Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Acha ijengwe tu kwani Chato iko Burundi?
Mobutu seseko mwingine huyo!
1.Mbuga chato
2.Bandari chato
3.Airport chato
4.Jengo la kisasa TRA chato
5.CRDB walilazimishwa kufungua tawi chato
6.Hospitali ya rufaa chato
7.Mataa ya kuongozea magari chato
8.Meli mpya chato
Chato ni wakati wenu sasa kuneemeka na utawala huu wa JPM!
 
Alisikika mlevi mmoja Kwanini makao makuu ya nchi yasipelekwe Chattle ili kuboresha utendaji kazi hata bandari ya Dsm hamishiwe Kama Kuna uwezekano pia mlima Kilimanjaro uhamishiwe huko ili kukuza utalii na biashara vipi kuhusu Chuo kikuu kujengwa Chattle
 
Hakuna cha ubaba! Taifa umaskini chanzo ni yeye. Magufuli ndiyo ananyoosha hii sasa.

Pwani ipi? Au hujui viwanda takribani 73 vimejengwa enzi za Kikwete?! Mloganzila kwanini haikupelekwa Iringa?!

Tuwe wakweli zama za Umwinyi na Umangi kwisha habari yake. U-Daslam utapotea ili taifa lisonge.

Haiwezekani mtu Kigoma na Kagera yupo mahtuti mpaka afike Daslam kwa tiba! Haiwezekani, Daslam ni kipande kidogo sana kwa Tanzania.

Maendeleo endelevu ya Tanzania
Kwanini hiyo hospitali isingejengwa kigoma ili ihudumie mikoa ya Rukwa,Kagera na Kigoma yenyewe?Chato kwenda bugando ni karibu,watu wa kigoma mpaka waende Mwanza na usafiri ni majanga!
 
Pembezoni ipi unayoisemea?! Daslam?, Zama hizo zimeisha.

Kwa takribani miaka 60 sasa wakazi wa Kigoma na Kagera wamekuwa wakifuata huduma za kijamii Daslam, Elimu ya juu, Hospitali, Usafiri wa Kimataifa na mengineyo. Haiwezekani hii lazima ifike ukomo kwa maendeleo ya taifa hili! U-Daslam lazima ufe.
we jamaa una mawazo ya kishetani kabisa, utalegea tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali imesema ina dhamiria kujenga hospital ya kanda ya Ziwa huko Chato mkoani Geita

Waziri wa Afya jinsia na watoto amebainisha hilo leo

My take: kwa nini ijengwe Chato na si Mwanza kitovu cha kanda ya Ziwa au Geita makao makuu ya mkoa?

Source Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Bugando iko wapi mkuu!! Au hapo hapo Mwanza zijengwe hosp 2 za rufaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi imejamba hii.
Rukwa, Kagera na Kigoma wanahitaji sana hiyo hospitali ya Rufaa kuliko Chato iliokaribu na Bugando hosptali.
Tumekwama kwa kweli sio ya kuchekea haya.
 
Wamejitokeza kutumia fursa baada ya kumsoma Magu,wanaona mamiradi yanaelekezwa huko,kwanini wasitumie fursa?Kigoma,Kagera,Rukwa hakuna hospitali yenye hadhi ya rufaa!Wagonjwa Wote hukimbilia Bugando Mwanza,hii ni wazi JPM ameamua kuwa Mobutu Seseko!
Kitaalamu inaitwa bureaucratic competition!!
 
... huko Kanda ya Kusini na Kanda ya Magharibi mko wangapi? Hamjazi hata kibaba ninyi! Hoja ya Waziri Ummy ni kwamba Kanda ya Ziwa wako wengi! Hata Prof. Kabudi aliwahi kulisemea hili nadhani kwenye Sherehe za Uhuru Mwanza (2019). Mtakapokuwa "wengi" mtajengewa! Ha ha ha.
Ndo maana safari hii membe twende naye, nyie mmekula imetosha, vyeo vyote vikubwa mmepeana wenyewe.
 
Hii si sawa, kanda ya ziwa hospitali za rufaa mbili, kanda ya kusini hakuna, kanda ya magharibi hakuna. mmhh ukabila/ ukanda unapanda chati, umoja mshikamano utaporomoka tusipojisahihisha
Hii nadhani inaweza kuligawa taifa
 
Aaah Tanzania ya viwanda....😂😂😂😂😂😂😂😂😂na mie pia nimecheka ingawa siyo mjumbe wa kamati...



Everyday is Saturday............😎
 
Back
Top Bottom