Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Acha ijengwe tu kwani Chato iko Burundi?
Mobutu seseko mwingine huyo!
1.Mbuga chato
2.Bandari chato
3.Airport chato
4.Jengo la kisasa TRA chato
5.CRDB walilazimishwa kufungua tawi chato
6.Hospitali ya rufaa chato
7.Mataa ya kuongozea magari chato
8.Meli mpya chato
Chato ni wakati wenu sasa kuneemeka na utawala huu wa JPM!
 
Alisikika mlevi mmoja Kwanini makao makuu ya nchi yasipelekwe Chattle ili kuboresha utendaji kazi hata bandari ya Dsm hamishiwe Kama Kuna uwezekano pia mlima Kilimanjaro uhamishiwe huko ili kukuza utalii na biashara vipi kuhusu Chuo kikuu kujengwa Chattle
 
Kwanini hiyo hospitali isingejengwa kigoma ili ihudumie mikoa ya Rukwa,Kagera na Kigoma yenyewe?Chato kwenda bugando ni karibu,watu wa kigoma mpaka waende Mwanza na usafiri ni majanga!
 
we jamaa una mawazo ya kishetani kabisa, utalegea tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Bugando iko wapi mkuu!! Au hapo hapo Mwanza zijengwe hosp 2 za rufaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndiye uliipatia Mwanza hicho kitovu?!, Kwanini isijengwe Musoma, Kahama, Shinyanga au Bukoba?!

Zama za Daslam na Coast zimefikia tamati, ilikusudi taifa liendelee lazima maendeleo yatapanywe.
Yanatapanyiwa chato tu, kwa nini yasitapanyiwe misenyi au ikungi?
 
Nchi imejamba hii.
Rukwa, Kagera na Kigoma wanahitaji sana hiyo hospitali ya Rufaa kuliko Chato iliokaribu na Bugando hosptali.
Tumekwama kwa kweli sio ya kuchekea haya.
 
Wamejitokeza kutumia fursa baada ya kumsoma Magu,wanaona mamiradi yanaelekezwa huko,kwanini wasitumie fursa?Kigoma,Kagera,Rukwa hakuna hospitali yenye hadhi ya rufaa!Wagonjwa Wote hukimbilia Bugando Mwanza,hii ni wazi JPM ameamua kuwa Mobutu Seseko!
Kitaalamu inaitwa bureaucratic competition!!
 
Ndo maana safari hii membe twende naye, nyie mmekula imetosha, vyeo vyote vikubwa mmepeana wenyewe.
 
Hii si sawa, kanda ya ziwa hospitali za rufaa mbili, kanda ya kusini hakuna, kanda ya magharibi hakuna. mmhh ukabila/ ukanda unapanda chati, umoja mshikamano utaporomoka tusipojisahihisha
Hii nadhani inaweza kuligawa taifa
 
Aaah Tanzania ya viwanda....πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚na mie pia nimecheka ingawa siyo mjumbe wa kamati...



Everyday is Saturday............😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…