Kubishana na wewe ni 'futile worth no effort' sababu hakutakuwa na muafaka.
Kama hauoni yaliyo fanywa na Nyerere basi sina namna ya kukufanya uyaone.
Kama ndege ziliuzwa, mashirika yaliuzwa, viwanda viliuzwa, nyumba ziliuzwa.
Reli ya TAZARA ipo, meli bado zilikufa au kuzama wakati ameshaondoka, vyuo vipo, shule zipo.
Hizo huduma za kijamii zilizokuwa zinatolewa wakati wa Nyerere huwezi kuzitunza kama kitu tangible, sijui ulitaka tukutunzie vipi uzuone.
Kwa kifupi nenda kawaulize wakubwa wako au kama ungekuwa karibu na Mh. Magufuli tafuta siku akiwa na nafasi japo dakika 2 muulize mambo ya Nyerere wakati yeye anasoma, muulize mzee unajipimaje na yule mzee muadilifu na mchapa kazi mwenzio?
Kama sio mnafiki, na mimi nina uhakika, nina imani nae atakuwa mkweli atakuambia yeye anafikia wapi kwenye kipimo cha utendaji na uzalendo wa Nyerere, achana na uadilifu.
Unachekesha unapojaribu kumponda sera za Nyerere kwamba ndizo zilizo tufanya tuwe maskini huku ukimsifia Magufuli ndio anatupeleka njia sahihi wakati anachofanya Magufuli ni kujaribu kuiga karibu kila kitu cha Nyerere.
Kuanzia sera na misimamo japo bado hajafikia level ya Nyerere.
Inaonesha hata hujui nini hasa anachokifanya Magufuli na nini alichofanya Nyerere. Haujui hata ideology ipi watu hawa wawili waliifuata au huyu anaifuata sasa.
Humjui kiitikadi mtu hata unaemshangilia na kumsifia.
Hizo document hazina chochote cha ajabu, na hazitakusaidi wewe wala Tanzania kuleta maendeleo yako binafsi na ya nchi yetu. Yamejaa propaganda za kimagharibi ambazo huyu Mwamba Magufuli anazijua na kuzipiga na Nyerere alikabiliana nazo hadi siku anakata kauli.