Chief Mangungo 2.0 na Ujinga wa Mwafrika 2013..

Chief Mangungo 2.0 na Ujinga wa Mwafrika 2013..

1.Kwa hiyo wewe unataka tuendelee kuwa na Bunge dhaifu milele? Lazima ifikie hatua kwamba wabunge watumie wataalam, kama wao hawana taruma husika katika kufanya maaamuzi ya mambo mhimu ya kifaifa.(Hao kina EMT, wanaweza kuajiriwa na bungeni kutoa hizo huduma na kuwashauri hao wabunge wasio na hizo elimu).

Kati ya

Mimi ninayetaka mikataba iwe public wabunge wapate challenge kutoka kwa general public kushughulikia sehemu zenye matatizo yatakayowekwa wazi.

Na,

Wewe unayetaka bunge ligeuke kuwa baraza wa makarani wa kupitia mikataba.

Nani anataka wabunge wawe dhaifu?

Hatujawapeleka wabunge bungeni wakawe makarani pale. Kama habari ya ku sort kuangalia redflags inaweza kufanywa JF kwa nini mbunge mwenye mambo mengi nyeti aanze from scratch kusoma mkataba wakati tunaweza ku dedicate taasisi ya ma watchdog tu itakayo filter mambo na ku raise yale yenye utata tu?

Utasemaje wabunge watumie wataalam halafu ukatae mikataba isiwe public? Wataalam wenyewe si ndio wako kwenye public?

Hata kama tuna bunge lililojaa wataalam, kuna ubaya gani kuongeza wigo wa wataalam watakaoangalia haya mambo? Kwa nini tujilimit na wataalam walio bungeni tu ambao hata kama hakuna illiterates humo bungeni ni mia kadhaa tu? Out of the millions of Tanzanians?

Kwa nini una assume wakina EMT wanataka kuajiriwa bungeni? Unajuaje kwamba EMT hana practice yake iliyo rewarding, akataka tu kutumia expertise yake hapa JF kuchambua mikataba jioni akirudi nyumbani? Participatory democracy without leaving his home? Anachambua vitu, mbunge anakuja kusoma hapa, kesho anaverify na staff wake, keshokutwa mnavisikia kwenye bunge.

Huoni tutatumia resources zetu vizuri zaidi badala ya kutegemea a couple of hundred overworked MPs wapitie kila kitu wao tu?
 
This is just an advocacy. Hai prove kitu chochote katika ku support your point.

But ime make some serious, sober, balanced, supported points towards supporting transparency. Points ambazo hujazijibu.

Halafu contrary na ulivyotaka tuamini kwamba ni watu wasio na uzoefu tu na mambo haya ndo wanataka transparency, hayo maandishi yanatuonyesha kwamba mpaka world class institutions zina support transparency na wataalam wanasema this is the trend of the future, we might as well start early and reap the benefits of being early adopters as opposed to being "Johnny come lately" all the time.

Hujakatazwa kusema hii ni advocacy tu, tuonyeshe hivyo. Huwezi ku dispute vitu by a fiat statement if you want to be taken seriously.
 
Kati ya

Mimi ninayetaka mikataba iwe public wabunge wapate challenge kutoka kwa general public kushughulikia sehemu zenye matatizo yatakayowekwa wazi.

Na,

Wewe unayetaka bunge ligeuke kuwa baraza wa makarani wa kupitia mikataba.

Nani anataka wabunge wawe dhaifu?

Hatujawapeleka wabunge bungeni wakawe makarani pale. Kama habari ya ku sort kuangalia redflags inaweza kufanywa JF kwa nini mbunge mwenye mambo mengi nyeti aanze from scratch kusoma mkataba wakati tunaweza ku dedicate taasisi ya ma watchdog tu itakayo filter mambo na ku raise yale yenye utata tu?

Utasemaje wabunge watumie wataalam halafu ukatae mikataba isiwe public? Wataalam wenyewe si ndio wako kwenye public?

Hata kama tuna bunge lililojaa wataalam, kuna ubaya gani kuongeza wigo wa wataalam watakaoangalia haya mambo? Kwa nini tujilimit na wataalam walio bungeni tu ambao hata kama hakuna illiterates humo bungeni ni mia kadhaa tu? Out of the millions of Tanzanians?

