Cheo cha Makamu wa Rais hakina tija, tukiondoe, tubakishe cha Waziri Mkuu

Sahihi kabisa, either Makamu was raisi au waziri mkuu, mmoja apigwe chini na cheo chake kifutiliwe mbali. Hizi mambo za kuweka nafasi nyingi ni kupeana ulaji tu hamna lolote.
 
Ni wazo zuri na nimekuwa nikisema hivyo mara kwa mara. Hakuna kitu cha msingi ambacho ofisi ya waziri mkuu haiwezi kufanya kinachofanywa na ofisi ya makamu wa Rais.

Nchi nyingi zina either ofisi ya waziri mkuu au makamu wa Rais, sio vyote.

Added bonus Rais akifariki madarakani, itabidi uchaguzi ufanyike labda ndani ya miezi mitatu anayegombea kupata (mandate) ridhaa ya wananchi na kuelezea sera zake.

Kufanya haya tunahitaji katiba mpya.
 
Cheo cha Makamu wa Rais ni kwa ajili ya kudumisha tu Muungano na si zaidi ya hapo.

Kwamba Rais akitoka Bara then Makamu lazima atoke Visiwani.

Kiutendaji cheo hicho hakitakiwi ila kwa ustawi wa Muungano, kinafaa.
 
Ni mzigo, kiondoke haraka, hakina tija!!
 
Cheo cha Makamu wa Rais ni kwa ajili ya kudumisha tu Muungano na si zaidi ya hapo.

Kwamba Rais akitoka Bara then Makamu lazima atoke Visiwani.

Kiutendaji cheo hicho hakitakiwi ila kwa ustawi wa Muungano, kinafaa.
Kama ni lazima iwe hivyo, basi ama raisi wa SMZ ndo awe VP au kuwe na serikali 3 sasa, raisi wa JMT ambaye atakuwa anasubiri kudra za partners wa muungano.

Au wawe direct tu kuwa raisi wa JMT ni lazima awe, kwanza ni raisi wa JMT na kwamba, ukiwa hata na kaharufu kwa uvisiwani, hupaswi hata kugombea ukiranja wa darasa huku bara KAMA ilivyo kule.

Vitambulisho vya ukaazi kila pande, marufuku za kutomiliki ardhi iwe ni kwa kila upande. Tukifikia hapo, muungano unajadilika na nafasi za uongozi kadhalika
 
Mmh, huko ni kuvuruga Muungano sasa, cheo kiondoke tu.
 
Hiki cheo cha vice president kifutwe tu hakina kazi. Tangu aingizwe madarakani hakuna lolote lile tumesikia kutoka kwake zaidi ya kwenda airport kumsubiri mama ampokee. Anakula kodi zetu bure tu. Aina hii ya viongozi ni mzigo na hasara kwa taifa, sijui kwanini wasomi wa Bongo akili zao hazileti matokeo chanya kwa taifa.

Huyu ni mwanauchumi wa makaratasi tu lakini utendaji ni zero kabisa, yupoyupo kuinama na kukunja mikono kumsalimia aliyemteua.

Hii safu kwanzia Rais, Makamu wake na waziri mkuu hapa tumepigwa hawafai hata kuwa monitor wa darasa la tatu. Ni unproductive wapo kuzunguka tu kila siku wanawaza kukutana na mzungu hali za wananchi zinazidi kuwa ngumu. Wananchi tusipobadilika kukataa viongozi wachumia tumbo tutaburuzwa maisha yetu yote.
 
Katiba inasemaje kuhusu majukumu ya Vice President? Usimuhukumu bila kuangalia majukumu yake kikakatiba
 
Tatizo Kuna wachezaji wametoka,
Timu imekua mbovu
 
We unajielewa kweli? Makamu wa Raisi hupangiwa kila kitu , ni Kati ya watu ambao ni high power Ila hawana nguvu ya maamuz , hawezi fanya chochote Kwa kujiamulia
 
Kama hawa wanaotegemewa kuwatetea wananchi wakishalamba asali na kunywa juisi ikulu wanakuwa laini hivi. Sasa we mwananchi wa kawaida utafanyaje? Inaonesha wazi kuwa sasa hivi kila mtu anapigania tumbo lake. Iwe kwa viongozi wa serikali au upinzani.
 
Attachments

  • Screenshot_20220605-082514_1.jpg
    159.8 KB · Views: 3
Kama hawa wanaotegemewa kuwatetea wananchi wakishalamba asali na kunywa juisi ikulu wanakuwa laini hivi. Sasa we mwananchi wa kawaida utafanyaje? Inaonesha wazi kuwa sasa hivi kila mtu anapigania tumbo lake. Iwe kwa viongozi wa serikali au upinzani.
Mm sitegemei mbowe wala cdm ktk harakati za kuitafuta justice, ninaamini ktk maandamano tu, finish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…