Chid Benz kama Case study: Wasanii wanamichezo wanarogwa sana

Chid Benz kama Case study: Wasanii wanamichezo wanarogwa sana

Ndugu nilichokiandika hapo nina ushahidi nacho 100%. Usidhani hata sasa hakuna wanaojaribu kuniroga.

Yesu yupo kazini mkuu. Wengi wanasikia tu habari zake lakini ni wachache sana wanaoushuhudia UWEZA wake maishani mwao.
All the best mkuu
 
Mkuu nimesoma heading tu sijaenda deep ila nikuulize ni nani pia anawaroga ma-star wote wa huko Ughaibuni ? Ni Wasanii wachache sana ambao baada ya peak wanakuwa juu na ni wachache zaidi ambao unakuta hawaja-abuse drugs n.k.

Mtu bado mdogo, Fame (kila mtu anakujua) madada wanajilengesha, Umezungukwa na machawa na ni partying kila dakika wakati mwingine huna mambo ya kufanya na ukiwa bored kuna party after party after party (unless una management nzuri sana ni rahisi kwenda haywire)

Vilevile ulizoea kila mtu anasimama anakushangaa na kukuomba autograph ukipitwa na wakati hata watu hawakuangalii zaidi ya kukupita (lazima upate stress)....; Like the say Its hard getting on Top but its even harder to maintain the Position

Entertainment industry is evil
 
Na sasahivi ndio imechangamka balaa industry.....madawa ni kama ymaerudi kwa kasi sana mana huko mtaani hakufai kabisaa

Hadi Mondi anatumia ( allegedly)
 
Amevuna alichopqnda hakuna wa kumtupia lawama! Hakuna aliyemroga zaidi ya kujiroga mwenyewe!

Chid Benz alipata nafasi akaichezea na akaona kula madawa ya kulevya ni suluhu sasa amepata matokeo ya matendo yake …ajilaumu mwenyewe hana wakumtupia lawama na hakuna aliyemroga!
 
Aliwahi kusema Ndugu. Haruna Rashid Juma Kahena almaaruf kama Inspekta Haroun kwenye wimbo Ngangari kwamba

" KULONDA KAZI YA MUZIKI UGANGAMALE" ambayo ni maneno ya kizaramo yanayo maanisha " KUTAKA KAZI YA MUZIKI UGANGAMALE"

( KIZARAMO : Kulonda = kutaka).

Hapo Inspekta alikuwa anazungumzia kungangamala katika ulimwengu wa kiroho.

Lazima uwe "MZITO" kama "KABWE" kama asemavyo Joh Makini kwenye wimbo " Niaje Nivipi".

Ukitazama kwa makini hayo maneno ya Babu " KULONDA KAZI YA MUZIKI UGANGAMALE" utakutana na maneno matatu 👇

1. Kulonda = Kutaka.

2. KAZI ya muziki = kazi ya muziki.

3. UGANGA ( male) = hiyo ( male) achana nayo hiyo baki na UGANGA. Male imetumika tu kukupoteza maboya.

Ila ujumbe ni KULONDA+ KAZI YA MUZIKI + UGANGA.

Ili kazi ya muziki uweze kuifanya kwa mafanikio lazima uloge ( uroge?) Lazima utembee kwa waganga. Inspekta alilijua hilo ndio maana alitoa code hiyo kwenye wimbo Ngangari na kama hiyo haitoshi aliyaishi maisha hayo. Ndio maana hata Zay B kwenye wimbo wake Gado remix ( featuring Juma Nature) ngoma ambayo ilikuwa aimed at Inspekta, Zay B anasikika akimwambia Inspekta kwamba " Fani haihitaji uchawi wala kuroga" Ukaribu wake na Inspekta wakati bado wapo kwenye good terms ulimfanya Zay B kujua lifestyle ya Inspekta katika hilo eneo la kiroho..

Wasanii wa muziki na filamu wanaroga na kurogwa sana.

Wachezaji wa mpira wanaroga na kurogwa sana.

Ni rahisi sana kwao kurogwa kwa sababu wanafanya kazi za wazi. Kazi zinazo onekana na watu wakiwemo maadui zao na watu wasio penda maendeleo yao. Tofauti na wewe ambae unafanya kazi ya ofisini au biashara. Sio kwamba hutarogwa, utarogwa but still you can be a little bit invisible from the point of all your enemies observation..

