Cheka sana, kula raha sana, Ruka sana, Tamba sana, Jirushe sana, Fanya starehe sana ila Omba ukiugua usije kupatiwa Matibabu kwenye Hospitali zetu!

Cheka sana, kula raha sana, Ruka sana, Tamba sana, Jirushe sana, Fanya starehe sana ila Omba ukiugua usije kupatiwa Matibabu kwenye Hospitali zetu!

KUMBUKA- Ukiwa kwenye starehe jitahidi kusevu na hela kwa ajili ya matatizo kwasababu matatizo yapo tu hivyo yanapaswa yawe na bajeti yake kama ambavyo starehe umeitengea bajeti.
Vijana ukiwambia haya watakwambia acha kutupangia maisha.

Lakini huku mtaani tunaona watu wanavyopata shida sana.
 
Kwa hospitali zetu, matibabu bila pesa jiandae kufa mkuu...nliwahi kumpoteza dada yangu kusa kukosekana damu wakati akijifungua.nMungu ni mwema, mtoto alibaki.
Hata ukiwa na pesa, bado uko mashakani
 
Hospitari zetu ni kama video vya polisi, hakuna ubinadamu, wagonjwa wanachukuliwa kama kelo tu, Kuna siku niliienda muhimbili kuangalia mgonjwa,nikasikia wale wahudumu kwenye wodi wanazungumza, haki ya Mungu nilitoka na stress, w alikuwa wanamzungumzia mgonjwa aliyefariki"Aaah si Yule mgonjwa aliye kuwa anakunya kunya Jana, amefariki"
Nilichoka, pembeni kulikuwa kuna mgonjwa mtu mzima Sana, amevalishwa pampasi,kijana wake akawa ana taka ampeleke chooni kumbadilisha,pambasi likaanguka, mapumbu yote nje, pale kwenye wodi walikwepo wadada wanafanya usafi, hata kusema tutoke kidogo, huyu mzee asitiliwe, waaapi, wamekomaa sura zimewekwa ndita,
Kwa mazingira Yale ya uchafu ukifanya kazi mle wodini,inabidi uwe na roho mbaya,wodi imejaa mbu kibao,
 
Back
Top Bottom