Kwa nini una assume wakina EMT wanataka kuajiriwa bungeni? Unajuaje kwamba EMT hana practice yake iliyo rewarding, akataka tu kutumia expertise yake hapa JF kuchambua mikataba jioni akirudi nyumbani? Participatory democracy without leaving his home? Anachambua vitu, mbunge anakuja kusoma hapa, kesho anaverify na staff wake, keshokutwa mnavisikia kwenye bunge.

Huoni tutatumia resources zetu vizuri zaidi badala ya kutegemea a couple of hundred overworked MPs wapitie kila kitu wao tu?

Ok, Kilanga, You have convinced me.

How do you make it happen??? in Tanzania?
 
But ime make some serious, sober, balanced, supported points towards supporting transparency. Points ambazo hujazijibu.

Halafu contrary na ulivyotaka tuamini kwamba ni watu wasio na uzoefu tu na mambo haya ndo wanataka transparency, hayo maandishi yanatuonyesha kwamba mpaka world class institutions zina support transparency na wataalam wanasema this is the trend of the future, we might as well start early and reap the benefits of being early adopters as opposed to being "Johnny come lately" all the time.

Hujakatazwa kusema hii ni advicacy tu, tuonyeshe hivyo. Huwezi ku dispute vitu by a fiat statement if you want to be taken seriously.

I have bought your urgument. With some extra reading down there.But It will take time for reality.

World Bank contract details to be published online in transparency push | Global development | guardian.co.uk
 
Ok, Kilanga, You have convinced me.

How do you make it happen??? in Tanzania?

Emma, nafikiri kuna point hapa ya msingi na nadhani kuna haja ya kutengeneza balance fulani.

a. The right of public to know what their government is doing. Msingi wa hoja yangu hapa ya Mangungo ndio hili hasa. Je wananchi wanahaki ya kujua kile ambacho serikali yao inafanya. Je serikali inaweza kufanya mambo kwa siri bila wananchi kujua.

b. Je, fedha za umma zinaweza kutumiwa kwa siri na serikali. Kama jibu ni ndiyo tujiulize wanaweza kutumia wapendavyo bila kuulizwa? Kama jibu ni hapana tujiulize tufanye nini ili serikali isitumie fedha za umma kwa siri?

c. Je wananchi wana haki ya kujua serikali inafanya nini na ardhi na maliasili yao? Je serikali inaweza kuuza kipande cha nchi kwa taifa jingine au kampuni ya kigeni bila wananchi kujua 'terms of sale". Mangungo aliposaini mkataba na Karl Peters sidhani kama alikuwa anajua anatoa sehemu ya ardhi yake kwa Ujerumani!

Nitakupa mfano mmoja mzuri sana. Kuna kampuni ya kiarabu miaka kama miwili au mitatu iliyopita iliamua kununua eneo kubwa la ardhi nchini ili kupanda mpunga. Mradi huo kwa juu juu ulionekana kusaidia kupunguza tatizo la chakula. Lakini kumbe mkataba wenyewe - ambao nilibahatika kuuona - ulikuwa unaweka sharti kuwa kiasi kikubwa cha mpunga utakaozalishwa ni kwa ajili ya soko la nchi hiyo ya Kiarabu. Kwa haraka haraka unaweza ukasema sawa tatizo ni kuwa kama tanzania inapata ukame na tatizo kubwa la njaa kampuni hiyo hailazimishwi kusupply soko la ndani bali itaendelea kuuza nje - kwa sababu Mkataba umesema hivyo.

Sasa nijaribu kujibu swali la tufanye nini.

a. Kuna haja ya kubadili sheria ya procurement (PPA) ili iakisi haki ya wananchi (moja kwa moja na kupitia wabunge wao kujua mikataba ya umma).

b. Pamoja na PPA, regulations za PPA nazo ziwekwe wazi ili kuweka muongozo wa mikataba ya umma. Kwa mfano kuna vitu ambavyo mikataba ya umma isiweze kufanya au vipengele ambavyo havitakiwi kuwemo. Kwa Wamarekani kwa mfano Wizara ya Ulinzi inatakiwa itangaze tenda zote inazotoa kila siku endapo tenda hizo zinazidi tola milioni sita hivi!

Kwetu tunaweeza tukaamua na kusema:

a. Mikataba yote ya madini au nishati ambapo inashirikisha makampuni ya nje na yenye thamani isiyopungua dola milioni 20 ni lazima iridhiwe na Bunge baada ya makubaliano ya vyombo husika.

b. Mikataba yote ambayo inahusu ukodishaji wa ardhi kwa kampuni ya kigeni na ardhi yenye ukubwa unaozidi ekari 500 ni lazima iridhiwe na Bunge na hasa ambayo inahusisha kuhamisha wananchi.

n.k

ni mifano tu hiyo.