Katika ulimwengu wa kiroho? macho ni adui wa mafanikio.Na katika vitu unavyo takiwa kujikinga navyo ni macho maovu ( evil eyes)

Wasanii wa muziki filamu na wana michezo wanarogwa sana kwa sababu hizo ni tasnia zinazo weza KUBADILISHA maisha ya mtu kufumba na kufumbua.

Msanii/mwanamichezo lazima ajigange haswa..

Nyota ya msanii wa muziki au mwanamichezo kuzimwa ni suala ka kufumba na kufumbua.

Unakumbuka kisa cha Muumini Mwinjuma na yule mzee wa pale Bagamoyo ambae kwa sasa ni Marehemu? Muumini alienda kusimikwa nyota na kugangwa kwa mtu huyo kwa makubaliano kwamba akitoka arejeshe fadhila kwa kulipa kiasi ambacho walikuwa wamekubaliana. Kilicho tokea Muumini baada ya kutoka akamdhulumu yule Mzee. Mzee wa watu akaapa kwamba labda sio yeye na kwamba Muumini haton'gaa tena kimuziki na hicho ndicho kilicho tokea Muumini hajawahi kusimama tena tangu kipindi hicho.

Ali Choki na watu wake walijaribu kuleta vita na yule mmama wa Kigoma mwanasimba lia lia, kilicho wakuta hawawezi kusahau. Kwanza walitwezwa na kufedheheshwa. Wakati beef lipo kwenye tension, Choki aliwahi kuapa kwamba hatorudi tena kwenye hiyo bendi na hatozungumza tena na mama yule hadi anarudi kwa Mola wake lakini miezi kadhaa baadae Choki alirejea kwenye bendi hiyo kwa magoti ambako hata hivyo hakudumu sana now nasikia yupo Mwanza huko..

Hawa machawa wengi mnao waona wengi wao wanapewa uchawa kwa sababu ya uchawi. wana wa link Wasanii wao na wachawi wazito. Yule jamaa mfipa wa Kigoma ambae zamani alikuwaga ana rap na kina Juma Nature wewe muone hivyo hivyo. Ana " watu" ndio maana Wasanii wana muweka karibu.

Mambo ni mengi sana so rahisi kuyaelezea yote but

BACK TO CHID BENZ.

1. Chid Benz anarogwa/ alirogwa...

2. Chid Benz harogi wala hawajui waganga.

3. Chid Benz alikuwa na nyota Kali sana.

4. Chid Benz kiuhalisia ni mtu powa sana na yupo generous sana hasa anapokuwa na nafasi. Ndio maana alivyo kuwa kwenye prime yake alisaidia watu wengi sana.

5. Chid Benz alikuwa anapendwa sana na kupitia kupendwa kwake angeweza kuinuliwa juu zaidi ya nafasi aliyokuwa nayo

Wachawi waliona nyota ya kukubalika kwake. Wakamtupia wadudu ambao wamemfunga kwenye uraibu wa mihadarati...

Nimetazama interview ya Chid Leo nimejisikia kutokwa na machozi kumuona mwamba akiwa katika hali hiyo...

Chid Benz why???
Hakuna kurogwa Wala Nini , hakuna mwanamuziki aliyefakiwa mwishoni mwa maisha yake sababu muziki ni kazi ya kishetani na Haina baraka yoyote.
Mifano ni mingi, bob Marley, Babu sea,Michael Jackson,Gurumo,R Kelly, Lucky dube,Matona ,n.k
 
