pia amebainisha kuwa kutokana na madhara ya #CoronaVirus upo uwezekano mkubwa wa kutokea kwa upungufu wa chakula, hivyo amewataka Wananchi kuzalisha chakula cha kutosha.
Pia, amesisitiza Wananchi waendelee kuchapa kazi kila mahali walipo huku wakichukua tahadhari ya kutokuambukizwa kwa kufuata ushauri wa Wataalamu na pia wasisahau kumuomba Mungu atuepushe na janga hili
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Waumini wa Kanisa Katoliki katika Parokia ya Mlimani, Wilayani Chato mkoani Geita ambapo alihudhuria ibada ya Ijumaa Kuu.
View attachment 1415488View attachment 1415489
Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita leo. Picha na Ikulu
Sasa utapata wapi pesa za kununua hizo mask. Kaendelee kuchapa kazi achana na mambo ya kuvaa maski. Chapa kazi kuna nchi zinatutegemea.
Mask siyo kama khanga mkuu. Zina utaalam wake. Ingekuwa ni kitambaa hata leso ingefaa...tuwe wabunifu.
..tunaweza kutengeneza za vitambaa.
..tufanye yaliyoko ndani ya uwezo wetu.
..pia tusitoe kauli za kupuuzia ugonjwa huu, kwani ni hatari.
..kwa mfano nimemsikia Raisi akasime Covid19 ni " kaugonjwa ". Nadhani siyo sahihi kusema hivyo.
Kwani Corona ni politics au ni science?
InsanityIulize Corona itakujibu
Hata mimi nashangaa watu wanalalamika kuwa kwa nini hakuna lockdown. Hivi si wakae nyumbani? Tumeambiwa tufate taratibu za kujikinga ambazo zinajulikana watu hawafati wanataka kulazimishwa. Watanzania Sisi ni watu wa ajabu sanaSalaaaam.....
Iv tunavolalamika mipaka aifungwi mara cjui rais ajasema lockdown...kwan sisi wenyewe atuwezi kujua kipi kizuri kipi kibaya.. kama cha msingi ni lockdown tukiamua watu wote ni lock down na tukakaa ndani kwani serikali itatulazimisha tutoke njee....au ndo mpaka kila kitu tupewe amri......
ila yote na yote hakunaga kaburi la mtu muoga.....pia ikifika siku yako ya kufa lazima utakufa tu.....salaaam
Acheni upumbav* fuateni utaratibu wa kujikinga sio lazima mfungiwe ndaniJamaaa anakera natamani corona imfuate huko huko alipo imchukue imtafune hvi ni mwanadamu kweli huyu au jinamizi tumeletewa
Mura unataka kusema hujui njia za kujikinga na huu ugonjwa?Kwa hili la kufunga nakuunga mkono kwa asilimia 100 japo tumechelewa lakini athari zinaweza kupungua kuliko hii njia tunayoitumia. Wataalamu wa afya wangeruhusiwa kutueleza hatua sahihi za kujikinga na ugonjwa huu badala kuamuliwa na wanasiasa. Tujiulize swali dogo Watanzania kule Makao Makuu ya Kabisa Katoliki ibada ilivyoendeshwa bila Misongamano kabisa kwa nin?