KUbwa ni kuwa wananchi ni lazima wawe na sauti katika miradi mikubwa. Juzi hapa eneo la jirani wamekataa kampuni ya Walmart kujenga soko lake kubwa kwenye eneo ambalo linamilikiwa na kanisa. Na walioamua hivyo ni wananchi wenyewe kwenye mashauriano. Japo Walmart ingekuja ingeleta ajira, n.k n.k lakini wananchi waliona kuwa faida hizo hazivutii. Serikali ingeweza kutoa eneo hilo na kuli-zone kwa ajili ya biashara bila kushirikisha wananchi.
No New Walmart for Southfield | News - Home

Fikiria kama sheria ingesema kuwa mradi wowote uchimbaji wa madini au gesi ni lazima uridhiwe na wananchi ambao wataathirika na mradi huo na lazima ifanye public hearing ya kutosha unafikiri si yaliyotokea Mtwara yangeweza kuepukika kwa kiasi kikubwa.
 
Ok, Kilanga, You have convinced me.

How do you make it happen??? in Tanzania?

"Power concedes nothing without a demand. It never did and it never will. Find out just what any people will quietly submit to and you have found out the exact measure of injustice and wrong which will be imposed upon them, and these will continue till they are resisted with either words or blows, or both. The limits of tyrants are prescribed by the endurance of those whom they oppress."

-Frederick Douglass
American slave, Abolitionist, Lecturer, Author and Statesman, 1817-1895

[h=1][/h]
 
Emma, nafikiri kuna point hapa ya msingi na nadhani kuna haja ya kutengeneza balance fulani.

a. The right of public to know what their government is doing. Msingi wa hoja yangu hapa ya Mangungo ndio hili hasa. Je wananchi wanahaki ya kujua kile ambacho serikali yao inafanya. Je serikali inaweza kufanya mambo kwa siri bila wananchi kujua.
b. Je, fedha za umma zinaweza kutumiwa kwa siri na serikali. Kama jibu ni ndiyo tujiulize wanaweza kutumia wapendavyo bila kuulizwa? Kama jibu ni hapana tujiulize tufanye nini ili serikali isitumie fedha za umma kwa siri?

c. Je wananchi wana haki ya kujua serikali inafanya nini na ardhi na maliasili yao? Je serikali inaweza kuuza kipande cha nchi kwa taifa jingine au kampuni ya kigeni bila wananchi kujua 'terms of sale". Mangungo aliposaini mkataba na Karl Peters sidhani kama alikuwa anajua anatoa sehemu ya ardhi yake kwa Ujerumani!

Nitakupa mfano mmoja mzuri sana. Kuna kampuni ya kiarabu miaka kama miwili au mitatu iliyopita iliamua kununua eneo kubwa la ardhi nchini ili kupanda mpunga. Mradi huo kwa juu juu ulionekana kusaidia kupunguza tatizo la chakula. Lakini kumbe mkataba wenyewe - ambao nilibahatika kuuona - ulikuwa unaweka sharti kuwa kiasi kikubwa cha mpunga utakaozalishwa ni kwa ajili ya soko la nchi hiyo ya Kiarabu. Kwa haraka haraka unaweza ukasema sawa tatizo ni kuwa kama tanzania inapata ukame na tatizo kubwa la njaa kampuni hiyo hailazimishwi kusupply soko la ndani bali itaendelea kuuza nje - kwa sababu Mkataba umesema hivyo.

Sasa nijaribu kujibu swali la tufanye nini.

a. Kuna haja ya kubadili sheria ya procurement (PPA) ili iakisi haki ya wananchi (moja kwa moja na kupitia wabunge wao kujua mikataba ya umma).

b. Pamoja na PPA, regulations za PPA nazo ziwekwe wazi ili kuweka muongozo wa mikataba ya umma. Kwa mfano kuna vitu ambavyo mikataba ya umma isiweze kufanya au vipengele ambavyo havitakiwi kuwemo. Kwa Wamarekani kwa mfano Wizara ya Ulinzi inatakiwa itangaze tenda zote inazotoa kila siku endapo tenda hizo zinazidi tola milioni sita hivi!

