Mkuu
Kipilipili, mimi nilikuwa Shaghai wakati wa CIP. Nilipitia pale kwenye soko lao la mnada nikachukua Laptop HP nane ambazo nilinunua kwenye 900 UAN kila moja. Nikipiga hesabu kwa madafu haikuzidi laki sita ila nilipokuja Bongo nilipata faida ya almost laki nne kwa kila laptop...Pia nilichukua iphon 7 na Samsung kadhaa ambazo airport vyote vilipita free...Nakuja huko mwezi wa pili nataka nifanye kabisa biashara ila nikiwa tayari na masoko kwa wanafunzi nk. Pia nataka nilete flight camera niziuze kwa wanahabari.
Vipi unaonaje soko la Shanghai kwa hizo bidhaa?
Una ushauri wowote wa bidhaa nyingine nzuri ambazo naweza kuchukua mbali ya hizo?
Ikibidi nikifika tuwasiliane mkuu ila nipe kwanza ushauri!