Hakuna andiko la moja kwa moja linalosema sabato ni jumamosi.Biblia imetaja siku ya maandalio,inafuata sabato,inakuja siku ya kwanza baada ya sabato(Luka 24:1).Biblia ya kiswahili Cha kisasa iliyotafsiriwa kwa ushirikiano wa wakatoliki kwa waprotestant INASEMA Yesu alifufuka alfajiri ya jumapili baada ya sabato(Luka 24:1),Kiswahili Cha zamani inasema hiyo ni siku ya kwanza ya juma.Siku aliyokufa Yesu biblia inasema ni siku ya maandalio na sabato ikaanza kuingia,wakitoa mwili,wakaenda kuuzika,kisha wapumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa(Luka 23:52-54). Kiswahili Cha kisasa inasema siku hiyo ilikuwa ijumaa na sabato ilikuwa inaingia.Kama wiki Ina siku 7,jumapili ni siku ya kwanza,ijumaa siku maandalio ya sabato,na sabato ni siku ya saba,haihitaji elimu ya chuo kikuu kufahamu siku ya 7 ni ipi.Quran yenyewe ndo imetamka waziwazi,sabato ni jumamosi,siku tukufu,yenye hishima(Quran 4:154,7:163,2:65,16:124).