Kwetu tunaweeza tukaamua na kusema:

a. Mikataba yote ya madini au nishati ambapo inashirikisha makampuni ya nje na yenye thamani isiyopungua dola milioni 20 ni lazima iridhiwe na Bunge baada ya makubaliano ya vyombo husika.

b. Mikataba yote ambayo inahusu ukodishaji wa ardhi kwa kampuni ya kigeni na ardhi yenye ukubwa unaozidi ekari 500 ni lazima iridhiwe na Bunge na hasa ambayo inahusisha kuhamisha wananchi.

n.k

ni mifano tu hiyo.

KUbwa ni kuwa wananchi ni lazima wawe na sauti katika miradi mikubwa. Juzi hapa eneo la jirani wamekataa kampuni ya Walmart kujenga soko lake kubwa kwenye eneo ambalo linamilikiwa na kanisa. Na walioamua hivyo ni wananchi wenyewe kwenye mashauriano. Japo Walmart ingekuja ingeleta ajira, n.k n.k lakini wananchi waliona kuwa faida hizo hazivutii. Serikali ingeweza kutoa eneo hilo na kuli-zone kwa ajili ya biashara bila kushirikisha wananchi.
No New Walmart for Southfield | News - Home

Fikiria kama sheria ingesema kuwa mradi wowote uchimbaji wa madini au gesi ni lazima uridhiwe na wananchi ambao wataathirika na mradi huo na lazima ifanye public hearing ya kutosha unafikiri si yaliyotokea Mtwara yangeweza kuepukika kwa kiasi kikubwa.

Mwanakijiji,

Ninakubaliana na wewe Swala la threshold, katika maamuzi ya mda mrefu yenye adhari kitaifa ni mhimu sana.Ingawaje kilanga anakuja na point nzuri lakini solution nzuri mimi ninaamini ni Bunge.
sheria ya ardhi ya sasa inawapa nguvu wanakijiji. Lakini tatizo kubwa (Prior and Informed Consent) haisaidii sana kwasababu Viongozi wa kijiji wamekuwa wara rushwa sana. Kwahiyo mwekezaji anapotembeza pesa nzuri, umaaana wa Prior and Informed consent unapotea.
Pili serekali inapotoa maeneno makubwa ya ardhi, mara nyingi unakuta sio maeneo ya makazi, kwahiyo applicability ya (Prior Informed Consent inapotea by default.
Ndio maana ninaona Bunge bado ni sehemu nzuri sana ya kuweza kutatua hili tatizo.
 
There needs to be more transparency in the way the government operates.

And in my opinion that need should evident to everyone.
 
Kwa sheria ya Ardhi ya sasa inawapa nguvu wanakijiji.

Ndio na siyo; ndiyo kwa maana bado kuna mchakato wa kuwahusisha wanakijiji lakini maamuzi yote ya wanakijiji yanaweza kuwa overulled na Rais kwani Rais ndiye anayeshikilia ardhi yote dhamana - hata ile ya kijiji!

Ndio maana ninaona Bunge bado ni sehemu nzuri sana ya kuweza kutatua hili tatizo.

Binafsi ningependa iwe tofauti kidogo na hapa niko more influenced na utaratibu wa Marekani na nadhani hata UK ipo. Bunge liwee na uwezo wa kunullify mkataba au Rais. Kwa mfano, Rais Obama hapa mwaka jana tu amesitisha mkataba wa kampuni binafsi kwa maslahi ya taifa. Ulikuwa ni mkataba wa Wind Farms huko Oregon. Sababu ya kusitisa mkataba huo ni kuwa ulikuwa ufanyike karibu na kituo cha kijeshi cha Navy.

Lakini pia Wamarekani wana chombo kinachoitwa Committee on Foreign Investments in the United States chini ya Treasury.. sasa tunaweza kuwa na chombo kama hicho vile vile ambacho kitakuwa na jukumu la kuridhia na kupitia mikataba yote ya uwekezaji ambayo inaweza kugusa suala la Usalama wa Marekani. Mara nyingi ile inayohusiana na energy, security n.k

Fikiria kwa mfano Mkataba wa Meremeta kule Buhemba umefanyika karibu na kambi ya kijeshi na inadaiwa kuhusisha JWTZ nani alipitia mkataba ule? Hakuna. Leo hii Buhemba yamebakia mashimo tu...
 
Uwezo wa ku- nullify Mkataba ni kitu kizuri lakini inabidi uwe very detailed na uelezee circumstances zitakazo qualify the nullification. Tatizo nchi zetu hizi haziaminiki na wawekezaji na ndio maana unatakiwa kuwa na balanced approach ili usionekane huna legal certainity.

