China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Kuhusu bidhaa zinazolipa, naweza kusema bidhaa yoyote inalipa ISIPOKUWA inategemea tu na soko lako ulilolikusudia likoje huku nyumbani Tanzania.
Cha muhimu ANZIA SOKONI ndio uende kiwandani. Hakikisha unajua soko linataka nini kwa muda husika.
Kwa hali ya sasa ya kiuchumi Tanzania, sishauri sana (mtazamo wangu) kwa anaeanza biashara aingie kwenye bidhaa za fasheni na urembo kama nguo na mikoba au viatu.
Kwa sasa "purchasing power" ya watanzania wengi imeshuka kwenye bidhaa za nguo, viatu na mikoba.
Mabadiliko ya kiuchumi, watu wengi wameanza kujiongeza na kufikiria kuwekeza kwenye ujasiriamali mdogo mdogo.
Kwa hiyo kwa sasa ukiuza bidhaa ambayo itatatua changamoto za watu basi utakuwa umejihakikishia soko lako. Kwa mfano: sasa hivi wajasiriamali wadogo wamejikita katika kilimo, ufugaju na usindikaji. Pia wamejikita katika kuongeza thamani ya bidhaa ambazo zimeshazalishwa. Kwa hiyo ukija na bidhaa mfano packaging materials utauza sana kwa sababu hiyo ni moja ya changamoto ya wajasiriamali wengi hawana parking materials kwa ajili ya bidhaa zao. Kwa hiyo utakuwa umetatua matatatizo ya wengi na unaweza ukawa general supplier mikoani (usifocus DSM tu, angalia pia mikaoni).
Bidhaa za nguo na fasheni watu wamepunguza kuvaa "vyuma vimekaza"[emoji16] unless labda utumie mbinu ya kukopesha [emoji16] ambayo nayo ni risk sana na mtaji unaweza ukazama huku unajiona!
Kingine kuhusu bidhaa za nguo na mikoba ni kuwa biashara hiyo inaendeshwa kwa nguvu ya fashion iliyopo, hivyo unaweza kununua mzigo china, mpaka unafika TZ (Kama ni meli umetumia siku 45 hivi) unaweza kukuta nguo au mikoba uliyoleta iloshaingia kariakoo kitambo (wakati mzigo wako ukiwa majini) na bei haipo kama ulivyotarajia, mwisho wa siku unajikuta unauza kwa hasara.
Pia ni muhimu kujikita kwenye biashara ambayo ushindani wake si mkubwa . Biashara ya nguo na mikoba ipo kila baada ya nyumba kadhaa. Kuna maduka ya madera, viatu kila kona! Shangwe za kuvaa siku hizi sio kiviiiileeee...hali si hali.
Biashara ya nguo na viatu ukiwa wewe ndio unaanza itakulazimu ushushe bei uweke "penetrating price" ili uweze kuingia sokoni vizuri mana tayari sokoni kuna wenzio ambao wapo kitambo, unless wewe uje na kitu cha kipekee sana.
Kuhusu usafirishaji, hiyo ni moja ya taratibu lakini binafsi nashauri uwe na mtu kule ambaye atasimama katikati yako na muuzaji ili kuondoa risk mana wachina nao si wote wa kuwaamini. Kuwa na mtu alieko kule yeye akague bidhaa kiwandani, kisha malipo fanya mwenyewe kwenye akaunti ya muuzaji (ambayo iko secured na incase of anything unaweza kuclaim refund na hela yako ikarudi mf. kupitia paypal/alibaba trade assurance nk nk) kisha mzigo ukifika kwenye Ghala la wasafirishaji basi huyo mtu wako aende akaukague na ajiridhishe kuwa ndio ule ule alioukagua kiwandani)
Kuhusu Bankok sina uzoefu napo. wenye uzoefu na huko wataongezea.
NB: Ni maoni yangu tu na yanaweza yasiwe mujarab kwa wengine
 

Mkuu nashukuru kwa majibu mazuri. Nakubaliana na wewe purchasing power imeshuka sana watu wanatumia pesa kwenye 'needs' kuliko 'wants'. Hilo la packaging pia niliwahi kulifanyia upembuzi haswa kutengeneza mifuko ya karatasi lakini nikagundua mashine nyingi zinapatikana india na ni za pesa ndefu zaidi ya $60k. Sijui hapo kwenye vifungashio kama una abc za kushea.
 
