Chereko chereko ujio Tume Huru ya Uchaguzi

Wajumbe wa kamati ya uteuzi wameteuliwa na Rais.Baadae tena Rais atamteua mwenyekiti wa tume miongoni mwa walioteuliwa na kamati ya uteuz i.sioni tofauti.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app

Kesi ya nyani kula mahindi sasa inatolewa kwa hakimu sokwe anakabidhiwa hakimu ngedere.

Binadamu mtaa wa Jukwani anaruka ruka akitegemea sasa hatimaye haki itatendeka ๐Ÿ˜๐Ÿ˜.
 
Hamna kitu hapo. Shida iko kwenye Katiba.

Tume huru iandaliwe na wanaccm tu? iwe huru?
 
Tume huru iliyojaa watumishi wa serikali . inatakiwa iwe na wajumbe wasio fungamana na upande woowote

Haipo nia njema kutokea kwa watawala waliojipa hadhi ya kuwa watesi wetu. Ingekuwapo nia njema:

1. Kwa nini kuweka vizingiti kwenye kurejelewa kwa mchakato wa katiba bora itakayo tupa taifa lenye usawa, haki, na uhuru kwa wote?
2. Kwa nini kuweka vizingiti kwenye kuwapo tume huru ya uchaguzi itakayo tupa viongozi wanaotufaa zaidi kama sisi wananchi tutakakavyoona inafaa?

Ni vizuri watesi wetu wakajua safari hii tunapenda kuung'oa mzizi wote wa fitina watake wasitake.
 
Punda ni yule yule kabadilishwa soji tu .
 
Hao wote ni ccm, sioni tume huru hapo. Hivi kwa nini wanapenda kuwaona watu hawana akili? Hao majaji wote ni wateuliwa wa rais ambae ni m/kiti wa ccm, hao maspika wote ni wabunge wa ccm, hivi wanafikiri watu ni wajinga Siku zote?
 
Hii ni sawa na kutuliza homa na panadol bila kutibu kinacholeta homa hio๐Ÿ˜…
 
Hiyo sio tume huru, wajumbe wake hawako huru, sababu spika hakupaswa atokane na chama cha siasa, halafu huku chini kinafanyika nini, wakurugenzi hawa bado wanatumika?
Ni tabia ya CCM hata kama watu watu wasio na chama wanapaswa kuomba nafasi kwenye tume, atalazimisha kuweka watu wao!
 
Jaji Makungu sasa ni jaji wa mahakama ya rifaa tanzania.kwa Zanzibar anaekaimu nafasi ya jaji mkuu ni Mh Khamis Ramadhan
 
Jaji Makungu sasa ni jaji wa mahakama ya rifaa tanzania.kwa Zanzibar anaekaimu nafasi ya jaji mkuu ni Mh Khamis Ramadhan

Asante sana kwa update hii ninarejea sasa kufanya marekebisho stahiki. Ndiyo maana nikaweka angalizo la kuitisha nafasi ya maboresho.

Umeona mambo hayo sasa mjumbe mwaminifu kutokea UP - Hapa Kazi tu, bwana johnthebaptist?

Mtoa mada ayajulie wapi haya ya nchi nyingine? Si sawa na kumfahamu jaji mkuu wa Malawi au Burundi?
 
Hatutaki tume huru ya michongo , Tunataka katiba mpya ambayo italeta tume huru, ikiangalia muundo wa hiyo tume huru hapo juu utagundua imejaza watu wa kuteuliwa , majaji michongo na maspika michongo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