Kuwa na kamati under wizara ya Fedha, Inaweza kusaidia lakini swali ni compostion ya hiyo team.Na access ambayo bunge linaweza kuwa nayo ya ku probe hii team.

Modernising Usalama wa Taifa is another area we need to look at. Maana kwa nchi kama Marekani na Uingereza Isuue zote za kiuchumi ni maswala ya National security. Na ndio maana hata waziri wa fedha wa Marekani ni member wa National security Council. (Tanzania need good Economic Intelligence itakayo- cover hata hizi areas za Mikataba)
 
Mkuu Mwanakijiji,

Ujinga wa wakti ule ulikuwa ni mkubwa kwelikweli maana Karl Peters aliandikishana mkataba na machifu wetu hao ndani ya wiki tatu akawa amemaliza.

Kuna mmoja wa machifu alikubali ndani ya mkataba kwamba hamtambui Sultan wa Zanzibar ingawa kwa wakati ule yeye ndie aliekuwa kiongozi wa pwani yote tuionayo leo.

Na cha kuchekesha zaidi nimenukuu sehemu ya mkataba wa chifu Mangungo wa Msovero na Karl Peters kama ifuatavyo:

Mwanzo wa kunukuu:-

"Treaty of eternal friendship :Mangungo, Sultan of Msovero in Usambara, offers all his
territory with all its civil and public appurtences to Dr. Carl Peters as the representative of
the society for German colonization for exclusive and universal utilization for German colonisation"-
mwisho wa kunukuu.

Fikiria mtu anasema "eternal friendship" yaani urafiki wa milele, na baada ya mambo haya tunaweza kabisa kusema kwamba hii ilikuwa ni "beginning of the end" kwa watanganyika.

Ujinga wa baadhi ya wale wanaokabidhiwa dhamana ni wa kushindwa kuchambua na kuona tofauti ya pumba na mchele.

Uwezo wa ku- nullify Mkataba ni kitu kizuri lakini inabidi uwe very detailed na uelezee circumstances zitakazo qualify the nullification. Tatizo nchi zetu hizi haziaminiki na wawekezaji na ndio maana unatakiwa kuwa na balanced approach ili usionekane huna legal certainity.

Kuwa na kamati under wizara ya Fedha, Inaweza kusaidia lakini swali ni compostion ya hiyo team.Na access ambayo bunge linaweza kuwa nayo ya ku probe hii team.

Modernising Usalama wa Taifa is another area we need to look at. Maana kwa nchi kama Marekani na Uingereza Isuue zote za kiuchumi ni maswala ya National security. Na ndio maana hata waziri wa fedha wa Marekani ni member wa National security Council. (Tanzania need good Economic Intelligence itakayo- cover hata hizi areas za Mikataba)

Emma sidhani kama tunaweza kuweka details zote za jinsi hili linaweza kufanyika. La msingi na la maana ni kuweka perimeters za nini hakipaswi kufanyika. Nimepitia sheria yenu hapo Uingereza ambayo imeweka regulations za public procurement. Iko very detailed na compliance ni muhimu na lazima. Na sisi kuna vitu tunapaswa kuvifanya hasa kwa sababu tayari tunajua tuna tatizo la ufisadi katika tenda.

Lakini jambo jingine naamini na kubwa zaidi na ambalo naliona pia kwenye hiyo hoja yako ni kuwa sisi tunatakiwa kuwaridhisha wawekezaji. Kwamba, tutengeneze mazingira ili wawekezaji wasije kuacha kuwekeza nchini. Sasa hili ni zuri kwa kiasi kama wewe ni mwekezaji lakini kama wewe ni mwananchi nani anakuwekea mazingira mazuri usinyonywe au kudhulumiwa.

Matokeo yake ni kuwa tumetoa nafasi kwa wawekezaji at the expense of our own people ... hence the Mangungo 2.0 conundrum.
 
Pia mkuu Mwanakijiji,

Suala la mikataba inayofanywa baina ya serikali yetu na kampuni za nje ni tofauti kabisa na mikataba ambayo inafanywa ndani ya hizo nchi zilizoendelea kuanzia China, USA UK France na kwingine.

Masuala ya usiri huwa yamo na inategemea "capacity" na "interest" za mikataba hiyo kwa kila upande kutegemea na ufuasi wa kampuni kwa serikali iliyopo madarakani. Lakini siku zote maslahi ya wananchi kufahamu kinachoendela huwa yanawekwa mbele.

