Niwakumbushe tu kwamba pamoja na kujikongoja kwa Chelsea na matatizo na uchanga wa Chelsea bado ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi na baada ya mechi 28
Kwa hizi mechi kumi zilizobaki usishangae tukadinda na kumaliza wa nne au watatu
Wesley Fopfana karudi yuko kikosini
Romeo Lavia Yuko na karudi kikosini
Nicolas Jackson anakuja kuungana na Cole Palmer baada ya mapumziko ya kimataifa
Madueke anarudi naye kama Jackson -kumbuka baada ya Palmer na Enzo Fernandez, Madueke ndie anafuatia kwa kutengeneza nafasi Chelsea.
Reece James kapteni yuko fiti na anacheza vizuri na kufunga magoli kama mfano wa kuigwa
Enzo Fernandez yuko kwenye form ya hali ya juu
Moises Caisedo jembe, haugui wala hapati majeraha wala hachoki
Pedro Neto huyo kasemwa semwa akaamua sasa kupress uwanja mzima mwenyewe
Jadon Sancho form inarudi kwa kasi
Marc Cucurela ndio sina la kuongeza Jembe na beki bora EPL
Levi Colwill na Tosin wameamua hapiti mtu kule nyuma
Wachezaji wote na kocha wamesema top 4 ni ya lazima na kushinda UECL ni ya lazima pia
Mechi hizi 10 zilizobaki zitakuwa ngumu sana sio kwetu bali kwa wapinzani wetu
Top 4 tunatinga na onyo tunatoa mwakani tupo kwenye mbio za ubingwa watake wasitake kwanza kwa sababu Liverpool watakuwa goigoi sana baada ya Mohamed Salah na Virgil van Dijk kuondoka.
Arsenal ni ile ile haibadiliki hata wakiwa kwenye form ya hali ya juu wao ni wasindikizaji tu
Man City ujenzi wa nyumba mpya unaanza mwakani, hii ya sasa haikaliki imechoka sana
Nani atatuzuia ubingwa mwakani?
View attachment 3266149