Hakika Intel ya Iran, ilizidiwa mahala.
Wataalamu wa mambo wanasema co-ordination ni muhimu.
Military intelligence ya Iran ipo imara. Civilian intelligence iko dhaifu.
Wataalamu wanasema; ikiwa intelijensia ya kijeshi iko imara, nchi inaweza: Kupanga mashambulizi ya kijeshi kwa ufanisi, kugundua haraka adui anapokusudia kushambulia na kuweka majeshi vizuri kimkakati wa kivita. Hii ni faida kwenye medani ya kivita ya moja kwa moja.
Lakini, civilian intelligence service wanasema ni ujasusi wa kimataifa yaani wa kistretijia zaidi. Na ukifeli hapa ndiyo kama matukio yaliyoitokea Iran yanavyowakumba.
Na ndiyo maana Iran ukiangalia kwa sasa hivi inapambana pakubwa sana kwenye kuuweka sawa ujasusi wa ndani kwa kuondoa mashushu wa Mossad, na kwa kiasi fulani wanafanikiwa.
Pengine kivipi? Ni kuweza kupunguza kuharibiwa miundombinu kwa ndani ya nchi, kwa kiasi fulani wamepunguza kudhurika kwa taasisi sa ndani na kasi ya kuuliwa kwa viongozi.
Kwa namna jinsi Iran alivyoshambuliwa, laiti ingelikuwa nchi nyengine basi isingeliweza kunyanyuka. Walipigwa pigo moja kubwa na la hatari sana. Kwa namna ambayo Iran ilivyoweza kuhimili na kujipanga na kupambana wameonyesha kitu kikubwa sana.
Na si ajabu hawakutaka moja kwa moja msaada wa kutoka nje. Wameamua wapambane na wajisafishe wenyewe. Nakumbuka Lissu alivyokuwa anafanyiwa interview kuhusu hali iliyowakuta Chadema alimnukuu Mzee Al Hassan Mwinyi, kuwa:
"Unapofungua madirisha upate hewa basi kila kitu kitaingia. Itaingia hewa, nzi na wadudu wengineo..."
Iran naye katumia njia hii! Laiti angeliruhusu kupokea msaada hali ya kuwa taasisi za usalama wake zipo vibaya ndiyo angeharibikiwa kabisa! Kwa sababu ma-nzi nao wangeliingia humo humo!