Nitatoa mifano miwili kuhusu mikataba ambayo mpaka sasa Tanzania imeingia na hatujafahamishwa inagharimu kiasi gani na mchanganuo wake umekaaje.

Jana kutwa katika moja ya globu za jamii kuna picha inayoonyesha mradi uliozinduliwa na raisi Kikwete wa kujengwa kwa uwanja wa ndege wa Kigoma na mwakilishi wa benki ya Dunia akiwepo hapo.

Mwandishi kwa kuwa amejaa ushabiki wa kisiasa na shamrashamra za sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM ameshindwa kuwaeleza wasomaji wa globu yake kwamba mradi ule umegharimiwa na Benki ya Dunia na mwakilishi wao ndie aliekuwa na raisi.

Hali hiyo ipo katika ukaguzi wa ujenzi wa daraja la mto Malagalasi na hakuna taarifa zaidi kuhusu hii miradi kwamba gharama zake zinafadhiliwa na vyanzo gani ingawa kuna wakorea ambao ndio wanasimamia.

Ikiwa hii ni mikopo na tumeingia mikataba nayo na haijulikani mikopo hii inagharimu miaka mingapi na italipwa kwa namna ipi, hii ni hatari- period.

Nchi za wenzetu walioendelea ni nadra sana kuona mtu anaegombea nafasi ya kuongoza nchi akiwa na timu ya watu wa fani tofauti tofauti za usanii.
 
Emma sidhani kama tunaweza kuweka details zote za jinsi hili linaweza kufanyika. La msingi na la maana ni kuweka perimeters za nini hakipaswi kufanyika. Nimepitia sheria yenu hapo Uingereza ambayo imeweka regulations za public procurement. Iko very detailed na compliance ni muhimu na lazima. Na sisi kuna vitu tunapaswa kuvifanya hasa kwa sababu tayari tunajua tuna tatizo la ufisadi katika tenda.

Lakini jambo jingine naamini na kubwa zaidi na ambalo naliona pia kwenye hiyo hoja yako ni kuwa sisi tunatakiwa kuwaridhisha wawekezaji. Kwamba, tutengeneze mazingira ili wawekezaji wasije kuacha kuwekeza nchini. Sasa hili ni zuri kwa kiasi kama wewe ni mwekezaji lakini kama wewe ni mwananchi nani anakuwekea mazingira mazuri usinyonywe au kudhulumiwa.

Matokeo yake ni kuwa tumetoa nafasi kwa wawekezaji at the expense of our own people ... hence the Mangungo 2.0 conundrum.

Unfairness kwa watanzania tunairuhusu sisi wenyewe.Mfano mzuri ni issue ya Bandari pale mtu anachomoa kipengere cha sheria kinachomtaka mjenzi kufanya after sales services free.

PILI:Kama tukiweza kusimamia sheria zetu tu tunazozitunga, Mangungo 2.0 Itakuwa sio tatizo. Mfano wa pili, Tumetunga sheria ya kuyataka makampuni ya simu yajiandikishe kwenye soko la mitaji la Dar Es Salaam, lakini hadi leo jiiii.Kwahiyo ni swala kuwa na udhubutu!!. Hata kama ukiwa na Uwezo wa Kunulify, kama watu unawaowapa hiyo nguvu hawako tayari kusimamia misingi ya UKWELI, wata nulify hizo contract ili wawape rafiki zao na haitakuwa kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa.

Wawekezaji hawana tatizo;sisi ndio tuna matatizo, wanachofanya wanatumia tu matatizo yetu kujinufaisha.
 
Ni kweli na ndio maana nasema upande mwingine ni hawa watawala ndio wenye kubeba lawama. sijui kama umepata nafasi ya kusoma mikataba ya Richmond au ile ya Airbus 320 na ya Dash 8; au mikataba ya ununuzi wa magari ambayo kina Mataka wa ATCL waliingia... imeandikwa na watu wenye akili lakini imeandikwa kwa makusudi kuwa ilivyo. Sasa bila kuweka kanuni za kuongoza serikali inapoingia mikataba na zikawa kanuni zenye kulinda nchi na maslahi yake wawekezaji tutaweza vipi kulinda maslahi yetu?

Lakini Bw. Tayari swali dhahiri ni hili tunaweza vipi kuwakatalia wawekezaji wanapokuja na masharti ya kutubana wakitishia kuwa tusipokubali wanaenda nchi nyingine?
 
