Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

yah..... na mimi nimei bold hapa chini!

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
Nashangaa wabunge hawajui kuwa hospitals zote za mikoa zine hadhi ya rufaa walichokuwa wanacheka mini kama siyo unafiki. Hospitals zote za mkoa ikiwemo Chato ndani ya Geita ni za rufaa. Fanyeni ufuatiliaji kuliko kuchekacheka
 
Watanzania tutulie kila jambo na wakatib wake.
JKN alijenga airport Musoma. Sasa hivi hamna ndege inaenda Musoma.

JK alijenga mloganzira, barabara ya bagamoyo; na maisha yalisonga.

Sumaye akiwa PM alilazimisha kujenga airport Arusha wakati KIA iko so close.

Mwandosya akiwa waziri wa Uchukuzi na mawasiliano enzi za Mkapa ali-miss alloate funds na kujenga airport ya Songwe. It took more that 8years tokea ujenzi kuisha ndege kuanza kutua.

Waziri Mramba wakati mmoja akasema hata tukila nyasi; sio tabu lazima kununua Presidential Private Jet.

Ukumbi wa Bunge ulijengwa right away wakati Mkapa anatoka JK anaingia. Thamani za ukumbi ule ulikuwa bora kuliko hata ukumbi wa Marekani au Uingereza.

Wanasiasa wetu ndo walivyo. Usilalamike..wewe shukuru Mungu maama hata ukilalamika huwa wanafanya yale ambayo wanadhani yanagusa malengo yao ya kisiasa.

Bila shaka kwa Population ya 15 Mil Lakezone na Bugando ina capacity ya viwanda chini ya 1200. Sio vibaya kujenga Chattle Zonal Referal Hospital. Then siku mzee anastaafu; Watanzania wanahukumu kati ya aliejenga another referral hospital to serve 15mil population vs wanunua ndege ili tule nyasi au walojenga Songwe na 8 years baadae ndo jet ya kwanza ikaanza operations.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa wabunge hawajui kuwa hospitals zote za mikoa zine hadhi ya rufaa walichokuwa wanacheka mini kama siyo unafiki. Hospitals zote za mkoa ikiwemo Chato ndani ya Geita ni za rufaa. Fanyeni ufuatiliaji kuliko kuchekacheka
....kwa hiyo Chato ndiyo makao makuu ya mkoa wa Geita siyo?
 
Tabora wanaiota Toronto Chato inageuzwa Seattle... Maendeleo hayana chama ila yana "kiongozi atokako". Cha ajabu ni akimaliza muda wake ndipo vijiongozi vitajitokeza kusema siosawa lkn kwasasa vitaunga mkono mia kwa mia!! Kiongozi mnafiki nimwiba kwa waongozwao...
 
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
Wanacheka nini hawa wapumbavu badala ya kukemea huo ujinga? Kwa nini iwe Chato na siyo Geita? Kama tunatafuta katikati basi inapaswa ijengwe Mwanza jiji au Sengerema!
 
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.

Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita
Magufuli anajenga miundo mbinu ya serikali na si ya kwake binafsi.Hata akiondoka hospitali itahudumia watu,kiwanja cha ndege kitasaidia wengi.Hongera kwa hilo!!
 
Nyerere angekuwa na akili kama za huyu mzee, basi ikulu ingejengwa butiama, tena ukizingatia uhuru alienda kudai yeye mwenyewe kwa mguu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.

Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita

Tuliambiwa na wengine hapa watu wa huko hawana upendeleo kabisa. Kwanini iwekezaji umeanza awamu hii 😂😂 Watanzania si wajinga. Hospital ijegwe hivi shinyanga masikini ndiyo kuna watu wengi lakini hata huko kuna kupendeleana.
 
Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.

“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.

Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.

Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.

Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita
Kama Baba wa Taifa na marais wengine waliomfuatia wangalikuwa na tabia hizi za kichoyo, kukosa aibu na upendeleo wa wazi wa maendeleo ya vitu, huku waliowazunguka wakishindana kupeleka kwa kasi maendeleo ya vitu ktk maeneo waliyotoka, sijui taifa letu leo lingalikuwa ni la namna gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yote unayotanabaisha hapa mbona ameyapokea baada ya kuwafukuza British? tokea hapo mbona hamna yaliyoongezeka?!.

Hivi vitu vya ubaba na umama ni siasa tu! Nina documents za Germany East Africa (Deutschland) na British Territory ambazo hata Jamhuri haina na haitokuwa nazo.

Narudia nina documents za Germany na British zenye ukweli wa yote ambazo hata Jamhuri haina.

Ukitaka kupiga maendeleo Tanzania hii kwanza ukatae ubaba na hivyo ndivyo Magufuli alipofanikisha na watu wanastaajabu.

"Kama walikuwa wanafanya, mbona hayaonekani?!." - John Pombe Magufuli
Kubishana na wewe ni 'futile worth no effort' sababu hakutakuwa na muafaka.
Kama hauoni yaliyo fanywa na Nyerere basi sina namna ya kukufanya uyaone.
Kama ndege ziliuzwa, mashirika yaliuzwa, viwanda viliuzwa, nyumba ziliuzwa.
Reli ya TAZARA ipo, meli bado zilikufa au kuzama wakati ameshaondoka, vyuo vipo, shule zipo.

Hizo huduma za kijamii zilizokuwa zinatolewa wakati wa Nyerere huwezi kuzitunza kama kitu tangible, sijui ulitaka tukutunzie vipi uzuone.
Kwa kifupi nenda kawaulize wakubwa wako au kama ungekuwa karibu na Mh. Magufuli tafuta siku akiwa na nafasi japo dakika 2 muulize mambo ya Nyerere wakati yeye anasoma, muulize mzee unajipimaje na yule mzee muadilifu na mchapa kazi mwenzio?

Kama sio mnafiki, na mimi nina uhakika, nina imani nae atakuwa mkweli atakuambia yeye anafikia wapi kwenye kipimo cha utendaji na uzalendo wa Nyerere, achana na uadilifu.

Unachekesha unapojaribu kumponda sera za Nyerere kwamba ndizo zilizo tufanya tuwe maskini huku ukimsifia Magufuli ndio anatupeleka njia sahihi wakati anachofanya Magufuli ni kujaribu kuiga karibu kila kitu cha Nyerere.
Kuanzia sera na misimamo japo bado hajafikia level ya Nyerere.
Inaonesha hata hujui nini hasa anachokifanya Magufuli na nini alichofanya Nyerere. Haujui hata ideology ipi watu hawa wawili waliifuata au huyu anaifuata sasa.

Humjui kiitikadi mtu hata unaemshangilia na kumsifia.
Hizo document hazina chochote cha ajabu, na hazitakusaidi wewe wala Tanzania kuleta maendeleo yako binafsi na ya nchi yetu. Yamejaa propaganda za kimagharibi ambazo huyu Mwamba Magufuli anazijua na kuzipiga na Nyerere alikabiliana nazo hadi siku anakata kauli.
 
Back
Top Bottom