MIRA01
JF-Expert Member
- Sep 18, 2023
- 319
- 695
Nafikri, wanaapa ili iwasaidie kulinda uaminifu wao kwa Mungu katika kushika Sheria zake hasa ya sabato.
Huku wamesahau kwamba Neno la Mungu linasema usiape kwa chochote.
Huku wamesahau pia kuwa kama unategemea torati, umelaaniwa kwa sababu huwezi kuitimiza:
Wagalatia 3:8
Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.
Wagalatia 3:9
Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.
Wagalatia 3:10
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.
Wagalatia 3:11
Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
Asante kwa ufafanuzi zaidi! Hope hakuna muadventista msabato anayeweza kutoka kwenye hoja kama hizo akaja na majibu nimeuliza kwa waumini nikakosa makini nikapanda kwa wainjilisti nako nikakosa nikasogea pia kwa wachungaji wa kisabato napo hapakuwa na majibu so nini kimejificha zaidi kwenye imani hii ya seventh day adventist ?
Bado nakosa majibu ya maswali kadhaaa
Moja wapo ni kupinga kuweka alama za vitu kwenye dhehebu hili japokuwa wameweka kwa siri tena yazidi hata walioweka wazi?
Tazama nembo ya kanisa la wasabato kuna msalaba uliogeuzwa chini juu na hii inaonyesha miungu ya kale ya misri yaani mungu baal
Lakini pia watapinga hilo lakin bila majibu, mwanzo hawakuwa wanaweka msala kwenye nembo hizo na hata makanisa ya kiadventist wasabato wanawek msalaba kuelezea kwamba ni kanisa na wanapinga hilo la msalaba
Lakini kwenye nembo wameweka msalaba wa siri wenye maana nyingine tofaut na kawaida ya msalaba wa kristo
Kipi wanachoficha nyuma ya pazia kwenye dhehebu hili lenye kujiaminisha kwamba ni kanisa teule na kusahau kwamba kanisa (hekalu) ni mwili wako na Mungu akaaye ndani yako?
Kiukweli napata ukakasi zaidi kuona na kuambiwa nikiwa masabato basi nina ticket ya kwenda mbinguni huku mafundisho tu yanakinzana pakubwa na biblia yenyewe