In the other parts of the word, transparency ya mikataba inaongezeka, albeit from a low base and poor historical record hasa kwenye sekta ya madini. The tide is gradually turning with more and more data being put online.

Trend inaonyesha kuwa baadhi ya nchi zimeanza kuweka hadharani mikataba wanayosaini baina yao na makampuni ya kimataifa ya mafuta. Tayari kuna nchi kama saba hivi zinazozalisha mafuta ambazo zinaweka hadharani mikataba yao ya mafuta na makampuni ya kigeni. Kuweka hii mikataba hadharani kunawasaidia wananchi kujua kinachoendelea.

Nimesoma baadhi ya wanaopendekeza kuwa bunge liwe linapitia presumably draft za hiyo mikataba kabla ya kusainiwa. Baadhi ya nchi kama Ghana na Sierra Leone zinafanya hivyo. Hata hivyo ili hiyo process iwe effective itategemea na uelewa wa wabunge tulionao. Otherwise, tutakuwa tunahamishia tatizo from one organ to another.

Kuna mikataba mingine inafikia mpaka zaidi ya kurasa 100 na imeandikwa in complicated legal jargons na concepts za sekta husika kiasi kwamba hata mtu anayejua sheria au aliye-specialise kwenye sekta husika may fail to pick up or even understand. Kwa jinsi bunge letu linavyofanya kazi sasa, watakuwa wanaipitisha hii mikataba kwa ushabiki wa vyama. Who knows hata hayo makampuni ya madini yanaweza kuwahonga wale wabunge ambao hawatosheki.

Ni vigumu ku-justfy why the agent (government) should be entitled to hide those contracts from the principal (citizens). Kunaweza kuwa na excuses nyingine kama confidentiality na kulinda trade secrets za other party to the contract ambaye mara inakuwa ni kampuni, but those secret parts can easily be excluded from the published copy anyway.

In addition, the fact that most of the mining companies are public companies, you can easily access the so called confidential information and trade secrets in their prospectus, at the listing authority or even at the patent office.

Lakini pressure ya kutoweka hadharani hiyo mikataba inatoka kwa hayo makampuni because they don't want people to see the tax breaks agreed in those secret contracts. It is a naked truth that multinational mining companies seeking to invest or expand their investment in Africa continue to enter confidential agreements with governments to acquire special tax rates and concessions that are outside the statutory framework.

Kwa kawaida, tax concessions huwa zinakuwa included kwenye mining development agreement. These are legal commercial contracts and override national law. So, if these agreements include tax rates, they override the national tax regime. Kwa hiyo, argument ya trade secrets, tena kwa makampuni ya madini, ni danganya toto tuu maana hata hizo secrets, kama kweli zipo, bado zinaweza kugunduliwa through reverse engineering.

Hata hivyo, pamoja na ukosefu wa transparency kwenye mikataba ya madini, there is a more fundamental problem. Kuna sehemu Dr Peter Kafumu, mmoja wa wataalamu wetu kwenye hii sekta, ameandikwa akidai kuwa "we have no capacity to look at their books. [The companies] can write the books so that third world countries cannot regulate. Even the contracts are difficult. I think the mining companies exploit our weaknesses in law and capacity." – TWN Africa, et al, (2009) Breaking the Curse: How Transparent, Taxation and Fair Taxes can turn Africa's Mineral Wealth into Development.

Lakini uki google wala haitakuchukua dakika 20 kujua kuwa annual reports za kampuni ya AngloGold inayochimba dhahabu Geita zinasema kuwa mwaka 2006, kampuni hiyo ilichimba ounces 308,000 za dhahabu. Kati ya mwaka 2006 hadi katikati ya mwaka 2007 kampuni hiyo ilitengeneza gross profit ya dola za kimarekani milioni 93 kutoka machimbo ya Geita peke yake. Lakini kampuni hiyo ililipa TRA dola za Kimarekani milioni moja tuu kama corporate income tax na kudai kuwa italipa tena corporate tax only in 2011, a whole 11 years baada ya kuanza operations.

Pia Barrick Gold iliripoti a net income ya dola za Kimarekani milioni 97 kati ya mwaka 2004 na katikati ya mwaka 2007, lakini ilikuwa bado haijaanza kulipa corporate incone tax. Kwa kipindi hicho, royalty payments ndiyo zilikuwa our main source of income. Kati ya 2002 and 2006, makampuni ya madini yalipeleka nje dhahabu yenye dhamani ya dola za Kimarekani bilioni 2.9. Katika kipindi hicho, serikali ilikusanya dola za Kimarekani milioni 17.4 tuu kwa mwaka in royalties, charged at 3% of the net back value of gold exports.

