Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Bandugu nimepita humu darajani, nawatafuta ndugu zangu BJ na Masanilo. Sijui wamesalimika na kuvunjika kwa daraja la kuelekea Roma.
 
Bandugu nimepita humu darajani, nawatafuta ndugu zangu BJ na Masanilo. Sijui wamesalimika na kuvunjika kwa daraja la kuelekea Roma.

Shadow..
Naona unalipiza uchokozi alioufanya Masanilo wakati wa mechi ya arsenal na manure..Tumesalimika ila bado hali haijawa nzuri, kama mshabiki hali ni hivi sijui kina Drogba,Essien na wenzao hali zao zikoje!!
Inshalaah hatujambo,kipigo kinasikiliziwa tu bado hakijasahaulika...
 

Oh that is good to know, BJ.

Manake nilishaanza kuwatafuta si unajua tena nawajali. Hasa homa za vipindi. I hope na Invinsible naye amesalimika na anaendeleza libeneke kama kawaida. Enjoy lambada to Rome!

Ciao.
 

...mmeamkaje???

mwambie masanilo life goes on bana, ...mbona mimi nimekubali matokeo? najua inauma kunyang'anywa tonge mdomoni, lakini sasa utafanyaje?

Drogba nilishasema anachangia sana ushindi au kufungwa kwa CHELSEA! Game ya Nou Camp alipoteza open chances za kuua game, jana pia hivyo hivyo! ...Jana pia 'aliuza' mechi.

...halafu akajifanya kaumia utadhani wamemuitia Ambulance! nashangaa baada ya final whistle anakuja mbio (tena bila wheelchair) kutaka kumtoa macho Ref! Come on, what a shame?!

Tuseme Chelsea wangekuwa wameshinda kagoli kamoja hako wangemlaumu bado Refa?

Kama masanilo hajiwezi kiasi hicho ABRAMOVICH anajisikiaje? Life goes on,
Jumapili, EPL;

ARSENAL vs CHELSEA
 
Yes the chubby ref was a disgrace but Chelsea did not deserve a win too. Pamoja na Barca kucheza 10 against 11 bado walikuwa wakiwachezesha ligwaride Chelsea nusu-uwanja kwenye home ground yao. Ball possession 30%-70%!

Ktk situation kama hiyo Chelsea ingeshinda, we, the fans of football we are the one who were losing ..😀
 
Kwa waliokosa kuangalia mechi hivi ni vibwagizo tu vya mechi ya Kwanza:

The teams line up in a packed Camp Nou before kick-off



... Alves gets a bit carried away and brings down Malouda



A flying Petr Cech claims a ball from Xavi Hernandez



Leo Messi tries to go inside Jose Bosingwa but the Chelsea defender stands his ground
 
Msiwe mnampanga Drogba kwenye mechi za Champions League sasa, maana last season kwenye finali alitolewa kwa ubabe wa kipuuzi, jana ndio hivyo badala ya kufunga anadive kwa sana tuu ebo.
 
Kwa niaba ya wenzako...Mkuu AB-TCHAZ pole sana!...am glad hujajinyo$%#@&^*....i mean U HAVEN'T GIVE UP!..
 
Oh that is good to know, BJ.

Manake nilishaanza kuwatafuta si unajua tena nawajali. Hasa homa za vipindi. I hope na Invinsible naye amesalimika na anaendeleza libeneke kama kawaida. Enjoy lambada to Rome!

Ciao.

Shadow, thank you indeed!..Tupo salama naamini na weekend inavyokuja machungu yake yatakuwa yamemalizika kabisa, hata ze bluez original bado wanamlaumu refa kwa penalt jana.Lol!..

Invisible,mafua yake yatakuwa yameongezeka!..Atakuwa amekubaliana na hali halisi by now..

Asante,let me enjoy zaidi hiyo Lambada to Berlusconi maana jana nilijua dansi ingeishia pale..
 

Yaani hata usingizi haujaja fresh maana Masa kila akifumba macho eti anamuona Andres Iniesta,muuaji wa ze bluez!..Naamini, he will get over it angalau weekend italeta burudani zingine ilimradi akubali ni historia kwasasa.
Huyo Drogba nae alipitiza hasira,naona hakuamini macho yake walivyofungwa. Sad zaidi kwa bwana mapesa wao huyo mrussi,kitakuwa kimemtachi sana ila ndo hiyo mpira hautabiriki..

Angalau J2 mjipooze wewe+Masa maana wote mmepata vipigo,ze ganaz wafungeni hao ze bluez kama mna vifua!..ha ha ha
 
Nilikubali mpira ni mwisho wa mechi.
Bj,shadow,babu................nimekubali kushindwa.

