luambo makiadi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2017
- 10,602
- 8,798
Hahaha naamWajenge tu huko chato mana huku kwetu kaskazin tulishamaliza kitambo labda waje kupaka rangi tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha naamWajenge tu huko chato mana huku kwetu kaskazin tulishamaliza kitambo labda waje kupaka rangi tu
Wacha weeeee !!Serikali ya Tanzania itajenga Hospitali ya Rufaa wilayani Chato Mkoa wa Geita.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii leo Jumatatu Januari 20, 2020, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali inatarajia kujenga hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu kuwa eneo hilo.
“Tumefanya utafiti na kugundua kuna wagonjwa wengi Kanda ya Ziwa kwa hiyo tunajenga Zonal Hospital (hospitali ya Kanda) Chato,” amesema.
Amesema kuwa sababu ya kujenga hospitali hiyo Chato ni Mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na watu zaidi milioni 15.
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
Baadaye wajumbe wa kamati hiyo watapata fursa ya kuichangia na kama kutakuwa na maswali, mapendekezo watayatoa.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita
Kila mradi unaoenda chato mnakuja na kauli hii hii,hamuoni sasa ni too much?Yaani kutoka chato hadi bugando ni umbali mfupi,angalia mikoa kama kigoma,rukwa na kagera,yote hii haina hospitali ya hadhi hiyo!Nenda huko Lindi,mtwara,Songea,Iringa,Mbeya,Ruvuma na kwingineko!Kwani Chato si ni Tanzania? Au chato hiko Rwanda? Hiyo hospital itatibu watu gani zaidi yakutibu watanzania? Sasa hole wake mtu acheleweshe mradi huo!!!
Pia Rukwa,kigoma na Kagera tunategemea Bugando!Huu sio mgawanyo ulio wa haki wa rasilimali za nchi yetu!Lindi, Mtwara, Ruvuma, kuna hospitali ya aina hiyo?
Tukichukulia kwamba huyu anaweza kukaa madarakani miaka zaidi ya ishirini, Chato itakuwa na picha gani baada ya muda huo kama kasi ndio hii!
Mwanza kuna Bugando mkuuSerikali imesema ina dhamiria kujenga hospital ya kanda ya Ziwa huko Chato mkoani Geita
Waziri wa Afya jinsia na watoto amebainisha hilo leo
My take: kwa nini ijengwe Chato na si Mwanza kitovu cha kanda ya Ziwa au Geita makao makuu ya mkoa?
Source Mwananchi
Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani tunaomba picha ya hiyo hospitalHospital inakaribia kukabiziwa ishajengwa kitambo afu leo wanatwambia eti wanatarajia kujenga ,,,,,,,,,,,,,kiufupi hospital ishamalizika kujengwa kilocho baki ni kuizindua tu mwanzo ilikuwa hospital ya rufaa wakabidil ikawa hospital ya kanda
( Chanzo ; mkazi wa chato)
Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa watawala wamechanganyikiwa,ndiyo maana yule mwingine alisema Kanda ya Ziwa inaweza kutosheleza kura za urais na kanda zingine ni kujazia jazia tu.Hilo ni pamoja na zaeni tutawasomesha bure.Unaganisha...Serikali imesema ina dhamiria kujenga hospital ya kanda ya Ziwa huko Chato mkoani Geita
Waziri wa Afya jinsia na watoto amebainisha hilo leo
My take: kwa nini ijengwe Chato na si Mwanza kitovu cha kanda ya Ziwa au Geita makao makuu ya mkoa?
Source Mwananchi
Sent using Jamii Forums mobile app
Wengi wenu ni wagonjwa?Sawa wajenge kabla ya 2020,ila msisahau kuwa tunaweka kumbukumbu vizuri.Tusije kutafutana uchawi.Watujengee haraka sana maana bugando imeelemewa mno
Umerasimishwa kisheria?Ni halali kufanya hivyo?Sasa hivi tuna kamsemo "Kila Rais na ajenge kwao"
Kasome vizuri fasihi utaelewa nilichoandikaWengi wenu ni wagonjwa?Sawa wajenge kabla ya 2020,ila msisahau kuwa tunaweka kumbukumbu vizuri.Tusije kutafutana uchawi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wamekuunganishia uziView attachment 1328631
Leo waziri wa afya mheshimiwa Ummy Mwalimu alisikika akisema kuwa serikali inatarajia kujenga hospitali ya rufaa wilayani Chato na eti swala hilo bado linajadiliwa.
Cha kushangaza ni kuwa kumbe mradi huu tayari umeanza. Mimi swala la mradi huu halinihusu.
Kinachonihusu mimi kama mdau wa maendeleo ni jinsi ambavyo serikali imekuwa ikitekeleza miradi kama hii kienyeji. (Serikali hii ya awamu ya tano)
Ni masikitiko kuwa siku hizi serikali inajiamulia tu kufanya mambo pasipo kufuata sheria ikiwemo kuweka uwanja wa ushindani wa miradi.
Mambo kama haya mwisho wa siku hupelekea Rais kuamua hata kuingiza jeshi ilimradi matakwa yake anayotaka yatimie. Kazi haziendi hivyo. Kinachoonekana hapo zote ni taasisi za serikali. Ushindani uko wapi? Nini maana ya ushindani?
Kwa kweli mambo haya yakiachwa na kufumbiwa macho tutazalisha miradi ya hovyo na hapatakuwa na wakuhoji maana ni kama serikali inajijengea na kujisimamia. Haya kwakweli yanaudhi na kuzalisha kazi za chini ya viwango.
Tuchukue tahadhari na hatua thabiti isitokee,vinginevyo TUMEKWISHA!!!Na bado. Tukiingia muhula wa pili, hakuna rangi tutaacha kuona kuhusu "kupeleka" maendeleo kule. Vitafanyika hata vile ambavyo huwezi kutarajia vifanyike kule.