Hapa ni nani wa kulaumiwa? Kweli sheria zetu na capacity tuliyonayo inaweza kutufanya tusiweze kuangalia the books of these public companies? Juzi tuu Barrick yenyewe ndiyo iliripott kuwa ime-renew leseni yake kwa miaka mingine 15. Lakini hii habari ilipita kimya kimya kwenye vyombo husika Tanzania. Sembuse utakuwa huo mkataba mpya?

Pia Dr Peter Kafumu ananedelea kudai kuwa negotiating with the mining companies was an intimidating experience, much like being faced with a traditional weapon: "The companies are holding a panga by the handle and we are getting the sharp end."

Kama wanao-negotiate on our behalf ni watu kama hawa, hata kama hiyo mikataba ikiwekwa hadharani itasadia kweli? Kwa nini a Ph.D holder na mtaalamu aliyebobea kwenye sekta ya madini anakuwa intimidated by these mining companies?

Kiini cha tatizo hakipo tuu kwenye kuficha hiyo mikataba bali ni incompetence, ubnafsi and probably woga wa hao wanao negotiate na kusaini hiyo mikataba kwa niaba yetu. Incompetence, ubnafsi, nk. unasababishwa na sisi wenyewe kutowawajibisha wahusika.

Hata kama hiyo mikataba ikianikwa hadharani kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kuingia kwenye mikataba mibovu kama hatutajirekebisha. Maana hata kule WTO, trade negotiators wa nchi zilizoendelea sometimes huwa wana walalamika kuwa Waafrika tunapeleka negotiators ambao hawana expertise with the issues subject to negotiations.

BTW, wala siyo hiyo mikataba tuu ambayo inafichwa maana serikali pia imegoma kuonyesha Mitaala ya Elimu hapa nchini. Tanzania ni member wa Open Government Partnership lakini tunaficha mpaka Mitaala ya Elimu hapa nchini? Tell me about that.
 
Mkuu wangu hapo kwenye rangi sina tatizo na hilo ikiwa bei ya kuwauzia itaamuliwa na soko (hakuna fixed price) na pia pasiwe na kipengele cha kutupangia kiasi cha kuuza nje ya soko lao bila kusahau kusiwe na masharti ya upande wao TU pale tutapokiuka masharti ya kuwauzia wao na sio pale kutapokuwa na any default kutoka kwao inayoweza kutishia mauzo ya gesi yetu nje ya wao.

MKUU!

Mbona kwa hili tulishachelewa!!! watu walishavuta na ziko Uswisi kilicho bakia ni kuuza kwa bei sawa na bure mkuu!!!!!
 
BTW, wala siyo hiyo mikataba tuu ambayo inafichwa maana serikali pia imegoma kuonyesha Mitaala ya Elimu hapa nchini. Tanzania ni member wa Open Government Partnership lakini tunaficha mpaka Mitaala ya Elimu hapa nchini? Tell me about that.

Ebana eeh, vipi kuhusu mishahara ya viongozi kuanzia rais on down? Unaijua? Staki unambie niende idara ya utumishi maana huko nahisi najua tu jibu ntakalolipata...
 
Mkuu mawazo yako ni mazuri and I wish ingekuwa hivyo katika ulimwengu wa Ukweli.

1. Mimi na wewe tunakubaliana kuhusu reduction, refer post zangu zote( Isipokuwa wewe umeiita reduction, na mimi nimeiita Talking points)

2. Hata Nchi ambazo freedom of Information iko juu na inaheshimika kama uingereza, inapokuja kwenye Mikata ya kibiashara huwa wana refuse kutoa Information. Sasa sijui wewe ndugu yangu una mfano wa nchi gani.

3. Article yako nimeisoma lakini, It doesnt make sence in legal and commecial world.Google UNCTAD uangalie wanasema nini kuhusu confidentiality.Wana Documents nyingi tu na nimekuwekea moja hapa jamvini.
hiyo article hai support unachokisema kwenye post zako. Isome uielewe.
Inapokuja kwenye mikataba inayodhuru Public interest, hawa-support huo usiri unaousema, wanai-turn down mikataba ya aina hiyo. Kwa hiyo hauwezi kufananisha na hapa kwetu, kwa hiyo article yako haitusaidii sisi kwa aina ya viongozi tulionao.
 
Back
Top Bottom