U have a point
 
Hakuna mtu kamloga Chid Benz.
Kinachomtesa Chidi ni kutotaka kukubali wakati wake wa muziki ulishaisha na hakutumia vizuri wakati wake.
Kama ni madawa kina Darasa waliingia uko lakini walisaidiwa wakatoka na wanaendelea kufanya maisha yao.
Pia Chidi ni mtu anaejipa umuhimu sana kwenye sanaa ya bongofleva kiasi kwamba amekosa discipline hii inamcost sana ashapewa sana second chance watu washampigania sana lakini ni sikio la kufa.
Analaumu kila mtu anataka awe amekaa hapo watu wanamtumia hela aende kuvuta unga kitu ambacho sio kweli...flan niliimbaga nae ila hanipi hela hii ni akili au matope?
Lazima Chidi akubali yeye kwenye mziki kazi ishaisha watu juzi hapa walitaka kumbeba kaandaliwa kila kitu ila ugomvi jeuri ujuaji watu wanamuogopa ni kama unafanya kazi na kibaka huwezi kuwa na amani.
Mungu amsaidie ila kama mama yake kanyoosha mikono juu basi unga na depression soon vitammaliza kabisa.
hujawahi kuuona upande mwingine wa shilingi nzee mwenzangu. wewe unayaona maziwa jamii nzima inaoneshwa kuwa ni maji ya tope.
 
Nguvu kubwa ya kutoka hapo alipo ipo ndani yake ili urogwe lazima ukubali kuruhusu Giza ndani yako.

Pia kanuni za mafanikio huwa zipo wazi na kanuni za kujilinda zipo wazi

Neno honest na neno vision
Uaminifu na Kuwa na maono hivi vitu ukivizangatia lazima utaukataa uharibufu ,pombe ,madawa n.k maana utakuwa unaiwaza kesho yako iliyojengeka kiuimara.
 
Hakuna mtu kamloga Chid Benz.
Kinachomtesa Chidi ni kutotaka kukubali wakati wake wa muziki ulishaisha na hakutumia vizuri wakati wake.
Kama ni madawa kina Darasa waliingia uko lakini walisaidiwa wakatoka na wanaendelea kufanya maisha yao.
Pia Chidi ni mtu anaejipa umuhimu sana kwenye sanaa ya bongofleva kiasi kwamba amekosa discipline hii inamcost sana ashapewa sana second chance watu washampigania sana lakini ni sikio la kufa.
Analaumu kila mtu anataka awe amekaa hapo watu wanamtumia hela aende kuvuta unga kitu ambacho sio kweli...flan niliimbaga nae ila hanipi hela hii ni akili au matope?
Lazima Chidi akubali yeye kwenye mziki kazi ishaisha watu juzi hapa walitaka kumbeba kaandaliwa kila kitu ila ugomvi jeuri ujuaji watu wanamuogopa ni kama unafanya kazi na kibaka huwezi kuwa na amani.
Mungu amsaidie ila kama mama yake kanyoosha mikono juu basi unga na depression soon vitammaliza kabisa.
Umemaliza yote mkuu.

Unga,,akili imeshavurugika kwa ufupi ni teja kwa sasa,,kumsaidia tena wakati hujamaliza shida ya kuathirika kwa madawa ni ngumu Ray C yuko wap?????????? Unga, bangi ni hatari sana.
 
pole kwa kuguswa na chidi mpaka kutaka kutokwa na machozi, Ila kalapina kamsaidia kumtoa naona imeshindikana kuachana na madawa.
Unamuachisha mtu madawa kwa kumbembeleza...lazima adeke
Yule wamuache akiwa serious atakuja aacha mwenyewe
Wampotezee tu

Ova
 
Huwezi toboa kwenye sanaa iwe muziki filamu bila kuuza nafsi yako.
Sale your soul die young
 
Ukirooga ni lazima urogwe hakunaga mshindi kwenye fani ya ndumba
 
Mkuu nimesoma heading tu sijaenda deep ila nikuulize ni nani pia anawaroga ma-star wote wa huko Ughaibuni ? Ni Wasanii wachache sana ambao baada ya peak wanakuwa juu na ni wachache zaidi ambao unakuta hawaja-abuse drugs n.k.

Mtu bado mdogo, Fame (kila mtu anakujua) madada wanajilengesha, Umezungukwa na machawa na ni partying kila dakika wakati mwingine huna mambo ya kufanya na ukiwa bored kuna party after party after party (unless una management nzuri sana ni rahisi kwenda haywire)

Vilevile ulizoea kila mtu anasimama anakushangaa na kukuomba autograph ukipitwa na wakati hata watu hawakuangalii zaidi ya kukupita (lazima upate stress)....; Like the say Its hard getting on Top but its even harder to maintain the Position
ndio maana namuona diamond anajitahidi sana asishuke chini, ulichosema ni sahihi 100%, ugopa sana kushuka level flani , lazima upate stress.
 
Back
Top Bottom