Najitoa rasmi kushabikia timu za majuu.
Nitakuwa tu namsindikiza rafiki yangu belinda.

Nabakia na timu yangu ya CHUO CHA POLISI MOSHI.
 
Nilikubali mpira ni mwisho wa mechi.
Bj,shadow,babu................nimekubali kushindwa.

Najitoa rasmi kushabikia timu za majuu.
Nitakuwa tu namsindikiza rafiki yangu belinda.

Nabakia na timu yangu ya CHUO CHA POLISI MOSHI.

EJM, rafiki yangu najua machungu yakishatulia utarudi kushabikia timu za majuu. Hizi timu za bongo na migogoro ya kina Kaduguda et al nani anaitaka? Najua mabo yako kwenye ligi za majuu najua kufikia mwezi wa nane utakuwa umerudi kwa kasi na hali mpya!!

Mapunziko mema ila Karibu kwenye kijua cha majira ya 'spring' hapo kwa wa-Roma. Kutakuwa na burudani tosha.
 
Nilikubali mpira ni mwisho wa mechi.
Bj,shadow,babu................nimekubali kushindwa.

Najitoa rasmi kushabikia timu za majuu.
Nitakuwa tu namsindikiza rafiki yangu belinda.

Nabakia na timu yangu ya CHUO CHA POLISI MOSHI.

Tatizo timu za majuu mnazoshabikia nazo mzozo tuu...sasa wewe timu miaka mitano haujachukua kikombe chochote unategemea wataamka tuu na kuingia final ya Champions League?
Hao Chelsea ndio tusiseme historia yao ya kuchukua makombe haijazi ata ukurasa mzima wa A4 paper lakini leo nao wanataka kututishia watu tuliozoea kuchukua vikombe.

Weekend njema na good luck kwenye mechi yenu ya jumapili mtoe draw tuu.
 
Nilikubali mpira ni mwisho wa mechi.
Bj,shadow,babu................nimekubali kushindwa.

Najitoa rasmi kushabikia timu za majuu.
Nitakuwa tu namsindikiza rafiki yangu belinda.

Nabakia na timu yangu ya CHUO CHA POLISI MOSHI.

Exaud!

Pole sana, ndo hivyo wabongo tunasema huna 'kismati' yaani bahati!lol
Kila timu uliyojikita 1/2 fainali umeambulia machungu..Ila easy,ni mpira tu!.

Haya unisikilize mimi, fainali nitakwambia ushangilie timu gani!!!!
Mie mwenyewe timu yangu ya Polisi Dodoma ni damu,hata majimaji haioni ndani..ha ha
 

BJ, hawa wenye majonzi hawako peke yao. Hebu tizama hapa:




Solo celebrations: A sombre looking Frank Lampard stepped out last night after Chelsea's defeat as did disgraced teammate Didier Drogba

Na hapa:


Disgrace: Drogba left the ground tight-lipped in comparison to his onscreen outburst

Na hapa:



Lean on me: Frank's family, sister Clare, and father Frank Snr joined him for dinner to offer him support

and then na hapa:



Losers: Nicolas Anelka and Michael Essien - who scored Chelsea's only goal - look drained post-match


Stunned: John Terry and wife Toni leave Stamford Bridge after Chelsea's nightmare night
 
Icadon,

Najua unafurahi mmekosa kipigo, we will meet FA! Umecheki nembo kwenye gari ya kaputeni wetu JT?

 
Icadon,

Najua unafurahi mmekosa kipigo, we will meet FA! Umecheki nembo kwenye gari ya kaputeni wetu JT?


Naona mbawa kwenye B heheheh mie hilo siliwezi labda kale kamradi kakifisadi kakipita au niuze figo na maini.

Pole sana kwa kutolewa, ila ndio ukubwa huo.
 
Kwa niaba ya wenzako...Mkuu AB-TCHAZ pole sana!...am glad hujajinyo$%#@&^*....i mean U HAVEN'T GIVE UP!..

Kwa niaba ya Ze Blues Fans ktk JF nasema tumeshapoa; tunaangalia yajayo hasa mechi ya Jumapili dhidi ya washika bunduki.

Pamoja na kutolewa kimizengwe tumethibitisha kwamba tunaweza kuifunga timu yoyote duniani.

Kuna watu walikuwa wanaota tutabebeshwa kapu la magoli kama c kontena; hao hao wakabaki wameduwaaa watu walivyopotezwa kwa 4-2-3-1.









BIG UP TO OUR PLAYERS 4 THEIR SPIRIT; ALUTA CONTINUE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…