Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Nashangaa wabunge hawajui kuwa hospitals zote za mikoa zine hadhi ya rufaa walichokuwa wanacheka mini kama siyo unafiki. Hospitals zote za mkoa ikiwemo Chato ndani ya Geita ni za rufaa. Fanyeni ufuatiliaji kuliko kuchekacheka
Chato imekuwa mkoa lini wewe Lumaga? Kwa nini wasijenge kwanza Katavi, Njombe au Songwe? Hiyo ndio mikoa mipya, nchi yako mwenyewe, lkn huijui.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Mloganzila iko Singida au

Sent using Jamii Forums mobile app
Usitake tuanze kutaja vyote vilivyojengwa Chattle kwa muda wa miaka chini ya sita kisha tulinganishe na miaka 10 ya JK mwenyeji wa Msoga Bagamoyo/Chalinze Pwani, na miaka 10 ya Mwinyi Mkuranga Pwani.

Usituletee kichekesho kama alicho leta mwenzio nikamyamazia kama sijaona cha kuhesabu na viwanda vilivyojengwa Pwani na wawekezaji binafsi kwa fedha zao huku hivyo vya Chattle vikijengwa na serikali.

Sina chuki na mpambanaji wangu Mh. Magufuli, I wish asome comment zangu zote aone ninavyo mtetea na kumkubali lakini pia aone na hizi nilizo kosoa watendaji wake kufanya yaliyofanyika kwao, sina hakika kama yana baraka zake au maagizo yake.

Huenda ni kujipendekeza tu kwa watendaji walio chini yake kwa boss wao. Kama ni maagizo yake basi namuomba aangalie ushauri wetu.
 
Pataachaje kuendelea pakiwa mkoa? Hivi ushawahi fika Bariadi kabla na baada ya kuwa mkoa? Kama ushawahi fika Bariadi nenda sasa hivi ukaone maendeleo ya pale
Wasukuma wa Bariadi uwezi linganisha na wasumbwa,wasubi na wasukuma wa Chato,Bariadi ndo inawasukuma wajanja na weupeπŸ˜‚πŸ˜‚,nafikiri nikisema wasukuma weupe unajua namaanisha wana ng'ombe wengi,pili ndo wanaomiliki biashara ya madini kanda ya Ziwa yote,huwezi linganisha msukuma (Mnyantuzu) wa Bariadi na ujinga huo wa Chatto,Chatto hata mfanye nchi kabisa haina human capital ya kupaendeleza,angejikita kuwasomesha wanachato zaidi ya anavyofanya hivi sasa,sijui nani anamshauri huu ujinga,nakumbuka alikuwa ana ndoto ya kupafanya mkoa siku nyingi,isingekuwa Kikwete Geita isingekuwa makao makuu ya mkoa
 
Magufuli sio wa kumtetea kabisa,hayo ni maelekezo yake asilimia 100,wala usisingizie wasaidizi wake
 
Wananchi wa chato naona neema imewatembelea kwakweli.
Pale kuna umaskini wa kutupwa,yaani hii roho mbaya aliyonayo kwa watanzania anayo mpaka pale kijijini kwake Chatto,yaani kama alivyosema Nyerere dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana,yaani anavyobagua mikoa na wilaya ndo anavyobagua mitaa na vijiji vya Chatto,huyu jamaa makuzi yake yalikuwa yana shida kubwa sana ,pale Chatto maendeleo na majengo mengi anajenga karibu na ka-hoteli kake ambapo ndo kwake,yaani kwa kifupi vitu vingi anajenga kijijini kwake pale,mita mia mbili tu kutoka kwake pale hali ni mbaya haswa,nilikosea sana kumpigia kura mtu wa namna hii
 
Magufuli sio wa kumtetea kabisa,hayo ni maelekezo yake asilimia 100,wala usisingizie wasaidizi wake
Mapungufu yake kwenye jambo au sekta moja hayawezi kuwa sababu ya kuto mtetea kwenye mengi mazuri anayofanya.
Kila mtu ana mapungufu flani, hakuna mtu mkamilifu kwa yote.
 
Mapungufu yake kwenye jambo au sekta moja hayawezi kuwa sababu ya kutomtetea kwenye mengi mazuri anayofanya.
Kila mtu ana mapungufu flani, hakuna mtu mkamilifu kwa yote.
Kwa hiyo ana mapungufu machache zaidi ya mazuri,seriously πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚,mimi nilikuwa namkubali sana kipindi akiwa waziri mpaka kuna kipindi kile iliposemekana kawekewa sumu akakimbizwa sijui hospitali ya dodoma mara Ujerumani roho iliniuma sana,lakini leo yaani kwenye ule wimbo Idd Amini akifa mimi siwezi kulia hapo kwa Idd Amin weka jina lake
 
Sikujua kama ulikuwa hapa kubishana! Binafsi nipo hapa kuelimishana.

Samahani naweza kuwa nimekosea lakini bado akili yangu inaimani sijakosea.

Tambua fika mtu anafanya unyanganyi wa mali na kuzihifadhi bila kujua vipi ataziendesha wala kuzalisha.

Aliowanyanganya kwa kisingizio cha uhujumu uchumi ndio hao hao wameshikilia uchumi, hivyo inaonyesha dhahiri shahiri zilikuwa mali halali na wanajua jinsi ya kutafuta.

Kiongozi imara na mzalendo hapimwi kwa kutojenga kwao!. nyerere huyu aliyetengeneza gap la ufaulu baina ya jamii fulani na jamii fulani ndio awe mzalendo?!

nyerere yupi anayenasibishwa na maono wakati alishindwa kuchanga karata vyema enzi za Muingeleza?!

nyerere huyu aliyeua viwanda na viwanda maeneo mbalimbali ya taifa hili?

Ni yupi unamsema hapa nyerere huyu aliyeiachia Nchi madeni ya kukata na mundu?! Umaskini wa kiwango ujamaa?! nyerere yupi anaemsema hapa aliyefia United Kingdom?! Leo ndio nimepata vigezo vya mtu kuwa mzalendo.

Istoshe nyerere anao ukoo mfupi sana, wacha kumnasibisha kuwa baba watu wanababazao bwana.
 
Huo ni mtazamo wako sio wa wote.
Najua hakuna mtu anapendwa na watu wote.
 
Geita kumenogaaaaa, ila mkuu tukumbuke na huku Mbogwe, Barabara ya Masumbwe- Lugunga- Geita mjini iwe ya lami
 
Kiongozi imara na mzalendo hapimwi kwa kutojenga kwao!. nyerere huyu aliyetengeneza gap la ufaulu baina ya jamii fulani na jamii fulani ndio awe mzalendo?!
Kwa sentensi hii nishakujua wewe wa namna gani.
Tujadili mengine, mjadala huu wewe umeshinda kwa maana upo sahihi kwa viwango vyako.
 
Kwahiyo ulitaka afanye kama baba wa taifa sio. achana na mawazo potofu nchi hii ni tajiri hatuwezi kuendelea kuwa maskini kisa Fulani akufanya ivyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…