Chawa wa Mama wamemgeuka Salim Kikeke; wamempora nafasi yake wamempa Mobhare Matinyi

Kwa kweli ameshusha sana CV yake. Ni bora hata angeanzisha kituo chake cha redio kama alivyofanya Abdalla Majura. Hata kijana mdogo Millard Ayo anamzidi ubunifu.
 
aah kumbe sio kosa lako ndugu yangu- ungalau umesoma kule kwa " Father dead Mother dead, now job". Nimekuelewa.. samahani, nilidhani ni wa level ya kuelewa maana ya QC au KC. nilikosea sana kusema maneno hayo. Jiongeze huko kwa wenye kiona mbali na usiishie hapo UDSM pekee...

Chukua mchOngo huu wa scholarship wa sheving labda utakusaidia, deadline bado hadi 6 Nov 2023: Apply | Chevening jaribu bahati yako ukaangaze macho na kuyatoa tongotongo usije sema hukujua....au Mtafute professor Makumila akupe mchongo wa Fulbright, ukishindwa huko, nenda jengo la umoja wa vijana palipokuwa makao makuu ya Unesco zamani na tafuta kitabu kinaitwa "study abroad prospectus", humo kuna ma-scholarships kibao ya kukusaidia kupanua mawazo duniani mpaka kwa mzee Yutong. Yote haya ni kwa kukusaidia tu. Kama hutaki, ruksa kupuuzia ushauri, mjumbe hauwawi... na ukitaka ushauri zaidi, ni pm nikusaidie jinsi dunia inavyo zunguka, sio kimatango pori kwa mlivyo karirishwa UDSM.
 
Daaah!....Tunataka kusema chawa wana nguvu kuliko "vetting pool" au merits?...Akili ya Taifa nayo tuseme inaruhusu "inner cycles" kushambuliwa na chawa?...sycophants wanazungukwa au? Nitakuwa wa mwisho kuafiki juu ya uchawa kwenye hili.
 
Kikeke hana shule yule ni mhuni mhuni tu. Kilichomtoa BBC ni shule sio kingine.
Kwa mtu mwenye maarifa hawezi kutoa kashfa kama hizi kwa mwenzake kwa sababu tu ya chuki binafsi
Labda niulize tu; Kwani huko BBC alijipa kazi mwenyewe au lile ni shirika la ndugu yake???
By the way, angekuwa hafanyi vizuri wangempandisha ngazi kiasi kile?
kuweni basi na kiasi tunapo ongelea maisha ya mtu (mwenzetu)
Baadhi ya Watanzania tuna hulka ya kuoneana wivu sana na ndio sababu watu hawasaidiani, badala yake tuna achia majirani zetu wanachukua fursa zote nzuri huko nje sisi tukiendelea kupiga domo kwa kuchafuana....
 
Umeandika vizuri sana isipokua kwenye kulipwa mamilioni ya paundi.
BBC ina matangazo ya lugha nyingi sana, kwenye Radio na kwenye Tv wana channel nyingi.
Anaelipwa paundi milioni ni mmoja tu Gary Lineker analipwa £ 1.35m kwa mwaka. Kipindi chake pendwa kinaitwa MATCH OF THE DAY.
 
Hivi inakuwaje mtu ana kazi nzuri na inalipa vizuri tu anarudi kufanya kazi ya kuteuliwa, Je kuna siri gani ambayo wenzetu wanayo? Tanzania si mbinguni aisee.
 
Sema umezoea maisha ya unafiki Kikeke shule hana, lazima kuishi kwa ukweli ujanja ujanja na uhuni ndio umemfisha hapo. Kikeke na Kitenge tofauti yao ni ndogo sana. Tuishi kwa ukweli mabadiliko ndani ya BBC ndio yamemtoa.
 
Hata haujui unachokiongea. Hoja yako kuwa Wazungu UK hawaangalii elimu sasa unataka nikasome tena mbona unaongea kama zimekuruka mzee. Nyie ndio wazee wajinga mnaozeeka vibaya, turudi kwenye hoja ya haya yoote ni kuwa Kikeke shule ndio imemtoa hapo BBC. Sasa unakuja na hoja dhaifu sana. Nimeishi kwenye media za hapa nyumbani kama miaka 34 hivi najua ninachokiongea. Kuwa na uhuru wa hekima na mawazo sio ujuaji usio na mawanda.
 
Kwa kweli ameshusha sana CV yake. Ni bora hata angeanzisha kituo chake cha redio kama alivyofanya Abdalla Majura. Hata kijana mdogo Millard Ayo anamzidi ubunifu.
Majura kauza Radio yupo hoi hakuwa na akili ya Uongozi na utawala. Akikaririshwa akili za KIPUSA.
 
Weka contacts basi twende kwa Pilato- mbona hilo hulitaki?
 

Sawa ndugu kikeke. Ila pole sana kama uliamini watakupata hiyo nafasi.

Ila endelea kuwa mvumilivu, usilalamike sana wasijekukuoa kesi ngumu.

Wewe chutama tu, utashangaa mwenyewe blanket litakapotoka. [emoji23]
 
Wewe ni mbishi wa kiswahili. Unapobisha jambo toa ushahidi. Usibishe tu kama upo kwenye kijiwe cha ghahawa.
Sasa huyo anayesema kikeke aliahidiwa usemaji wa serikali wapi ushahidi wake. Si aheri mimi nasema facts. Ni uongo bbc hawafanyi kwa mkataba? Je ni uongo wafanyakazi bbc hawana muongozo? Je tido hakua na kesi kisha kuhusu mkataba na star times?...
 
Kikeke vs Mobhare Matinyi, liTISS lililokubuhu kiasi cha wenzake kuliogopa lisipewe uDGIS, nani anastahili kuwa Mkurugenzi wa Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali?
 
Umemaliza [emoji2956][emoji2956]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…