Nitumie fursa hii kuwapa wasiojua utawala wa CHADEMA ulivyoanza kabla ya Mbowe na uhusiano wa viongozi wake.
Mtei
Ni muanzilishi na Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA, alikuwa gavana mkuu wa benki kuu (BOT) na Waziri wa Fedha kipindi cha Nyerere.
Bob Makani
Huyu alikuwa mwenyekiti wa pili wa CHADEMA ambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa Mtei alipokuwa gavana msaidizi wa benki kuu (BOT). Aidha marehemu Bob Makani alimuoa dada yake Mtei ambaye alizaa nae watoto kadhaa.
Mbowe
Huyu aliwahi kufanya kazi benki kuu pamoja na Mtei na Bob Makani, hivyo walianza kufahamiana huko.
Mbowe baadae alimuoa mtoto wa Mtei ambaye amezaa nae watoto kadhaa. Hii ilichangia pakubwa Mbowe kupata uenyekiti wa kwanza wa BAVICHA kabla ya kuwa mwenyekiti wa 3 wa CHADEMA. Ili kuhakikisha Mbowe anakuwa mwenyekiti wa milele, CHADEMA kwa amri ya Mtei (Mkwe wa Mbowe) ilibadilisha katiba yake mwaka 2002 kutoka kwenye ukomo wa kugombea mihula 2 tu kwa mwenyekiti mpk bila ukomo.
Ndoa ya Mbowe na mtoto wa Mtei iliingia kwenye misukosuko pale ambapo Mbowe alianzisha uhusiano wa siri na dada mmoja ambaye baadae alimhonga ubunge wa viti maalum, aitwaye Grace Mukya na kuzaa naye mtoto mmoja wa kike, lkn kuishi naye km nyumba ndogo.
Mbowe na Mtei walimshawishi Dk. Warid Aman Kaborou kuhama kutoka Marekani kuja Tanzania ambaye alikuwa mhadhiri wa muda mrefu kwenye vyuo mbalimbali vya USA.
Walimuahidi kumpa fedha taslim, gharama za kuhama yeye na familia yake mpk Tanzania lkn kumfanya katibu mkuu wa CHADEMA, walfanikiwa na Dk. Kaborou akawa katibu mkuu wa CHADEMA, walimnunua.
Ni wazi kabisa uongozi wa CHADEMA ni wa kiukoo.