Cheo cha Makamu wa Rais hakina tija, tukiondoe, tubakishe cha Waziri Mkuu

We unajielewa kweli? Makamu wa Raisi hupangiwa kila kitu , ni Kati ya watu ambao ni high power Ila hawana nguvu ya maamuz , hawezi fanya chochote Kwa kujiamulia
Basi atoke tu, Katiba ifanyiwe amendment arudi chuoni akashike chaki, mshahara wake wa mwezi unalipa zaidi ya walimu Mia moja wa sekondari
 
Naunga mkono hoja.
 
Hii nafasi nilisema apewe Majaliwa ila basi tu watu wabishi mno pale juu.
 
Hicho cheo kilianzishwa kwa ajili wa kuwatawala watu wa Zanzibar, safari hii Mungu ameona sisi wa Bara kuanza kutawaliwa then mnaingiza hasira.
Nyakati za tawala zote watu watu walikua kimya...na sisi tuwe kimya.
Sheria ni msumeno, mama tunae hadi 2030 ndo akili itatukaa sawa na ukoloni mamboleo.
 
Anasubiri litokee kama la 17 March aende front
 
Akili zako hazipo Sawa nenda hospital Sasa hivi
 
Vyeo vipo kugawana ulaji tu,
Jiulize kuna wabunge wangapi kutoka Zanzibar bungeni wakijadili mambo yasiyo ya muungano,
Mfano wanajadili mradi wa maji Bariadi na wanalipwa salary na posho zote,
Angalia idadi ya watu na wabunge wa Zbar
na ukubwa wa eneo,
Na wakati huohuo wana bunge lao(Baraza La Wawakilishi) ambalo hakuna Mtanganyika anayeruhusiwa kuingia humo.
Tunahitaji marekebisho kuboresha Muungano wetu,
 
Kuna yule mwingine alikuwa na koti kuubwa kumbe mfukoni alikuwa anachukua mkasi kazi yake kukata tepe
 
Akili zako hazipo Sawa nenda hospital Sasa hivi
Kama utaki kukubali kuwa cheo Cha Vice President pamoja na hizo job description kwa ajili kuwalambisha watu wa Zenji ni wewe... Ila ukweli ndo hiyo.
Nitajie makamu wa Rais aliewahi kufanya Jambo la maana ili Mimi niwahi Hospitali.
 
Andiko zuri ila ungeweza kuliboresha zaidi. Hakuna muungano wa nchi mbili halafu zikabaki kuwa nchi mbili au moja na serikali mbili, huo ni UNAFIKI. Hapa hamna muungano ni mazingaumbwe na sekeseske za viongozi. Vunja muungano au vunja nchi na serikali ya Zanzibar na kuunda nchi moja na serikali moja ya Tanzania....FULL STOP.
 
Hicho Cheo ni Ceremonial tu ndio maana hata JPM alivokufa, Makamu wake baada ya kusworn in akaanza kulalamika utawala wa JPM kama hakuwa sehemu ya utawala huo hio ina prove kuwa Cheo cha VP kipo tu kusubiri hali ya hatari kama kifo cha incumbent, Lakini naamini ofisi hii ya Vice president imesheheni watu wa kila aina ivo ofisi hii tunaihudumia kwa kodi zetu bila impact yoyote ile, Nashauri Office hii iwe demolished
 
Job desc yake iko wazi, ni nafasi ya kimkakati hasa kwa nchi yetu ya mfumo wa Muungano. Mara nyingi idara yake ni ile ya mazingira! Iko hivyo miaka yote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…