Chato wamshukuru Rais Samia kwa kuwapa Tsh 3.24 bilioni walizojengea Shule 13 Mpya, Madarasa 188 na Matundu ya Choo ya kutosha

Chato wamshukuru Rais Samia kwa kuwapa Tsh 3.24 bilioni walizojengea Shule 13 Mpya, Madarasa 188 na Matundu ya Choo ya kutosha

Kuna ubaya kwasababu hiyo hela italipwa na Tanganyika sio Zanzibar sababu hawana bajeti ya kulipa mikopo.
Hakuna kitu kinaitwa Tanganyika.

Hiyo ni historia.

Kuna nchi kamili ya Zanzibar.

Kisha kuna Jamhuru ya Muungano wa Tanzania
 
Hakuna kitu huwa nahuzunika kukisikia, kwamba hadi matundu ya choo kujengwa kwa msaada...

Yaani kwamba mtu umekuwa masikini hadi huoni umuhimu wa kuwa na choo au?

Dah!!!
 
Nchi ina mikoa 31 fedha ya mkopo ni 1.3 trillion. Mgawanyo sahii ilikuwa kila mkoa upate 40+ billion. Zanzibar wamechukua fedha za mikoa 5 ikiwa idadi yao ya watu na eneo haizidi hata wilaya ya Ikungi.

Hao wanaoshukuru ni kuwa hawajui hesabu.
Tangu lini wana ccm wakijitambua na kudai haki yao?

Wao kila siku maishani mwao ni tunashukuru tunashukuru utadhania wanapewa kwa hisani wakati ni haki yao.
 
Kama ni hivyo Tabora ilitakiwa ipewe nyingi zaidi, kwanini iwe Chato na si Sumbawanga, Kigoma, Shinyanga ama Mtwara ?
Tuache unafiki pakijengwa popote pajengwe tu ni Tanzania

Kama inakuwa tabu sana basi tuwaachie waZanzibari Nchi yao kwanini tunawang'ang'ania au ndio yale maneno ya mh Mnyaluko ?
Lukuvi alikuwa sahihi sana ila sema kwa tabia za wana ccm leo hio wanamuona kuwa alikosea kusema ukweli.
 
Zanzibar ni mkoa uliopewa hadhi ya kuwa wizara inayojitegemea ndio maana Rais wake akija kwenye baraza la mawaziri anakuwa mjumbe wa kawaida hana tofauti na Waziri wa mazingira ndani ya vikao vya baraza la mawaziri.
Mkuu nakushauri wacha kupoteza nguvu zako kwa kujibu utumbo wa huyu mtu.
 
Hii lugha ya kumshukuru
Samia badala ya serikali inaukakasi sana!
Fedha ametoa samia au serikali?
 
Wakazi wa wilaya ya Chato wamemshukuru sana Rais Samia kwa kuwapatia jumla ya tsh 3.24 bilioni walizotumia kujenga Shule mpya 13 za sekondari, Madarasa 188 na Matundu ya Choo ya kutosha.

Mbunge wa jimbo la Chato mh Kalemani amesema hiyo haijawahi kutokea tangu kuasisiwa kwa Wilaya hiyo na kwamba Wanamuunga mkono Rais Samia kwa 100%

Source: Star TV habari

92EA6789-3406-4FA9-9D61-D66047A9A422.jpeg
 
Hii lugha ya kumshukuru
Samia badala ya serikali inaukakasi sana!
Fedha ametoa samia au serikali?

Kwenye matumizi huwa inatajwa zimetoka kwake...

Lakini thubutu kutaja alikozitoa kwamba ni hisani ya mabeberu 😁 au kodi za wananchi...
 
Back
Top Bottom