Kwenye suala la mashine ni kweli, mashine zipo ghali na hata sisi tunaozileta huku Tanzania, bado watanzania wanataka mashine NZURI ila za bei rahisi kitu ambacho hakiwezekani 100%.
Watanzania tunapata tabu moja kwenye "kuyatoa maisha"! Yaani kila mtu anataka aminyane yeye kama yeye yaani peke yake ili atoke! Vijana wa nchi zilizoendelea/makampuni makubwa yaliyoendelea yalianza chini lakini baadae yaliunganisha nguvu, yaani mfano mwenye wazo la biashara aliunganisha nguvu na mwenye mtaji wa pesa, mwisho wa siku wote mnatoka. Wengi bado tuko nyuma katika kuamini vitu kama patnership (inayotambulika kisheria) na sio ya "kishkaji"! wengi hawaamini kwa kuwa flani na flani walifanya kisha wakadhulumiana! kwa hiyo kila mtu anatoa mfano huo ambao labda ukiangalia haukuwa hata na mikataba ya kisheria nk.
Kwa hiyo nitoe wito kwa vijana KUUNGANISHA NGUVU ya pamoja kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo ili kuweza kumudu kununua hizo mashine ulizosema nk.
Packaging ni mfano tu nimetoa lakini vipo vimashine vidogo vidogo ambavyo unaweza kwenda china ukanunua na ukaja navyo ukauza kwa bei ya kawaida na ukawa mkombozi kwa wengi na pia hata wewe mwenyewe badala ya kuziuza lakini ukaamua kuzitumia. mfano wa mashine (small scale):
1. Mashine ya kusaga vitu vikavu kama viungo
2. Mashine za kukamua mafuta
3. mashine za kubana mifuko
4. mashine za kushona viroba
5. mashine za kupalilia
6. mashine za kupukuchua mazao ya nafaka kama mahindi, mtama, maharage nk
7. Mashine za kuvuna mpunga nk.
8. mashine za kuponda unga wa ngano
9. Mashine za kuchanganya vyakula vya mifugo
10. Mashine za kusaga/kukata majani kwa ajili ya mifugo
11. vyerehani vya umeme
12. mashine za kukoroga sabuni
13. Mashine ya kuprint label kwenye vifungashio

Pia unaweza kuuza vigungashio ambavyo tayari vimeshatengenezqa kama mifuko, chupa za aina mbali mbali nk. ukizinunua hizi china kutoka kiwandani moja kwa moja na kuzileta Tanzania utauza sana tu hasa hasa kama utanunua na kisha ukija Tanzania unatengeneza label kulingana na mahitaji ya mteja ili mteja auze bidhaa yenye brand name yake. Tsh 10M ni mtaji mkubwa saba kama utaamua kuwekeza kwenye hili la vifungashio.
 
Habari!nahitaji mshine ya kukamua mafuta ya alizeti na peanuts medium size,je naweza pata bei gani mpaka hapa Bongo?
 
Habari!nahitaji mshine ya kukamua mafuta ya alizeti na peanuts medium size,je naweza pata bei gani mpaka hapa Bongo?
mkuu, asante kwa swali. ili uzi huu tusiuchanganye kidhima, nashauri ubakie kama ulivyo uwe ni ushauri tu tena wa BUREEEEEE na nitaendelea kuutoa BUREEE kadri MUNGU atakavyoniwezesha. Kuhusu mashine hizo ulizouliza na nyingine naomba ingia kwenye hii link hapa utaona
Niulize kuhusu mashine za ujasiriamali na upatikanaji wake
 
Mnaojibu kwa tag thread nzima nzima mnaudhi bhnaa
 
NSamahani nlikuwa naomba kwamba natawezaje kuanza biashara hiyo na process inakuaje kwa sababu naamini ni fursa nzuri kwa upande wangu...!!
 
kama umesha wahi fanya biashara yoyote kuchukua mzigo china na kuleta TZ, naomba mrejesho wa garama na changamoto
 
nami nasubiri...japo mkuu hujaainsha ni aina gani ya biashara ili wachangiaji watoe data vizuri!
 
kama umesha wahi fanya biashara yoyote kuchukua mzigo china na kuleta TZ, naomba mrejesho wa garama na changamoto
Mkuu naleta kila siku mizigo Tanzania. Gharama nimeeleza hapo juu mwanzo kabisa wa uzi huu. Changamoto pia zimejadiliwa sana humu ndani. Tafadhali chukua muda kupitia huu uzi kuanzia mwanzo hadi mwisho na naamini hutajuta bando lako utakalitumia. You will never be the same ! utapata cha kujifunza na majibu ya maswali yako
 
Huu uzi nimeusoma kwa wakati muafaka.Nataka kufungua shop la kuuza phone accessories&phone but nataka niagize kutoka China.Sina uzoefu hata kidogo nimesoma nimepata primary information lakini najiona bado nina inferior
 
safi
 
Huu uzi nimeusoma kwa wakati muafaka.Nataka kufungua shop la kuuza phone accessories&phone but nataka niagize kutoka China.Sina uzoefu hata kidogo nimesoma nimepata primary information lakini najiona bado nina inferior
soma tena
 
Mkuku sasa sisi wengine sio wapenzi wa safari kivile na tunatamani kuagiza baadhi ya vitu kutoka china ila sasa confidence level ni ndogo hasa kutokana na ukweli kamba bado hatuna uzoefu.Nimewahi fanya window shopping kwenye tovuti mbalimbali za china ningependa kufahamu iwapo mtu anaweza agiza mzigo wake online tokea china na akaletewa kama ambavyo tunafanya na magari kwenye hizo local offices zao

Asante
 
Ndio mkuu unaweza kuagiza na mzigo kukufikia ulipo. Pitia comments za wadau kuanzia mwanzo, michango ni mingi sana inayoelezea hilo. ukishindwa kabisa nitafute nitakusaidia kupata unachohitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…