Cheo cha Makamu wa Rais hakina tija, tukiondoe, tubakishe cha Waziri Mkuu

Kwenye suala la waziri mkuu hoja yako ni dhaifu na haina mashiko. Waziri mkuu ni mtu mdogo kwa Rais wa Zanzibar which means hawezi kuextend utendaji wake Both Tanganyika and Zanzibar

Ka Zanzibar ni kadogo sana kangefaa kuwa mkoa tu wala haifai kuwa Nchi ni mara mia muungano ufe waachwe wenyewe uone Tanganyika itavyopumua baada ya kujivua zigo la kuilea Zanzibar iliyojaa watu wengi wavivu wakaa vibarazani hawapendi kufanya kazi mda mwingi huutumia kulalamika tu juu ya muungano usio na Tija kwa Taifa kwa sasa Zaidi ya kuwa muungano mzigo kwa walipa kodi
 

Mipaka ipo na Tanganyika ana nafasi kubwa baharini pia ukumbuke muungano ukifa lazima na pemba watajitenga na unguja na kuwa Nchi tofauti hilo lipo na halina Ubishi.
 
Mam
Yule mama anatusaidia kweli kutuwakilisha huko nje. Sasa hivi kungekuwa na references kibao za font page, hiyo hiyo huko duniani.
Mama pia anatusaidia sana kupoza moto ENGINE pindi ENGINE ikipata moto!
 
Umekosea kusema ivo.

Nadhani hujui majukumu ya Makamu wa Rais wewe vizuri.

Ungesema kua aondolewe kwa kua hana kazi tena awamu hii.

Traditionally, Kazi kubwa ya Makamu wa Rais ni kua MKATA UTEPE mkuu wa Serikali.

Kumbuka enzi za Gharib Bilal alikua anatembea na mkasi wake huku akitoa hotuba maridhawa!

Ila awamu hii Kazi ya Makamu wa RAIS inafanywa na Rais....kila utepe unakatwa na John Pombe...

Sasa Makamu wa Rais hana kazi tena zaidi ya kula mshahara wa bure tuu.
 
Makamo wa raisi alikuwa bwana mikasi ila awamu hii raisi ndo bwana mikasi mzinduzī
 
Ukiniuliza Makamu wa Rais wa Tanzania kazi zake ni zipi hata sijui
 

maana ya makamo wa raisi ni sawa hospitali kuwa na madaktari wawili. wanao tibu hakiwepo huyu hata msaidia mwengine
 
Ngoja wengine wenye damu ya Kunguni kuelekea ' Krismasi ' hii tunyamaze.
 
Mkuu kama ndivyo, washawishi wakubwa waiache Zanzibar ili uchumi wa Tanganyika unawiri. Nionavyo ni kinyume na uonvyo wewe, na hii ndio kibinadamu. Tafadhali anza hiyo kampeni.
 
Mfano sasa hivi Rais ni Pombe. PM ni Majaliwa. Ukimwondoa Samia, Zanzibar watakosa uwakilishi nafasi za juu.

Dhana ya running mate ni kwamba kati ya Rais na Makamu wake, mmoja akiwa Mtanganyika, mwingine awe Mzanzibar
 
Majukumu ya Makamu wa Rais yanaweza kufanywa kwa urahisi sana na ofisi ya waziri mkuu, hivyo basi itakuwa ni jambo la busara endapo cheo hiki kikafutiliwa mbali, na majukumu yake akapewa Waziri mkuu, maana hata hivyo hakuna kazi yeyote inayoonekana moja kwa moja ikifanywa na makamu wa Raisi, kikubwa ni kusibiri mtu atangulie ili ashike kiti cha urais, hakuna lingine.

Kuna tetesi nazisikia huko, eti kuna bilioni 18 zinatumika kumjengea ofisi Makamu wa Rais, nadhani hii habari ni ya upotoshaji, sitaamini hadi nione kwa macho yangu hiyo ofisi ikijengwa kwa pesa hizo; hii habari itakuwa ni ya uzushi, nchi hii hakuna taahira wa kupitisha bajeti ya bilioni 18 kujenga ofisi.

Taahira wa hivyo hajazaliwa bado, tusidanganyane hapa..; hostel za Magufuli zilijengwa kwa bilioni 10, na leo vijana wanajiachia tu pale, sasa ofisi ya bilioni 18? Ridiculous joke!
 
Sasa atakae kata tepe za makanisani atakuwa waziri mkuu?


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Huwajui ccm wewe! Chato unakuwa mkoa soon ndio wafute VP?
 
Hii nchi ni maskini kwa sababu Mapato yake karibu yote yanatumika kwenye utawala.

Hiyo ndiyo siri kubwa ya CCM kungangania madaraka makubwa yabaki kwa Rais na wakubwa ili waendelee kuneemeka kupitia maofisi na miradi ya kuwajengea maofisi huku wananchi na wafanyakazi wa Chini wakiwa hawana makazi bora ya kuishi.

Tanzania tungekua na uchumi mkubwa kama Uingereza nadhani Jengo la Bunge au ofisi ya Malkia ingejengwa inayoelea angani kwa dola trili. 100.

Watawala ni tofauti sana na viongozi. Tanzania tuna watawala. Watawala wanawaza ufahari na kuwa juu ili waogipwe na kuheshimiwa.

Viongozi wanaonyesha njia ya kutoka kwenye utumwa na unyonge wa jamii. Afrika na Tanzania bado tuna watu wanaopenda kutawala wengine. Mtu anapewa nafasi kwa miaka mitano lakini ukichunguza muda wote huo anachoangalia ni kujenga hofu kwenye jamii ,kujikweza na kuifanya jamii imuogope na kumwona ni mtu wa hali ya juu asiyehojiwa wala kukosolewa wala kulaumiwa . Watawala wanapenda kusifiwa tuu na kuheshimiwa tu hata kwa Lazima.

Hivyo hatutashangaa ikijengwa ofisi kwa mabilioni ya fedha kwenye nchi inatotegemea miamala kujiendesha.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Huwajui CCM au wewe sio wa nchi hii, au ni nini?

Unafikiri wanajali matumizi sahihi ya kodi? Basi jitayarishe, kama umesikia ujue hilo balaa linakuja. Waliuza nyumba zote za serikali muda mfupi kabla ya Rais kumaliza muda wake.

Rais aliyefuata kama kawaida akafanya mabadiliko, wateule wote walikaa mahotelini kwa miaka. Ni mabilioni mangapi yaliyoteketea, kuna anayejali?
 
Aisee, ila hii ofisi kwa bilioni 18 hapana, nasisitiza, waunganishwe na ofisi ya waziri mkuu, hiki cheo kife, awamu ya 6 ndio iwe ya mwisho kubeba huu mzigo! Umakamu wa Rais ni mzigo kwa wanachi!
 
Mkuu hili mbona lipo wazi, kama ni swala la succession plan endapo rais atashindwa kufanya majukumu mbona yupo spika wa bunge na jaji mkuu? mmojawapo anaweza kukaimu madaraka ya rais na uchaguzi kuitishwa katika kipindi cha miezi sita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…