Cheo cha Makamu wa Rais hakina tija, tukiondoe, tubakishe cha Waziri Mkuu


1. kuna gharama za logistic za ofisi zitapungua mfano mashangingi, misafara etc
2.kuna gharama za ulinzi zitapungua
3.kuna mshahara, pensheni na perdiem zitapungua
4.kuna watu wanafanya majukumu yaleyale yanayofanana kwa mfano mwandishi wa hotuba za makamu wa raisi watapungua maana hatuwezi kuwa na watu wawili wafanye kazi moja
5.Kuna bajeti ya furniture, marupurupu ya makamu na watu wazito katika hiyo ofisi yatapungua


,
 
Sahihi mkuu hakina tija Kwa taifa na sioni km anawajibika ipasavyo Kwa taifa hili bora abakie waziri mkuu
 
Mleta mada kashauri majukumu ya ofisi ya makamu wa rais yatafanywa na ofisi ya waziri mkuu.
 
Kwenye suala la waziri mkuu hoja yako ni dhaifu na haina mashiko. Waziri mkuu ni mtu mdogo kwa Rais wa Zanzibar which means hawezi kuextend utendaji wake Both Tanganyika and Zanzibar
 
You are right lakini vilevile kwa kuwa Rais ni executive, Makamu naye awe executive achukue madalaka yote ya Waziri Mkuu ili tusiwe na Waziri Mkuu kabisa huku succession ya nafasi ya urais ikibaki kama sasa.
 
Yule mama anatusaidia kweli kutuwakilisha huko nje. Sasa hivi kungekuwa na references kibao za font page, hiyo hiyo huko duniani.
Mama sio tatizo, tatizo huo wadhifa. Kwa kweli mie sioni umuhimu wake. Waziri mkuu anatosha. Hata wakuu wa wilaya sioni kazi yao, mkuu wa wilaya asiwepo, wakurugenzi wanatosha wataripoti kwa mkuu wa mkoa. Mbunge awakilishe wilaya yaani wilaya ndio iwe jimbo.
 
Halafu mtu mwenyewe Mzanzibar.

Mambo ya Tanganyika yanamhusu nini?
Mkuu hata mimi huwa nashangaa Watanganyika mambo ya Zanzibar yanawahusu nini ?
Kuna mashoga eti oo Zanzibar isijiunge na OIC na lazima tuungane nao..
mtaolewa
 
Tatizo wapo wanasiasa ambao hawataki kabisa uguse katiba ya 1964 na badae kuwa revised 1977 maana inawapa mandate ya utawala wa ku maintain status quo..Wananchi wengi walitoa maoni yao kuhusu muundo wa muungano na utawala wa Zanzibar na Tanganyika lakini hayo mapendekezo ya katiba ya Marehemu Adrian Mvungi na Warioba yatavuruga mfumo wa utawala wa ku maintain status quo wanaona bora tukae na katiba hii ya muundo wa chama kimoja.
 
Mleta mada kashauri majukumu ya ofisi ya makamu wa rais yatafanywa na ofisi ya waziri mkuu.
Sahihi.
Nami nikaongezea kuwa kitendo hicho kitaongeza majukumu na matumizi ya OWM kama niliyoainisha
 
Kwa maana hiyo ndiyo maana baba hataki kusafiri...

Anaweza kuta mambo yamepangwa vile asivyataka yeye...


Cc: mahondaw
 
Kwa maana hiyo ndiyo maana baba hataki kusafiri...

Anaweza kuta mambo yamepangwa vile asivyataka yeye...


Cc: mahondaw

Bajeti ya kuendeshea ofisi ya Makamu wa raisi ikiwekwa kwenye kujenga hata vyuo vya VETA kuna faida zaidi kwa Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.
Hii kazi ya kusubiri raisi aumwe/asafiri ili ukaimu haina tija!
 
Ni kweli ni gharama kubwa kuwe na Rais kisha Rais wa Zanzibar awe makamu wa Rais na Waziri mkuu anayepenya mpaka Zanzibar kwani Zanzibar kenyewe ni kadogo kuliko hata wilaya ya Bagamoyo iweje kawe na utitiri wa Viongozi wakati Tanganyika ndiyo hutaabika kuwahudumia
 
Unajua kuwa katiba mpya inataka serikali nyingine ya tatu. Yaani raisi, makamu raisi, na wabunge nadhani wa Tanganyika.

Yaani kila mwanasiasa apate fursa. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Biko Kila Mtu Apate πŸ˜€πŸ˜πŸ˜ƒπŸ˜‚
 

Kipindi cha Nyerere ujue Rais wa Zanzibar ndiyo alikuwa makamu wa Rais, wachenjii juu kwa juu mbona katiba yenyewe magufuli huwa haifuati? Katiba inaruhusu mikutano ya siasa kwa Wapinzani lakini yeye kapiga marufuku, mahakama hazipo huru inaingiliwa ni mara mia afanye kupunguza viongozi ili ile kauli yake ya kubana matumizi ilete maana
 
Moja ya mambo ya hovyo aliyotuachia Mwl Nyerere.
Muungano ufe kila mmoja akae kwake kwani pesa inayotumika kuubembeleza kuulea muungano, kuwalipa mishahara utitiri wa watumishi Zanzibar ikibakia Tanganyika ujue kuwa Tanganyika itakuwa Nchi tajiri kuliko Nchi zote barani Africa kwani pesa inayotumika huko Zanzibar ni kubwa mno kupita wanachozakisha wao kama visiwa, Hazina ya Tanganyika inamenyeka kuwalisha Zanzibar ambao huwa hawana shukrani na mda wote hulalamika na wanataka muungano Ufutike ili waolewe na kufunga ndoa na Oman wakidhani Zanzibar itakuwa kama Dubai wana ndoto nyingi za asubuhi saa 12 .
 
Mkuu hata mimi huwa nashangaa Watanganyika mambo ya Zanzibar yanawahusu nini ?
Kuna mashoga eti oo Zanzibar isijiunge na OIC na lazima tuungane nao..
mtaolewa

Zanzibar iachwe maana mda mwingi hudai talaka ndoa yao na Tanganyika ni ndio ya mkeka wameichoka
 

Tatizo ukivunja Muungano, Je unaujua mpaka wa Tanganyika na Zanzibar ulipo?

Baada ya Muungano kufa ama ni vita ya kugombea mpaka wa maji baharini baina ya Tanganyika na Zanzibar au ni kwa Tanganyika kupata kaeneo kadogo ka bahari katika uelekeo wa bahari ya zanzibar na Pemba!. Yaani ili kuipata Bahari kuu kutokea Tanga na Dar lazima ushuke hadi mtwara huko ndo uitafute, La sivyo utalazimika kupita ama katika maji ya Kenya au katika maji ya nchi ya Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…