Checkmate ya Siasa: Pale Mfumo Unapolazimika Kujilinda Dhidi ya Shinikizo baada ya kufanya blunders

Checkmate ya Siasa: Pale Mfumo Unapolazimika Kujilinda Dhidi ya Shinikizo baada ya kufanya blunders

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Post zilizopita nilisema serikali au mtu hutawaliwa na kwa kutumia mambo matatu. Yaani ili serikali yeyote dunia iongoze hutumia. Mambo haya matatu;

a) Hofu
Kile watu wanachokiogopa. Serikali nyingi za kimabavu hutumia njia hii. Hata hivyo hasara ya njia hii ni haifanyi utawaka udumu kwa muda mrefu.

Kutisha watu, kufanya matendo fulani yanayoogopesha wananchi. Hivyo watu hutii kwa kuogopa lakini bahati iliyo mbaya. Saikolojia ya binadamu hofu huzoeleka na mtu hutafuta namna ya kujikomboa.

b) Matumaini na matamanio.
Hii ndio njia iliyobora zaidi. Serikali au viongozi hutoa maono, ahadi na ndoto kulingana na matamanio ya watu. Hii hufanya watu kuamini, kuipenda na kufikia hatua kujitolea hata kama mtu anaumia atavumilia.
Hii aliitumia sana Magufuli. Kwamba vumilieni tuu. Tanzania ninayoenda kuijenga itakuwa kama uraya(in magufuli voice)

Njia ya matumaini hufanya wananchi wa chini kupenda viongozi wa juu.

c) Imani. Kile watu wanachoamini.
Imani huja kwa kusikia. Masimulizi. Mjenzi wa simulizi na habari za media huamua hatma ya utawala.

Serikali huratibu media na wenye masimulizi kama vyombo vya habari, waandishi wa vitabu vya fasihi, viongozi wa dini. Kwa sababu hiyo team ndio msingi wa kujenga masimulizi kwenye jamii.

Kumbuka watu huishi kwa simulizi. Hadithi za mashujaa wa kale, viongozi wa kitaifa kupambwa ili lengo kujenga uaminifu kwa wananchi.

Dola nyingi duniani zilizodumu kwa muda mrefu karne na karne zilichanganya njia hizo zote tatu kwa uwiano mzuri. Huku njia ya hofu ikiachwa isitumike mara kwa mara.

Njia ya hofu hapa nazungumzia kutishana, kutekana, kubambikiziwa kesi, kufanyiana siasa chafu n.k.

Serikali ikishatumia njia ya hofu kwa kiwango na kwa muda mrefu inajikuta katika hatari ya kukosa uhalali. Kutoaminiwa. Na hivyo kutishia kuanguka.

Katika mchezo wa siasa, serikali haipigani vita vya silaha pekee; inapigana pia vita vya taswira(kulinda taswira, uaminifu na mtazamo wa wananchi. Kama nilivyosema siasa ni kama mchezo wa Chess. Ndani ya mchezo huu wa chess, kuna silaha mbili kubwa ambazo watawala hutumia: hofu na matumaini.

Serikali yenye busara hujenga utawala wake kupitia matumaini; huaminisha wananchi kuwa kesho inaweza kuwa bora. Lakini mifumo mingi ya kisiasa hasa katika nchi zenye taasisi dhaifu zimejikuta zikitumia hofu kama chombo cha kudhibiti nguvu ya umma.

Hofu hujengwa kwa njia mbalimbali: kudhibiti sauti zinazopinga na kukosoa serikali, kuonyesha nguvu ya dola, au kufanya wananchi wajione kuwa gharama ya kupinga mfumo ni kubwa kuliko faida yake. Ndio ile mtu kusema ukweli utakuta anaambiwa shauri yako utapotezwa, kaa kimya hakuna faida ya kujihusisha na hayo. Au kuna ile kuambia achana na wanasiasa na mambo yao.

Lakini tatizo la hofu ni kwamba ina uwezo wa kutawala kwa muda mfupi, si kujenga uaminifu wa muda mrefu.
Wakati mfumo unapokutana na shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi, mchezo mpya huanza, ni kama kwenye draft itumike force kingi kwa wale wadau wa draft. Na force kingi haiji bila mitego.

Hapa ndipo wana mikakati wa ndani ya dola huingia kwenye hatua ya “damage control” kurekebisha taswira, kupunguza presha na kurejesha imani. Kisha kutoa matumaini. Kama nilivyoandika kule juu. Na hii ni kuondoa ile presha iliyosababishwa na mbinu ya kutia watu Hofu kufeli au kuelekea kufeli.

Hapa serikali watafanya hatua kuu zifuatazo;

1. Hatua ya kwanza huwa ni vita ya mawasiliano.
Serikali itajaribu kueleza msimamo wake, kuonyesha mafanikio yake na kujenga picha kwamba mfumo bado una udhibiti wa hali. Serikali katika hatua hii itaonyesha bado inaaminiwa na wanachi, inaweza kuendesha nchi na kulinda rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na wananchi wake.

2. Hatua ya pili ni kuelekea diplomasia ya kimataifa.

Mawaziri, mabalozi na viongozi wa juu hutumika kueleza sera za nchi, hapa safari nyingi zitafungwa kwenda nchi za nje na mialiko ya wakuu wa nchi kuja nchini. Lengo ni kurekebisha na kusafisha taswira ya nchi kimataifa. Pia kupunguza ukosoaji kwa kuwaweka karibu wapinzani na watu wenye ushawishi ikiwezekana kutoa msamaha ya wafungwa wa kisiasa.

3. Hatua ya tatu ni kujaribu kubadilisha simulizi.

Mtibeli katika utunzi wa riwaya hii tunaita Plot twist. Sasa Katika siasa, anayemiliki simulizi mara nyingi huwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo.
Lakini changamoto kubwa kwa mfumo wowote unaotegemea hofu ni kwamba dunia imebadilika. Teknolojia, mitandao ya kijamii na ongezeko la uelewa wa wananchi vimefanya iwe vigumu kuficha kila kitu.

Ndio maana wanaharakati wa mtandaoni wanajitahidi sana kwenye kipengele cha Simulizi. Wanaeleza matukio, wanayapa hisia, wanayapa makazi katika mioyo ya watu. Mara kadhaa hutumia propaganda ilimradi wao ndio wamiliki Simulizi. Na hili likifanikiwa mchezo utakuwa wakwao. Hii ni Chess games.

Kete ya mwisho katika chess haiamuliwi na nguvu pekee; inaamuliwa na uhalali (legitimacy). Serikali inaweza kuwa na vyombo vya dola vyenye nguvu, lakini bila uaminifu wa wananchi, nguvu hiyo huwa na mipaka.

Mwishoni katika kila mfumo unafika mahali lazima uchague: kuendelea kujenga utawala kwa hofu, au kubadilisha mchezo na kujenga utawala wa matumaini, haki na uwajibikaji.

Kwa sababu katika Saikolojia hofu inaweza kumfanya mtu anyamaze, lakini ni matumaini ndiyo yanayomfanya mtu aamini.

Jipatie kitabu cha SIASA NAA UTAWALA: CHESS GAMES
huko ukikosa cha kukusaidia nishtaki.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom