Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Olmost

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
337
Reaction score
441
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania

---------
Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
 
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania‬

___
Mipango ipo mbioni kukamilika,
Tunamshukuru Mungu Kupata Rais Mzalendo, anayeanza kupaendeleza Chato, baadae itafuata Mikoa Mengine
 
Back
Top Bottom