Good morning.....
Angalizo: soma bila jazba inaweza kukukera, ukimaliza mcheki mkeo msonye kupunguza hasira.
Wataalamu wa mambo ya mahusiano wanasema mapenzi kwa mwanaume ni moja kati ya vitu, ila kwa mwanamke mapenzi ni kila kitu, yani kwa mwanamke mapenzi ni maisha. Ndio maana mwanamke unaweza kumkera basi asikupikie, asifanye chochote yani hapo kila kitu kipo connected na hayo mapenzi tofauti na mwanaume. Mwanaume unaweza kuwa na wanawake kadhaa na wanajuana na maisha yanaendelea ila kitendo cha kujua mwanamke wako kuna mtu anasimamia kucha ni pigo sana na usipokua imara unaweza rudi kwa muumba kizembe kizembe.
Bwana kujua mali zako zinaliwa inauma, iwe analiwa mwanaume au analiwa mwanamke inauma, japo wanaume mnajitoaga tu ufahamu mnajikuta mliumbwa na kibali cha kupiga yani nyie mpige tu mkipigiwa inakupa tabu. Cha ajabu ukute umeoa kabisa unajua uchungu wa mke na unaenda kupiga wake za wenzio tena unawapenda ndio mambo yako yani ila eti wako hautaki aguswe hihihihi nacheka kisukuma brother hebu kuwa serious kidogo!!!
Mwanaume anachepuka kwa tamaa tu yani kifupi hana madhara kiiivo tukiachana na wivu wivu tu hana madhara makubwa, labda kuchunwa chunwa tu na vitu vya hapa na pale, ila sasa tukija kwetu viumbe wa kike watu ambao mioyo yetu inashape ya kopa, kopa ndio na mioyo wanaume ina shape ya korosho (tusibishane katika hili π) mwanamke kuchepuka ni hatari kuchepuka sio tu tamaa kuchepuka ni mapenzi tena mapenzi mazito, mahaba ya dhati kabisa, we don't offer mabao tu bali tunajitoa sana hadi hisia tunaweka rehani, yani kuchepuka ni kufall in love kabisa unampa mtu moyo na hisia (micheps msizingue jamani mtatuua) na hapa ndiyo hatari ilipo mwanamke usipohusisha akili nyumba itasambaratika, utaanza kama masihara tu mara unajikuta mme unamuona kama zombie huko kwenye ateri na aota kajaa mchepuko, mchepuke kwa makini na kwa akili jamani
Evelyn Salt (fisi jike)