Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Mmegongwa MAKENGE nyie😂😂
 
Mmeshinda ngapi MAKENGE nyie
 
Baada ya matokeo ya sare na Everton, hii mechi na Fulham nilikuwa naiogopa sana. Nikasema kama Everton walitusumbua basi Fulham atatukera

Fulham ametoa draw na Arsenal & Liverpool ambazo ni team bora zaidi yetu.

THE BLUES ikicheza mashabiki wake duniani kote wanapita mtaani wakiomboleza, bingwa wa dunia amewambwa msalabani
 
Jamani sisi hatuko kwenye mbio za ubingwa tunajenga katimu tukutane wikiendi
 
Ndugu yangu umenipa matumaini ya uwongo, Ahsante kwa kuharibu bajeti yangu. Baada ya ushauri wako nikaagiza kuku choma na kinywaji baridi nikaanza kujipongeza kwa ushindi tutakaopata.
 
Nyie Kenge mshaanza na nyinyi kuleta Unyumbu au hua mnatuona tunafaidi?
Sisi Nyumbu dua zetu zote tunazielekeza kwenu mchukue Epl msimu huu ili mtuepushie fedheha ya kutwaa ubingwa watesi wetu Liverpunda au ile misukule ya Tetea lakini naona mnaleta utoto.
Sasa mnafungwaje goli na mchaga anaitwa Munisi?
 
Kenge zimetolewa damu.

Eti mnajifanaisha na team inayoweza kuchukua ubingwa mbele ya Liverpool.

Kenge maji kabisa nyie.
 
Tumefungwa na Fuham kwa makosa makuu mawili kwanza kumtoa Jackson ambae anadefend na kuweka Nkunku kosa la pili Neto alichoka mapema na kocha kashindwa kumuondoa na kumueka madueke goli zote zimepita kwa Neto.

Enzo hawezi kumudu midfield tunahitaji Lavia arudi wakiwa na Coicedo kati kati tunakua vizuri sanaa, tumekua dhaifu sanaa kati kati ya uwanja.
 
Dah ,wakuu ,tumewambwa msalabani , tumeshenyentwa kiufupi mamaee
Hii game inaniuma sana
Mliongalia game mtupe mrejesho game ilikuwaje ?
 
Najua Arsenyetoz huko wanachekelea chooni mamaeee ,yatakuja kutujazia nzi humu mpaka basi ,we ngoja tu .🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…