Magari ya kukodisha
JF-Expert Member
- Sep 16, 2019
- 412
- 695
Chatoville avenue
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chato haiwezi kukua,bora yeye angejikita kuwajengea shule na kuwatafutia kazi za upendeleo zile nono kama huko TRA na bandarini,ila hayo madude ya majengo atafurahi mwenyewe akitoka madarakani yatakavyochakaa,hawaamini,jamaa huyu akili zakeVitu vyote hivyo vingeweka ( kujengwa ) kahama .Kahama ingewini sana
Chato Mzee ndio anaikuza aseh
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimecheka kama mjinga...umenikumbusha mbali sana,sijui hii kitu iliishia wapi... dah! Umenikumbusha MATEMBEZI YA MSHIKAMANO! Sijui hii kitu iliishiaga wapi.
Chato inaenda kuwa mkoa wa Rubondo, na chato itakuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Rubondo, so hiyo economic and social infrastructure itabaki kuwa relevant hata akiondoka. Sababu mkoa ni tofauti na kijijiChato haiwezi kukua,bora yeye angejikita kuwajengea shule na kuwatafutia kazi za upendeleo zile nono kama huko TRA na bandarini,ila hayo madude ya majengo atafurahi mwenyewe akitoka madarakani yatakavyochakaa,hawaamini,jamaa huyu akili zake
Hata akifanya mkoa,kwanza atakuwa ni mpuuzi,na pili Chato hapataweza kuendelea,angesomesha watu na kuwawezesha kiuchumi kwanza,pale watu wana umaskini wa kutisha,na nimiongoni mwa maeneo yanayosababisha watu wa kaskazini watucheke sisi watu wa kanda ya Ziwa,upuuzi mkubwa kabisa,Chato inaenda kuwa mkoa wa Rubondo, na chato itakuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Rubondo, so hiyo economic and social infrastructure itabaki kuwa relevant hata akiondoka. Sababu mkoa ni tofauti na kijiji
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.
“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.
Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita
Kwani Mloganzila iko Singida auWacha Nyerere aitwe baba wa Taifa.
Ingawa nahisi watu wa 'Butihama' karibuni wataanza kumlaumu kwa kutotumia fursa.
Mzee Mwinyi na Kikwete mlikwama wapi mbona Mkoa wa Pwani haukupata mavitu makubwa haraka?
Hadi leo hakuna mataa ya kuongozea magari kama 'Chattle'
Pataachaje kuendelea pakiwa mkoa? Hivi ushawahi fika Bariadi kabla na baada ya kuwa mkoa? Kama ushawahi fika Bariadi nenda sasa hivi ukaone maendeleo ya paleHata akifanya mkoa,kwanza atakuwa ni mpuuzi,na pili Chato hapataweza kuendelea,angesomesha watu na kuwawezesha kiuchumi kwanza,pale watu wana umaskini wa kutisha,na nimiongoni mwa maeneo yanayosababisha watu wa kaskazini watucheke sisi watu wa kanda ya Ziwa,upuuzi mkubwa kabisa,
Hospitali ya rufaa, tena ya serikali inajengwa wilayani! Yaani mji wa Chato? Chato kunani?Hakuna cha ubaba! Taifa umaskini chanzo ni yeye. Magufuli ndiyo ananyoosha hii sasa.
Pwani ipi? Au hujui viwanda takribani 73 vimejengwa enzi za Kikwete?! Mloganzila kwanini haikupelekwa Iringa?!
Tuwe wakweli zama za Umwinyi na Umangi kwisha habari yake. U-Daslam utapotea ili taifa lisonge.
Haiwezekani mtu Kigoma na Kagera yupo mahtuti mpaka afike Daslam kwa tiba! Haiwezekani, Daslam ni kipande kidogo sana kwa Tanzania.
Maendeleo endelevu ya Tanzania
Tunasubiri Zitto awe mkulu tupatePembezoni ipi unayoisemea?! Daslam?, Zama hizo zimeisha.
Kwa takribani miaka 60 sasa wakazi wa Kigoma na Kagera wamekuwa wakifuata huduma za kijamii Daslam, Elimu ya juu, Hospitali, Usafiri wa Kimataifa na mengineyo. Haiwezekani hii lazima ifike ukomo kwa maendeleo ya taifa hili! U-Daslam lazima ufe.
Huyu babu yetu mbona mnamsingizia sana. Kwani alifanya nini cha ajabu kule Mwanga hata kila siku mnamfanyia rejea?Wenzie wanatumia hii formula ya Msuya enzi za uwaziri mkuu.
Kijiografia Chato ni katikati ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Kagera na Simuyu.